Mabadiliko haya TRA aliyoleta Rais Magufuli hata aondoke leo yatadumu milele

Mabadiliko haya TRA aliyoleta Rais Magufuli hata aondoke leo yatadumu milele

Mkuu Janja PORI umedadavua vizuri pia umekosoa,umeonya,umeshauri na umesifia.

Pia ungegusia na suala la ajira...kuwepo na balance hata watoto wa vigogo na wa wakulima/wafugaji wagawane Keki ya Taifa.

Kwa sababu:-

1: Kuna vijana huku mtaani wamehitimu Uhasibu more than 2years hawana ajira,wanazurura tuu na kukaa vijiweni.

2: Inasadikika ajira za TRA ni za kibaguzi,yaani kujuana.Vipi kuna uhalisia kwenye hili????? Na kama sivyo ni hatua gani mnachukua ili kuwapa ajira wale tunaowaona maofisini wakati tukilipa kodi.

3:Na pia Ajira za TRA hazitangazwi,hapa inakuaje?? Sasa hivi kuna system inatumika ndani ya TRA inaitwa Interns hii inakaaje???! Na jee? Vijana wale wa kitanzania wote wakimaliza mtawaajiri?na kama baadhi ya hawata ajiriwa si litakuwa ni suala la kupoteza muda wa vijana wetu???


Naamini mkuu Janja PORI wewe ni mtaalamu wa masuala ya uchumi na msomi mzuri,Hivyo sasa kwa busara zako ningependa kuona mchango wako kuhusu hili uliwa kama Expert member wa humu.

NAWASILISHA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja nzuri sana ntarudi kwako
 
Hujui rafiki Yangu ,rais akiondoka ataondoka na kila kitu chake,maana anavyotupeleke yeye siyo asili ya watanzania wengi,sisi hadi tusimamiwe,angalia mifano midogo kwenye jamii unayoishi utanielewa,we angalia mfano tamaduni wetu wakusafisha mazingira ka kuna mgeni anakuja
 
Bado kuna tatizo la account examination na uhalisia wa mahesabu. Wafanyabiashara wameumia sana kutokana na hili.

Mfano: upo china, mmejipanga watu 20 mmejaza container la bidhaa. Mmoja wenu anawaona door to door wawaletee mzigo, mnawalipa as a group kulingana na ukubwa wa mzigo.

Mzigo unaingia unakatwa kodi kwa pamoja, unafikishiwa wa kwako dukani kwako na door to door, stock yako inaongezeka, mkaguzi anaingiza stock kwenye hesabu.

Miaka miwili au mitatu inapita, Tra wanafanya examination ya hesabu, wanagusa stock then wanaona una stock kubwa purcheses haionekani uliyolipia VAT kwa sababu mliingiza container lenye bidhaa tofauti tofauti na sehemu yako ya mzigo ni ndogo tu, na Tin yako pale haipo.

TRA wanakulima kodi kwa hoja kuwa inawezekana umetempt around na purcheses zako ili kudanganya faida,

ukijibu hoja wanaikataa kwa kuwa huna reliable evidence, hujakaa vizuri upambane upate angalau evidence assessment inatoka, kuappeal unatakiwa ulipe 1/3, hujakaa vizuri account inafungwa. Hili ni tatizo.

Halafu kuna tatizo jingine. Sijalipa Mfano SDL sahihi, ni human error za kawaida hizi, TRA niliwapa hesabu kwa wakati ila wao wanakaa miaka mitatu ndo wanafanya examination halafu examiner ananipiga interest and penalty ya miaka mitatu.

Kama mm nilikupa hesabu wakati sahihi kwann ww ufanye examination miaka mitatu mbele halafu unipige interest na penalty kwa miaka yote uliyokaa na hesabu zangu bila kufanya examination?
Halafu majibu yanakuwa mepesi tu kuwa appeal au omba usamehewe hizo adhabu.

KAZI N NZURI YA KUKUSANYA KODI ILA KAMA TAIFA TUNAHITAJI KUWEZESHANA NA KUANGALIA UHALISIA WA BIASHARA KABLA YA KUMPA MTU KODI.
 
Back
Top Bottom