Mabadiliko Jeshini: Mpambe wa Rais apandishwa cheo na kupangiwa kazi nyingine, Kanali Mulunga awa mpambe mpya

Nasikia ADC mpya ni Msukuma, hadi sasa major general 5 Wasukuma.......Wasukuma mwaka wenu huu.....
 
Kumbebea makabrasha raisi ,kumshikia mwamvuli pindi mvua ikinyesha,kwenda kuchukua karatasi na kumpa rais atie saini na kama kuna mzigo anabeba ..msaidizi wa raisi
Ni kweli. Ila kuna lingine kubwa zaidi ya hayo.
 
Wadau kwahiyo mlitaka afande Mkelemi aendelee kuwa ADC! Mungu anawaona jaman khaaaa. Ile kazi iskieni tu jaman muoneeen huruma mwenzenu akapumzike
 
Kanali mkelemi sio tena ADC wa mukulu,anakuja kanali mwingine" sawa, kwani ukiwa brigedia general huwezi kuwa ADC wa presidar?
Wanaofahamu mambo ya inteligencia watujuze
cc. Brother GENTAMYCINE,na wengineo
Hata Rais wa Zanzibar yeye anapambiwa na Luteni Kanali na si Kanali. Hayo ni mambo ya itifaki, na Brigedia mtu mzito, mpaka gari yake inavaa nyota !
 
Hivi CDF huwa anateuliwa kutoka kwenye rank ipi ya jeshi?
Kwa kawaida Brigadier, Major na Luten General anaweza kuwa CDF

Mara nyingi, Luten General ndio anakuwa kwenye nafas nzur ya kuwa CDF kutokana na seniority

Hata hivyo, Rais anaweza kuteua yoyote kati ya General niliyetaja hapo paragraph ya kwanza baada ya kupitia hatua mbalimbali za uteuzi
 
dah awamu ya vurugu mechi "ZINDUA" , "TEUA","TUMBUA" tutafika 2025 tumechoka kweli kweli!
2025? Kwa nini?
Hujui kuwa kuna uchaguzi 2020 lakini pia kuna tendo la hiari 26042018 ana option ya Ku step down
 
Hilo neno "mpambe" lina ukakasi mjue?
Maana tunaambiwa na wahenga "MPAMBE NUKSI" sasa sielewi wanavosema ati "mpambe wa Rais"
 
Mwambata wa kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania - Abuja. It is self-explanatory Mkuu.
Sasa "mwambata" inajiexplain vp apo?
Viswahili vyenu vya BAKITA havieleweki!
Codify the language na sio kujitungia misamiati kutokana na akili zenu finyu
 
Atakua anamaanisha "Nchi Jirani"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…