Mabadiliko ya Kanuni za Mpira wa Miguu kwa Msimu wa 2019/2020

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
26,021
Reaction score
79,710
The International Football Association Board (The IFAB) , imebadilisha baadhi ya kanuni za mchezo wa soka kwenye kikao kilichofanyika wiki iliyopita nchini Scotland . Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:-

1. KUTAKUWA HAKUNA MREJESHO KUTOKANA NA PIGO LA PENATI

Mchezo utasimama kwa kuanzishwa kama penati imeokolewa au imegonga mwamba , hii ina maana hakuna tena nafasi ya kufuata mpira na kufunga ( Rebound ) kwa maana hiyo wachezaji hawatokuwa na uhitaji wa kujipanga nje ya 18.

2.MPIRA KUCHEZWA NA MKONO.

Kuanzia Juni mosi goli litakalofungwa ambalo limegusa mkono wa mchezaji kwa maksudi au bahati mbaya ( Mfungaji ) halitakubaliwa.

3.MABADILIKO YA MCHEZAJI

Mchezaji ambaye atakuwa anafanyiwa mabadiliko ataruhusiwa kutoka kupitia upande wowote ule wa uwanja

4. GOAL KICK

Mchezaji ataruhusiwa kugusa mpira hata ndani ya eneo la 18 kutoka kwa kipa , ambapo sasa hivi ni mpaka mpira utoke kwenye 18 ndio unaruhusiwa kuugusa.

5. KADI KWA MAKOCHA.

Makocha sasa nao watakuwa wanaoneshwa kadi ya njano na nyekundu tofauti na sasa hivi wanaambiwa tu toka kwenye eneo la benchi la ufundi.

6. KWENYE UKUTA WA KUZUIA MIPIRA ILIYOKUFA

Wachezaji wa upande ambao wanapiga mipira iliyokufa ( freekick ) hawatoruhusiwa kwenda kujumuika kwenye ukuta wa timu ambayo inazuia mipira hiyo , tofauti na sasa huwa wanachanganyika kama kuwatoa mchezoni.

7. PENATI .

Magolikipa wataruhusiwa kuweka mguu mmoja tu kwenye mstari na huo mwingine wataamua wao wenyewe waweke wapi , tofauti na sasa kwamba miguu yote lazima iwe kwenye mstari wakati anapigiwa penati.

Kusoma zaidi [emoji116]

Football rules: How will new IFAB laws affect the game?

Update: Sheria ya penalty itabaki kama ilivyokuwa kufuatia clarification kutoka IFAB kuhusu sheria ya rebounds. [emoji116]
 
Attachments

  • Screenshot_20190306-084643.png
    Screenshot_20190306-084643.png
    22.3 KB · Views: 164
Afadhali mpira wa mrejesho/rebound ulikuwa wa kidwanzi....

Sent using Jamii Forums mobile app
Mie hiyo ya penalty imenifurahisha. Sasa wapigaji Watakuwa makini sana.
Halafu hiyo ya ukuta pia nimeipenda.
Zaidi ni kwamba wale wachezaji wanaopenda kupoteza muda wakati wa kutoka sasa watotekea hata kama wapo kwenye line nyingine na sio karibu na fourth official.

Siku ikiwa team yako ndio imekosa pen alafu unaona kabisa rebound ingekuwa inaruhusiwa utatamani hizi sheria zifutwe. Mbaya ukute ndio fainali na labda goli lingefungwa ndio ubingwa ulikua tayari [emoji23]
 
Mie hiyo ya penalty imenifurahisha. Sasa wapigaji Watakuwa makini sana.
Halafu hiyo ya ukuta pia nimeipenda.
Zaidi ni kwamba wale wachezaji wanaopenda kupoteza muda wakati wa kutoka sasa watotekea hata kama wapo kwenye line nyingine na sio karibu na fourth official.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah hata kupoteza muda kutapungua kwa kiasi chake. Huwa inakera mchezaji kujivuta kama kobe alafu unakuta ni dakika za majeruhi.
 
Kwangu naona ni positive changes.
 
The International Football Association Board (The IFAB) , imebadilisha baadhi ya kanuni za mchezo wa soka kwenye kikao kilichofanyika wiki iliyopita nchini Scotland . Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:-

1. KUTAKUWA HAKUNA MREJESHO KUTOKANA NA PIGO LA PENATI

Mchezo utasimama kwa kuanzishwa kama penati imeokolewa au imegonga mwamba , hii ina maana hakuna tena nafasi ya kufuata mpira na kufunga ( Rebound ) kwa maana hiyo wachezaji hawatokuwa na uhitaji wa kujipanga nje ya 18.

2.MPIRA KUCHEZWA NA MKONO.

Kuanzia Juni mosi goli litakalofungwa ambalo limegusa mkono wa mchezaji kwa maksudi au bahati mbaya ( Mfungaji ) halitakubaliwa.

3.MABADILIKO YA MCHEZAJI

Mchezaji ambaye atakuwa anafanyiwa mabadiliko ataruhusiwa kutoka kupitia upande wowote ule wa uwanja

4. GOAL KICK

Mchezaji ataruhusiwa kugusa mpira hata ndani ya eneo la 18 kutoka kwa kipa , ambapo sasa hivi ni mpaka mpira utoke kwenye 18 ndio unaruhusiwa kuugusa.

5. KADI KWA MAKOCHA.

Makocha sasa nao watakuwa wanaoneshwa kadi ya njano na nyekundu tofauti na sasa hivi wanaambiwa tu toka kwenye eneo la benchi la ufundi.

6. KWENYE UKUTA WA KUZUIA MIPIRA ILIYOKUFA

Wachezaji wa upande ambao wanapiga mipira iliyokufa ( freekick ) hawatoruhusiwa kwenda kujumuika kwenye ukuta wa timu ambayo inazuia mipira hiyo , tofauti na sasa huwa wanachanganyika kama kuwatoa mchezoni.

7. PENATI .

Magolikipa wataruhusiwa kuweka mguu mmoja tu kwenye mstari na huo mwingine wataamua wao wenyewe waweke wapi , tofauti na sasa kwamba miguu yote lazima iwe kwenye mstari wakati anapigiwa penati.

Kusoma zaidi [emoji116]

Football rules: How will new IFAB laws affect the game?
Hiyo Sheria no 2 goli kufungwa kwa mkono mbona ilikua haikubaliki tangia huko kitambo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi FIFA na hao IFAB na mkubwa apo?

Yan FiFA scope yao ikoje na IFAB pia..

Sent using Jamii Forums mobile app

Extract ya Wikipedia:-

"It is a separate body from FIFA, though FIFA is represented on the board and holds 50% of the voting power.

Purpose: Guardians of the Laws of the Game..."

Kina member 8, wa 4 ni kutoka FIFA. Ili jambo lipite kura 6 au zaidi ni lazima zipatikane.
 
Hiyo Sheria no 2 goli kufungwa kwa mkono mbona ilikua haikubaliki tangia huko kitambo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna magoli ya mikono ambayo yameruhusiwa ku stand either kwa refa kutokuona au sababu nyingine. Hii sheria inasaidiana na VAR kwamba ikitokea utata inabidi VAR itumike na ikionekana mpira umegusa mkono kwa bahati mbaya au makusudi basi goli linakuwa cancelled.

Kabla ilikua ni discrition ya refa tu ndio ina stand akiamua kukataa au kuamua kutokana na mazingira hakuna alieweza kupinga.

Kwa mantiki hiyo hakutakaa kuwe na goli la Nape tena kwenye football.
 
Extract ya Wikipedia:-

"It is a separate body from FIFA, though FIFA is represented on the board and holds 50% of the voting power.

Purpose: Guardians of the Laws of the Game..."

Kina member 8, wa 4 ni kutoka FIFA. Ili jambo lipite kura 6 au zaidi ni lazima zipatikane.
Thanks Kop kwa clarification [emoji109]
 
Kuna magoli ya mikono ambayo yameruhusiwa ku stand either kwa refa kutokuona au sababu nyingine. Hii sheria inasaidiana na VAR kwamba ikitokea utata inabidi VAR itumike na ikionekana mpira umegusa mkono kwa bahati mbaya au makusudi basi goli linakuwa cancelled.

Kabla ilikua ni discrition ya refa tu ndio ina stand akiamua kukataa au kuamua kutokana na mazingira hakuna alieweza kupinga.

Kwa mantiki hiyo hakutakaa kuwe na goli la Nape tena kwenye football.
Sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom