Mabadiliko haya TRA aliyoleta Rais Magufuli hata aondoke leo yatadumu milele

Magufuli is a president for life nani amesema ataondoka Leo au kesho?
 
mawazo mazuri sana haya mhusika lazima atayapata hebu tuyafanyie kazi tutoke hapa tulipotusonge mbele
 
Kuna jambo moja unapaswa kulijua, watanzania wengi wana nunua vitu wanavyo lipia VAT kuliko kuuza vitu vingi wanavyopaswa kukusanya VAT kwa niaba ya TRA.
Kuna hatari serikali ikajikuta inadaiwa madeni makubwa na raia ukisema watu wa kawaida sio bishara au kampuni wa-file VAT returns.

Kiujumla wake umetoa hoja na ushauri mzuri kwakweli.
 
Kama ajasajiliwa na VAT atadaije serikali.
Anaye claim VAT refund ni mtu aliyesajiliwa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa nazani anamaanisha return za income sio vat
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapongeza ,Unashauri,Unakosoa
Hii ndio Maana Nzuri ya Kuipenda nchi yako
Safi sana Ndugu huu ni Ushauri mzuri sana
Naimani wahusika wataupokea
Kama watasoma hii thread...
 
Mkuu kila mahali watu wanalalamika biashara hazitoki, Unemployment rate i am sure itakuwa inacheza above 12% maana kenya leo wametoa 10.8%

Sasa sijui ngombe akikamuliwa sana mwisho wake atafariki. Mkuu on the ground hali inatisha na huu ndio mwaka tulizoea wa uchaguzi labda vyuma vingepakwa grisi.

Mkuu wauza mihogo wameongezeka sababu ya kusaidia mlo kuwa mkuu. Unapiga mihogo ya kukaanga mpaka jioni.

Kodi zikizidi itakuwa hatari. Moja ya sababu za kuwa na NIda ID ni kutekeleza hayo uliyoyaongea. Ila wasisahau wao wako kwenye ma landcruiser V8 full viyoyozi sisi tunaitafuta corona kwenye mwendokasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Janja PORI umedadavua vizuri pia umekosoa,umeonya,umeshauri na umesifia.

Pia ungegusia na suala la ajira...kuwepo na balance hata watoto wa vigogo na wa wakulima/wafugaji wagawane Keki ya Taifa.

Kwa sababu:-

1: Kuna vijana huku mtaani wamehitimu Uhasibu more than 2years hawana ajira,wanazurura tuu na kukaa vijiweni.

2: Inasadikika ajira za TRA ni za kibaguzi,yaani kujuana.Vipi kuna uhalisia kwenye hili????? Na kama sivyo ni hatua gani mnachukua ili kuwapa ajira wale tunaowaona maofisini wakati tukilipa kodi.

3:Na pia Ajira za TRA hazitangazwi,hapa inakuaje?? Sasa hivi kuna system inatumika ndani ya TRA inaitwa Interns hii inakaaje???! Na jee? Vijana wale wa kitanzania wote wakimaliza mtawaajiri?na kama baadhi ya hawata ajiriwa si litakuwa ni suala la kupoteza muda wa vijana wetu???


Naamini mkuu Janja PORI wewe ni mtaalamu wa masuala ya uchumi na msomi mzuri,Hivyo sasa kwa busara zako ningependa kuona mchango wako kuhusu hili uliwa kama Expert member wa humu.

NAWASILISHA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mzuri... Tatizo sio kukusanya mapato tatizo Ni matumizi...
TRa wanazidi kuongeza mapato lakini huku mbagala Ni heri ya jana kuliko leo... Sijui kesho Corona itakuwaje..
 
Huu ndo aina ya nyuzi tunazotaka humu.
Kwa kweli kuna umuhimu mkubwa mno wa tax base kuongezeka ili walau kila mwananchi anayepata chochote atoe return kwa mamlaka za nchi.

Lakini pia kuna umuhimu sana kusimamia na kuhakikisha kila kinachopatikana kinatumika vizuri kwa ajili ya wote.

Sasa hapo ni muhimu sana kwanza kulifanya suala kulipa kodi kama utamaduni au ibada. Pili tujifunze kuchagua viongozi waadilifu,wazalendo,wasio na tamaa,wabunifu na walio tayari kuitumikia nchi kwa uaminifu.
Tukikusanya kodi kwa mafanikio na bado tukawa na viongozi wa hovyo juhudi zote zinakuwa HOVYO na BURE.
 
mkuu naona unatatafuta ugomvi na wakna tunda la masiara[emoji38]-jokes

Kiukweli mkuu umeongea jambo la maana sana unastahili pongezi!

Kama ulivyosema utoaji wa kodi uwe ni kama ibada ni kweli kabisa sipingani na wewe..na hii pia itapelekea uchumi wa Taifa kugrow zaidi.

NIMEYAPENDA MANENO YAKO ya“Pili tujifunze kuchagua viongozi waadilifu,wazalendo,wasio na tamaa,wabunifu na walio tayari kuitumikia nchi kwa uaminifu. ” sio viongozi tuu! Hata watendaji wa mamlaka yenyewe wapatikane watu wachapa kazi,waadilifu na wasio na tamaa Taifa litafika eneo..

Japo sina evidence za kutosha na zozote za Maofisa wa TRA,lakin suala la uadilifu na uaminifu kutokuwa na tamaa ni suala muhimu sana katika hii sector.Na ndio maana mchujo wa kuingia kwenye hizi mamlaka na kuwa mfanyakazi ni ngumu sana achilia mbali na yasemayo kuwa mamlaka hii kipindi cha nyuma ilifanya shughuli zake kwa kujuana hususani kwenye soko la ajira.

Lakini pia mkuu suala la kula keki ya taifa ni la kila mmoja wetu! Hivyo kama ulivyoshauri kuwa-“Lakini pia kuna umuhimu sana kusimamia na kuhakikisha kila kinachopatikana kinatumika vizuri kwa ajili ya wote.”

ni muhimu sana kwa ajili ya nchi yetu na tuzidi kulijenga TAIFA.

NAWASILISHA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KALIPE KODI TUJENGE TAIFA, LAZIMA TUWE NA STANDARD YA WENZETU, SIO NCHI UNA BIASHARA YA BILLION UNALIPA LAKI 2 A WENGINE NDO WANAUMIA
Dogo umetoka chuo juzi, bado una mihemuko ya ajira mpya, ukikua utajua kuwa mfumo mzuri wa TRA unategemea pia mifumo mingine,

Unaua sekta binafsi ambayo ndo engine ya uchumi alafu eti unaimarisha mifumo ya kodi hiyo kodi utatoa wapi? Acha kuwadanganya wajinga
 
Deni LA taifa limepaa mpaka tril.58.
Maana yake hiyo no indicator kuwa uchumi wetu umekufa, biashara zimekufa, maana yake hat ukiwa na mifumo mizuri ya kodi huwezi kupata kodi, kukopa Sana ni dalili ya kutokuwa mapato yanayo kidhi matumizi

Usidanganye tupo kwenye kipindi kigumu sana. Hiyo mifumo mizuri ya kukusanya kodi haitusaidii kwa sasa. Ikiwa hakuna walipa kodi

Tuko kwenye janga LA korona. Tumepoteza biashara ya utalii tumepoteza biashara ya airline mahoteli yamefungwa, sasa TRA na mifumo yao mizuri watatoa wapi kodi,?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…