Mabadiliko makubwa ya viongozi wa serikali yakamilika; yatawagusa pia viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama

Mkuu inaonekana una imani na bunge. Kama wabunge wanapatikana kwa maagizo ya rais unategemea kuwa na bunge la kufanya maamuzi sahihi? Mfano hili suala la bandari umeona bunge likifanya lolote nje ya utashi wa rais?
 
Nimesema hili sehemu, bora walivyojitenga na awamu ya 5.
Bora hata awamu hii kuliko hiyo ya 5. Ile ilikuwa ni awamu ya vitisho na isiyofuata utawala wa sheria bali kusaka kiki za kijinga. Na hata hivyo hii ni awamu ya tano wala sio ya sita. Bali hatukuwa tumejipanga na rais kufia madarakani, hivyo kila mtu akaja na tafsiri yake.
 
Kwa katiba hii bado bungee ni kimeo lipo chini ya mwenyekiti wa CCM uchuro na Rais huyohuyo huitisha vikao vya wabunge wa CCM, katiba inaufala mwingi
 
Huyu Rais uwezo binafsi kiakili hana huo ndio ukweli hio nafasi ni kubwa sana kwake anapelekeshwa tu na mahisia mengi tu
 

Tupe source ya habari hii, vinginevyo credibility yake ni questionable.
 
Mkuu hongera na shukrani kwa mchango wako mzuri.

Ni vizuri kwamba Bunge lingetumika kuchuja watendaji wa baadhi ya taasisi, lakini pia ili tuwe na imani na bunge, ni vyema utaratibu wa kuwapata wagombea ubunge pia ubadilike.

Kwa mchakato uliopo wa upatikanaji wa Wabunge, ni sahihi mtu kusema kuwa wananchi tunawapigia kura wawakilishi na chaguo la chama badala ya kupigia kura machaguo au mapendekezo yetu. Haiwezekani mtu wa Mchambawima na Geita wakakae kamati kuu ya chama X waamue ni nani miongoni mwa watia nia ya ubunge anafaa kugombea jimbo la Ngorongoro.

Tuache Wana-Ngorongoro waamue nani awe mgombea wao maana wao ndo wanajua watu wao na si kamati kuu ya chama. Hii itaepusha kupeleka bungeni wabunge ambao si wawakilishi wa wananchi.

Hakika yapo mambo mengi ya kubadilisha nchi hii.
 

Hoja safi sana ya kisomi na kitaalamu.
 
Panga pangua shida ni ccm hata mkifanya je mnapoteza muda, kubomoa uchumi ni rahisi kujenga inachukua miaka,jiandae kuondolewa kwa aibu nyie sio watu wa kuamini tena.
Komboa Taifa tupa nje ccm.

Hao jamaa wote ni wezi hakuna wa kumuonya mwenzake.

Hata wapangue vipi.

Tazama hata wakipangua wanarudi wale wale
 
DpW
 
Kikwete ndo alimwambia afagie wateuzi wa magufuli ,ndo kikwazo chake ,kumbe alimwingiza chaka
 
Bora hii awamu ikaitwa ya sita,ingebaki ya tano ingetia doa Sana.
Asante kwa ufafanuzi safi. Maana hata mimi nilikuwa mjinga nikiamini hii ni awamu ya 5 ya Magu na mama anamalizia awamu ya Magu. Kumbe awamu ya 5 isingewaleta dpw kamwe wala bandari ya Bagamoyo.
 
Vyovyote atakavyofanya, wengi hatuna Imani naye kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…