Mabadiliko ya bei

Mabadiliko ya bei

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
MARKET EQUILIBRIUM

Market ni soko na Equilibrium ni usawa.

SUPPLY PRODUCT = DEMAND PRODUCT

Kwahiyo usawa wa soko unapatikana pale bidhaa zilizozalishwa kwaajli ya mauzo ni sawa na bidhaa zinazohitajika na wanunuaji.

UPANGAJI WA BEI KUTUMIA DEMAND NA SUPPLY

1. Demand isipobadilika, ila supply ikaongezeka basi bei itapungua.

Mfano: Mananasi yakiwa mengi basi bei ya mananasi itashuka.

2.Demand ikipungua ,ila supply isibadilike basi bei itapungua.

Mfano:

Bei ya viatu vya shule mwezi wa 3 inapungua kwasababu watu wengi walishanunua mwezi wa kwanza kwahiyo uhitaji wa viatu umeshuka basi bei inashuka pia.

3. Demand isipobadilika, supply ikapungua basi bei itaongezeka.

Mfano:

Msimu usio wa mahindi basi hufanya bei ya mahindi kupanda bei

4. Demand ikiongezeka, ila supply ikawa ni ile ile basi bei itaongezeka.

Mfano:

Nyama kipindi cha sikukuu au bidhaa za kupikia futari kipindi cha ramadhani.

Karibuni sana kutoa maoni na mifano mengine.

Kumbuka tuna assume vitu vyengine vyote havijabadilika kama kipato, technology, nk

Pia tumetoa bidhaa zile zinazokiuka sheria ya supply na demand.

#equilibrium #pricemaking #demandandsupply #quantity #uchumi #economics
 
Je ni bidhaa zipi 'zile' ambazo 'zinakiuka sheria' ya supply and demand?

CASE AMBAZO ZITAFANYA DEMANDTHEORY ISIFANYE KAZI NI KAMA ZIFUATAZO:

1.Veblen goods

Hizi ni bidhaa ambazo bei inavyokuwa kubwa mtu anaamini ni bora zaidi, kama vipodozi, simu, laptop,magari nk

2.Necessity goods

Kama shule ni kitu muhimu kwahiyo hata ada ikipanda bado wazazi watalipa ili watoto waende shule.

Bei ya dawa za wagonjwa, hata bei ikipanda bado watu watanunua.

3. Giffen goods

Hizi ni bidhaa ambazo zinauzwa bei rahisi

Mfano hata bei ya mchele ikipanda bado watu watanunua mchele, hata bei ya mahindi ikipanda bado watu watanunua maana

unavihitaji kwenye matumizi ya kila siku.

Kuna bidhaa kama chumvi, sukari ni muhimu katika matumizi ya kila siku. Kwahiyo hata bei ikipanda bado watu watanunua.

4.Kubadilika kwa kipato

Ulikua huna kazi ghafla ukapata kazi inayokulipa mshahara mzuri, automatically kama ulikua unashindia ugali dagaa basi utaanza kula pizza na burger kila siku kwasababu una uwezo wa kununua pizza japo ni gharama.

5.Prestige goods

Hizi ni zile bidhaa ambazo humpa mtu thamani katika jamii, mfano kuvaa pete ya Diamond, kuvaa viatu vya leather nk

Kwahiyo bidhaa za ufahari kadri vinavyopanda bei ndio vinavutia watu kuvi demand.

6.Kuamini bei itapanda zaidi

Mtu akiamin bei ya bidhaa flani itazidi kupanda basi anaona anunue mapema atunze. Kama mtu akiamini share za kampuni flani zitapanda basi atanunua hizo share hata kama bei ipo juu.

EXCEPTIONS OF LAW OF SUPPLY

Hizi situation zikitokea basi zitakiuka sheria ya kuwa bei ikipanda lazima na supply itaongezeka au bei ikishuka basi supply itapungua.

1. MFANYABIASHARA AKIWA ANA FUNGA BIASHARA.

Kama mfanya biashara anafunga biashara yake ili aanze biashara nyengine au aachane na biashara kwa ujumla basi atauza bidhaa zake hata kwa bei ndogo ili tu amalize stock aliyo nayo.

"kheri nusu hasara kuliko hasara kamili"

2.AGRICULTURAL PRODUCTS

Kwasababu bidhaa za kilimo zinategemea ardhi na ardhi ina limit kwahiyo supply ya bidhaa za kilimo ina kikomo chake.

Haileti sense kwasababu utasema mbona ardhi bado ipo ya kutosha.

mfano:

Kilimo cha cabbage huwezi kukifanya sehemu zenye joto ni lazima sehemu zenye baridi kwahiyo hii ina limit supply ya cabbage. Kwahiyo hata bei ya cabbage ipande vipi ni ngumu kuongeza supply kubwa kiasi hicho ya cabbage.

3. Muuzaji mmoja

Kama muuzaji wa bidhaa ni mmoja basi mara nyingi yeye ndio anayepanga bei, kwahiyo law of supply haitaweza ku apply kwake.

4. Ushindani

Mfano:

Bei ya vifurushi vya internet imepanda lakini kwasababu ya ushindani basi kampuni moja wapo huamua kushusha bei za vifurushi ili iweze kuongeza wateja. Kwahiyo hiki kitendo kinakiuka sheria ya supply, kwasababu kampuni imeamua kuuza vifurushi vingi kwa bei ya chini.

5. Bidhaa zinazowai kuharibika au zinazokaribia ku expire

Mfano:

Muuza genge akiona nyanya zimeiva sana na akiendelea kubak nazo zitaharibika basi atauza kwa bei rahisi ili asipate hasara kamili.

6. Rare goods

Hizi ni bidhaa hadimu, kwasababu ni hadimu hata bei ipande kiasi gani bado uzalishaji hautobadilika kwasababu ni hadimu.

Mfano:

Mtu atangaze leo anataka kununua kakakuona kwa milllion 500 bado upatikanaji wake ni wa shida.

7. Mnada

Kwenye mnada huwekwa bidhaa chache, tofauti ambazo kila bidhaa itauzwa kwa yule atakayetoa pesa nyingi kununua ili hio pesa itumike katika jambo flani lililokusudiwa na mnada.

Bei huwa haziendani na uhalisia wa bei ya ile bidhaa.

Mfano:

Kwahiyo kwenye mnada mtu akisema atanunua kanga kwa shillingi laki 5 supply haitooongezeka kwasaabu vitu huwa vichache, tofauti na lengo ni kukusanya pesa ili itumike kwaajili ya jambo flani.

8.Wafanyakazi

Kukiwa na uhitaji wa wafanyakazi hata uongeze bei ya mishahara haitofanya wafanya kazi waongezeke kwasababu mwanadamu mpaka azaliwe, afikie umri wa kufanya kazi ni miaka 18 mingine.

Mfano:

Mishahara ya watu wenye degree ya Mechanical engineering imeongezeka haitofanya waliosoma mechanical engineering waongezeke kwa wakati huo, kwasababu itabidi waende wakasome ambayo itachukua miaka 3 - 10 ili wapate ujuzi.

9. Makisio ya bei kupanda zaidi

Mfano:

Bei ya mahindi imependa lakini watu wanahisi inaweza kupanda zaidi basi watu hawatouza kwa wakati huo mahindi yao pamoja na kwamba bei ipo juu.

10.Muuzaji kuwa na shida ya pesa kwa uharaka

Mtu akiwa na shida basi anaweza kujikuta ameuza kitu kwa bei rahisi mno kuzidi thamani yake au bei ambayo ipo sokoni.
 
Back
Top Bottom