Mabadiliko Jeshini: Mpambe wa Rais apandishwa cheo na kupangiwa kazi nyingine, Kanali Mulunga awa mpambe mpya

Mabadiliko Jeshini: Mpambe wa Rais apandishwa cheo na kupangiwa kazi nyingine, Kanali Mulunga awa mpambe mpya

Nimemwomba Mh. Rais....
Nimemwomba Mh. Rais.....
Nimemwomba Mh. Rais....
Kwani hawezi kufanya teuzi bila kumwomba Huyo...?
You recommend as a CDF and the President approve since he is the Commander in Chief to the little of my knowledge thanks!
 
Kanali mkelemi sio tena ADC wa mukulu,anakuja kanali mwingine" sawa, kwani ukiwa brigedia general huwezi kuwa ADC wa presidar?
Wanaofahamu mambo ya inteligencia watujuze
cc. Brother GENTAMYCINE,na wengineo
Hili mkuu liliandikwa jukwaan ,,wanaokuwa ma ADC huwa ni wenye cheo cha kanali tu.
Ndo utaratibu wakuu waliouweka.
Kanali ukipandishwa cheo basi unapangiwa kazi nyingine.

Mkelemi ni mtiifu sanaa na nilitokea kumkubali sanaaa.
Saluti kwako Afande.
 
Kila cheo jeshini kinakua na majukumu yake mfano afisa mteule (Non-commisioned officer NCO) ndo hua anakua RSM (kiongozi wa nidhamu jeshini-kwa maafisa wadogo).
ikitokea akapewa kamisheni na kua afisa hawezi kuendelea na cheo hicho.
hujo Mkelemi hawezi kuendelea kuwa bodyguard kwa sababu amekua afisa wa juu. afisa wa juu hawezi kuwa body guard.
Kimsingi yule anayevaa nguo za kijeshi anakuwa na rais muda wote sio bodyguard kiswahili ni mpambe wa Rais anakuwa pale kwa sababu rais ni Amiri jeshi Mkuu wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama ,walinzi wa rais ni kikosi maalum cha ulinzi kwa sisi Tanzania nafikiri kina ukubwa wa watu mpka 36 wanaopena majukumu ya kumlinda rais muda wote
 
Wakurya teuzi hizi sijasikia majina yetu kama zamani.mfano Majenerali hawa,Gimonge,Marwa,igoti,chacha,Waitara,Rioba,isamuhyo,Kiaro,nk.walioteuliwa kachape kazi kwa taifa tunawategemea.
 
Mkuu wa wilaya kafanya nini?
Sija muelewa Mobeyo! Ndio karudi kutumikia jeshi na cheo kipya ama ndio kamshusha?
26042018 [emoji38] [emoji38]
 
Kuwa bodyguard wa rais vs kuongoza brigade! Ipi ni nyadhifa kubwa kuliko nyingine?
Duh! Mkuu! Hilo halihitaji hata kuuliza. Chulia scenario hii; Rais, yaani Amiri Jeshi Mkuu, akiamua kubadilishana mawazo/kuongea na makamanda wa vikosi (mabrigedia and above) wewe umebeba mikoba yake tena kimya wala huruhusiwi kutia neno wakati makamanda wakitoa options kwa Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa scenario hiyo ndogo common sense tu inaonesha ni ipi nyadhifa kubwa. Cheo cha kijeshi kikishakuwa na neno "General" hiyo ni level nyingine Mkuu - Brigadier General; Major General; Lieutenant General; and General ambao kimsingi wanastahili za kuwa na wapambe pia na diplomatic passports kama sijakosea.

Makanali ndio kazi zao kuwa wapambe wa viongozi na sio majenerali; kama iliwahi kutokea ni kwa bahati mbaya sana.
 
Kwa nini msijibu hizi hoja za msingi? Huyo mkuu wa wilaya alikuwa mjeshi kabla hajapewa hicho cheo cha kisiasa ambacho ni kada wa ccm, sasa amerudishwa jeshini kuendelea na utumishi, je huku sio kuchanganya jeshi na siasa?
 
Kuwa bodyguard wa rais vs kuongoza brigade! Ipi ni nyadhifa kubwa kuliko nyingine?
Ulinzi gani wakati msaidizi wa rais ,anambebea makabrasha na vitu na kukaa nyuma yake tu kama adc ..walinzi ni yule anayekaa upande wa kulia akiangaza macho(kiongozi wa walinzi ana earphone) na wengine waliovaa suti na earphone na siku hizi kuna makirikiri

Brigadier anayeongoza brigedi ana heshima na cheo kuliko mpambe ,msaidizi na mbeba viatu vya rais

Maswali mengine bwana alikuwa kanali kapandishwa cheo cha juu kuwa brigadier jenerali na kwa cheo hicho cdf anasema apangiwe kazi nyengine yenye hadhi hiyo ya upambe haimfai.halafu unakuja ww unaanza kuropoka eti brigedi ya jeshi haina hadhi kuliko upambe ..

Ina maana ww mjuzi kuliko cdf ??/
 
Kwa nini msijibu hizi hoja za msingi? Huyo mkuu wa wilaya alikuwa mjeshi kabla hajapewa hicho cheo cha kisiasa ambacho ni kada wa ccm, sasa amerudishwa jeshini kuendelea na utumishi, je huku sio kuchanganya jeshi na siasa?

Na hata wakijibu wanakuwa wakali kama nini ,au ndio kina Mabeyo mpo huku ?.

Tunaomba Majibu tafadhali ...
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Aprili, 2018 amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika vyeo mbalimbali.

Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Paul Massao kuwa Luteni Jenerali.

Meja Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli (TMA) na kwa uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa na Luteni Jenerali wawili.

Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Brigedia Jenerali Henry Kamunde kuwa Meja Jenerali.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 27 wa JWTZ kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali na Afisa 1 kutoka Luteni Kanali na kuwa Kanali.

Waliopandishwa vyeo hivyo ni D.D.M Mullugu, J.J Mwaseba, A.S Mwamy, R.K Kapinda, C.D Katenga, Z.S Kiwenge, M.A Mgambo, A.M Alphonce, A.P Mutta, A.V Chakila, M.G Mhagama, V.M Kisiri, C.E Msolla na S.M Mzee.

Wengine ni C.J Ndiege, I.M Mhona, R.C Ng’umbi, S.J Mnkande, A.C Sibuti, M.M Mumanga, I.S Ismail, M.N Mkeremy, G.S Mhidze, M.A Machanga, S.B Gwaya, P.K Simuli na M.E Gaguti.

Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Luteni Kanali Bernard Masala Mlunga kuwa Kanali na ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais (Aide de Camp – ADC)

Kanali Mlunga ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mbaraka Naziad Mkeremy ambaye amepandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

12 Aprili, 2018
 
Kwa nini msijibu hizi hoja za msingi? Huyo mkuu wa wilaya alikuwa mjeshi kabla hajapewa hicho cheo cha kisiasa ambacho ni kada wa ccm, sasa amerudishwa jeshini kuendelea na utumishi, je huku sio kuchanganya jeshi na siasa?

Wakikujibu naomba unitag please
 
Back
Top Bottom