Mabadiliko ya elimu Tanzania

Mabadiliko ya elimu Tanzania

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Posts
2,180
Reaction score
1,291
Namshika mkono wa heri na shukurani nyingi Rais Samia Hassan kwa mabadiliko mazuri ya elimu anayoyaleta nchini.

Namshukuru sana Rais Samia kwa kutatua kero moja iliyotutesa sana miaka nenda rudi ya Watanzania kuwa wanachama wa jumuia ya madola lakini kiingereza hakizungumzwi na walio wengi.

Mpango wa Rais Samia wa kuhakikisha somo la Kiingereza litafundishwa shuleni ili kuhakikisha mwanafunzi anelewa na kukizungumza ni swala la shukran na kumshika mkono.

Pamoja na kuwa swahili ni lugha yetu ya taifa lakini Watanzania lazima tujue sisi ni wanachama wa jumuia ya madola na lugha yetu ya kimataifa ni kiingereza.

Kwa hiyo kitendo cha kumfunza mwanafunzi lugha ya kiingereza mpaka akizungumze ni ukombozi wa lugha ya kimataifa tuliolilia miaka kadhaa.

Muda si mrefu mabadilko haya tutaona ya kuwa, Tanzania inatoa marefa wa kuchezesha world cup, wasananii kuimba nyimbo za kiingereza na kupanua masoko africa na duniani, makocha wa kitanzania kusambaa kokote uchezwako mpira na kupata ajira na wasomi kutopoteza ajira katika usahili kwa Wakenya na Waganda kwa sababu ya lugha

MAMA SAMIA ASANTE SANA MUNGU AKULIMDE NA KUKUBARIKI. AMINA
 
Ni mabadiliko yapi hayo yanaongelewa? So far momo sijaona mabadiliko yoyote kwenye elimu yetu
 
Mchina,mjapani,mrusi,mkorea etc.

Hawajui hiyo English yako lakini wanakimbiza.

Wanapata tenda za ujenzi wa miundombinu mpaka Uingereza
 
Back
Top Bottom