Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huu ni mwanzo wa kutoa ball to hand,kwangu Mimi kushika ni kushika tu iwe mpira umeufuata mkono au mkono umeufuata mpiraHiyo Sheria no 2 goli kufungwa kwa mkono mbona ilikua haikubaliki tangia huko kitambo?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ningekuwapo ktk hiko kikao ningependekeza No Substitution During injury time...hakuna kubadilisha mchezaji wakati ule wa muda wa nyongeza wa majeruhi.The International Football Association Board (The IFAB) , imebadilisha baadhi ya kanuni za mchezo wa soka kwenye kikao kilichofanyika wiki iliyopita nchini Scotland . Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:-
1. KUTAKUWA HAKUNA MREJESHO KUTOKANA NA PIGO LA PENATI
Mchezo utasimama kwa kuanzishwa kama penati imeokolewa au imegonga mwamba , hii ina maana hakuna tena nafasi ya kufuata mpira na kufunga ( Rebound ) kwa maana hiyo wachezaji hawatokuwa na uhitaji wa kujipanga nje ya 18.
2.MPIRA KUCHEZWA NA MKONO.
Kuanzia Juni mosi goli litakalofungwa ambalo limegusa mkono wa mchezaji kwa maksudi au bahati mbaya ( Mfungaji ) halitakubaliwa.
3.MABADILIKO YA MCHEZAJI
Mchezaji ambaye atakuwa anafanyiwa mabadiliko ataruhusiwa kutoka kupitia upande wowote ule wa uwanja
4. GOAL KICK
Mchezaji ataruhusiwa kugusa mpira hata ndani ya eneo la 18 kutoka kwa kipa , ambapo sasa hivi ni mpaka mpira utoke kwenye 18 ndio unaruhusiwa kuugusa.
5. KADI KWA MAKOCHA.
Makocha sasa nao watakuwa wanaoneshwa kadi ya njano na nyekundu tofauti na sasa hivi wanaambiwa tu toka kwenye eneo la benchi la ufundi.
6. KWENYE UKUTA WA KUZUIA MIPIRA ILIYOKUFA
Wachezaji wa upande ambao wanapiga mipira iliyokufa ( freekick ) hawatoruhusiwa kwenda kujumuika kwenye ukuta wa timu ambayo inazuia mipira hiyo , tofauti na sasa huwa wanachanganyika kama kuwatoa mchezoni.
7. PENATI .
Magolikipa wataruhusiwa kuweka mguu mmoja tu kwenye mstari na huo mwingine wataamua wao wenyewe waweke wapi , tofauti na sasa kwamba miguu yote lazima iwe kwenye mstari wakati anapigiwa penati.
Kusoma zaidi [emoji116]
Football rules: How will new IFAB laws affect the game?
Yeah ManHuu ni mwanzo wa kutoa ball to hand,kwangu Mimi kushika ni kushika tu iwe mpira umeufuata mkono au mkono umeufuata mpira
Sent using Jamii Forums mobile app
Itabidi takers wawe tu clinical otherwise robounds itakua sawa na aliepaisha tuPamoja Kop.
Hapo kwenye penati siyo favorable.
Mo? [emoji23][emoji23][emoji23]Kwenye kudive vp? Maana kina Neymer, na Mo wamezidi kwenye hii area
Sent using Jamii Forums mobile app
Aha..umetisha mze babaExtract ya Wikipedia:-
"It is a separate body from FIFA, though FIFA is represented on the board and holds 50% of the voting power.
Purpose: Guardians of the Laws of the Game..."
Kina member 8, wa 4 ni kutoka FIFA. Ili jambo lipite kura 6 au zaidi ni lazima zipatikane.
Naona unawatafuta ubaya MikiaNingekuwapo ktk hiko kikao ningependekeza No Substitution During injury time...hakuna kubadilisha mchezaji wakati ule wa muda wa nyongeza wa majeruhi.
Pia ningependekeza football iwe na knock out...ukipigwa goli 5 au goal difference ya goal 5 mpira unaisha hapohapo,ushindi wa hivyo uitwe super win na unapata point 5
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23]
Hamna jinsi mkuu,si umeona soka litakavyokuwa la ushindani??itakuwa hakuna kupaki basi,ukipigwa 3 unakaza msuli ukafunge upunguze goli difference usipigwe KO
True football inapotea taratibu Hawa viongoz WA Sasa wanachojua n kurekebisha kanuni na kuongeza kanuni na kuongeza technology yao nying kwenye Mpira Sasa Kulikuwa kuna haja gan Ya kubadilika Mbona wanapoteza ladha ya Mpira wa Miguu
Walisema mpigaji haruhusiwi kucheza rebound kwa vile ana faida ya ukaribu na kipa ila badae wakaruhusu kwa maana mchezo unakuwa bado unaendelea kwanini umnyime haki ya kucheza mchezaji ambae yuko ndani ya uwanja wakaruhusu mpigaji kuweza kucheza rebound na kufungahio sheria ya penalty mbn waliitoa wakaacha rebounds ziwe halali kama kawaida kwa ufahamu wangu?
Dah ndio hivyo yaniUko tunakoenda ndo ladha ya mpira wa miguu inaenda kupotea.Kuna watu wamekaa kwa interest zao kazi yao sio kuboresha bali kuharibu kwa mgongo wa maboresho.