SoC01 Mabadiliko ya elimu kwa vijana wa Kitanzania

SoC01 Mabadiliko ya elimu kwa vijana wa Kitanzania

Stories of Change - 2021 Competition

winchester

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
247
Reaction score
250
Navuta picha ya kijana wa kitanzania anayewakilisha vijana wengi wa kiafrika vijana waliokosa mbinu za kujikwamua kiuchumi, kijamii, vijana wasiojua ni nini wafanye kutoka hapo walipo kwenda kwenye hatua nyingine na kupata kile wanachotamani katika ndoto/maisha yao.

Naangali na kutathimini ni nini kimemfikisha hapa alipo leo hii kimemfikisha hapo alipo leo hii kijana huyu na kugundua kuwa serikali yetu, viongozi wetu na jamii ,wazazi , ndugu na jamaa hawakumuandaa katika njia iliyo sahihi , kumpa mwanga /exposure na hali halisi ilivyo , kumnyima nafasi ya kujifunza , kutambua na kuelewa mazingira yaliyomzunguka .

Kijana huyu tangu akiwa mdogo mpaka anamaliza shule/chuo basi amekuwa akibanwa na jambo moja nalo ni kusoma muda mwingi akiwa na matarajio ya kuja kuajiriwa na kupata kazi nzuri hivyo kupelekea kukosa ufahamu wa vitu vingine vingi, Kijana amekuwa akipatiwa elimu ambayo haikidhi mahitaji ya wakati uliopo na pia jamii na wazazi wakishindwa kumpatia elimu mbadala.

SASA NINI KIFANYIKE

Hapa ndipo dhana ya mapinduzi ya kielimu na elimu inapokuja ili kumjenga kijana wa kitanzania , ambayo itamuandaa kijana kukabiliana na mazingira ya aina yoyote, kumpa mwanga na upeo. Elimu hii siyo tu ile atakayoipata shuleni , bali hata nyumbani, na katika jamii.

Elimu ya sasa yapaswa imjenge kijana ambaye atatoka na ujuzi katika ngazi yoyote ya elimu atakayomaliza na sio nadharia pekee elimu itakayompa nafasi ya kujinza mambo mengi nje ya kile ambacho mtaala wa shule unampa kwa sasa. Natamani kuona elimu iwezayo kukuza uelewa wa mtoto katika masomo ya nadharia machache ana huku ikimpa nafasi ya mtoto / kijanaa kuwa na maarifa na ujuzi kama uchoraji , ufumaji, uresemala , usindikaji, kilimo , umeme , kompyuta/tehama, ujenzi na hii iende kwa kila ngazi huku ikua kwa kadiri ya ngazi ya elimu unavyoongezeka huku pia ikimpa nafasi ya kijana kupata maarifa tofauti kupita usomaji wa vitabu tofauti , ili kumpa uwanda mpana wa kupata maarifa (´´ A reader lives a thousand lives before he dies `` a quote by George R.R Martin).

Inapaswa kijana aandaliwe kiasi cha anapohitimu elimu ya sekondari basi awe ana ujuzi mkubwa na kuwa na ufahamu mkubwa wa vitu mbalimbali ili kumsaidia mtoto huyu kuwa tayari kukabili aina yoyote ya mazingira na kujua ni lipi haswa atalifanya katika maisha yake na hata lisipofanikiwa/ timia basi isiwe ndi mwisho/mkwamo katika maisha ya kijana huyu

Natamani kuona akizungukwa na jamii inayomwambia soma upate elimu , lakini pia ikuze kipaji chako badala ya sasa isiyothamini vipaji au soma upate elimu uje kutengeneza ajira badala ya sasa inayomuhusisha kuja kuajiriwa , soma upate elimu na ujuzi mbalimbali badala ya sasa inayosisitiza kwenye nadharia.

Natamani kuona jamii ikimjenga kijana aliyekomaa kiakili na maarifa , uthubutu , shupavu aliyekuzwa ana kuelewa jinsi ya kupambania ndoto zake.

Mzigo huu sio wa kutupiwa serikali peke yake , bali ni kwa kila mmoja katika jamii yetu kuhakikisha kuwa tunakuwa sehemu muhimu na bora kumuandaa kijana tangia akiwa mdogo kwa kumpatia elimu bora itanayoenda na mzingira ya sasa na yajayo.

“Don’t fight in the North or the South. Fight every battle everywhere, always in your mind. Everyone is your enemy, everyone is your friend. Every possible series of events is happening all at once. Live that way and nothing will surprise you. Everything that happens will be something that you’ve seen before”. Quote Game of Thrones Season 7 ep 3
 
Upvote 0
Back
Top Bottom