Mabadiliko ya Kanuni za Mpira wa Miguu kwa Msimu wa 2019/2020

Mabadiliko ya Kanuni za Mpira wa Miguu kwa Msimu wa 2019/2020

True football inapotea taratibu Hawa viongoz WA Sasa wanachojua n kurekebisha kanuni na kuongeza kanuni na kuongeza technology yao nying kwenye Mpira Sasa Kulikuwa kuna haja gan Ya kubadilika Mbona wanapoteza ladha ya Mpira wa Miguu
 
The International Football Association Board (The IFAB) , imebadilisha baadhi ya kanuni za mchezo wa soka kwenye kikao kilichofanyika wiki iliyopita nchini Scotland . Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:-

1. KUTAKUWA HAKUNA MREJESHO KUTOKANA NA PIGO LA PENATI

Mchezo utasimama kwa kuanzishwa kama penati imeokolewa au imegonga mwamba , hii ina maana hakuna tena nafasi ya kufuata mpira na kufunga ( Rebound ) kwa maana hiyo wachezaji hawatokuwa na uhitaji wa kujipanga nje ya 18.

2.MPIRA KUCHEZWA NA MKONO.

Kuanzia Juni mosi goli litakalofungwa ambalo limegusa mkono wa mchezaji kwa maksudi au bahati mbaya ( Mfungaji ) halitakubaliwa.

3.MABADILIKO YA MCHEZAJI

Mchezaji ambaye atakuwa anafanyiwa mabadiliko ataruhusiwa kutoka kupitia upande wowote ule wa uwanja

4. GOAL KICK

Mchezaji ataruhusiwa kugusa mpira hata ndani ya eneo la 18 kutoka kwa kipa , ambapo sasa hivi ni mpaka mpira utoke kwenye 18 ndio unaruhusiwa kuugusa.

5. KADI KWA MAKOCHA.

Makocha sasa nao watakuwa wanaoneshwa kadi ya njano na nyekundu tofauti na sasa hivi wanaambiwa tu toka kwenye eneo la benchi la ufundi.

6. KWENYE UKUTA WA KUZUIA MIPIRA ILIYOKUFA

Wachezaji wa upande ambao wanapiga mipira iliyokufa ( freekick ) hawatoruhusiwa kwenda kujumuika kwenye ukuta wa timu ambayo inazuia mipira hiyo , tofauti na sasa huwa wanachanganyika kama kuwatoa mchezoni.

7. PENATI .

Magolikipa wataruhusiwa kuweka mguu mmoja tu kwenye mstari na huo mwingine wataamua wao wenyewe waweke wapi , tofauti na sasa kwamba miguu yote lazima iwe kwenye mstari wakati anapigiwa penati.

Kusoma zaidi [emoji116]

Football rules: How will new IFAB laws affect the game?
Ningekuwapo ktk hiko kikao ningependekeza No Substitution During injury time...hakuna kubadilisha mchezaji wakati ule wa muda wa nyongeza wa majeruhi.

Pia ningependekeza football iwe na knock out...ukipigwa goli 5 au goal difference ya goal 5 mpira unaisha hapohapo,ushindi wa hivyo uitwe super win na unapata point 5

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona unawatafuta ubaya Mikia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi naona kama watakuwa wameondoa utamu hapo kwenye Penalt,...
 
True football inapotea taratibu Hawa viongoz WA Sasa wanachojua n kurekebisha kanuni na kuongeza kanuni na kuongeza technology yao nying kwenye Mpira Sasa Kulikuwa kuna haja gan Ya kubadilika Mbona wanapoteza ladha ya Mpira wa Miguu

Unajua sasa hivi makampuni ya betting yanachangia kipato kikubwa sana kwenye mpira, in terms ya matangazo, subscriptions na sponsorships.

Kwa hiyo basi, ili kuzuia/kupunguza iwezekano wa makampuni hayo ku-influence matokeo, inabidi power ya referees ipunguzwe na maamuzi yawe ya wengi.

Pia zile incidences zinazoweza kuleta utata pia zinatengenezewa sheria ili kuondoa mikanganyo.

Tafuta makala kuhusu sports betting zinavyoathiri michezo utanielewa.
 
hio sheria ya penalty mbn waliitoa wakaacha rebounds ziwe halali kama kawaida kwa ufahamu wangu?
Walisema mpigaji haruhusiwi kucheza rebound kwa vile ana faida ya ukaribu na kipa ila badae wakaruhusu kwa maana mchezo unakuwa bado unaendelea kwanini umnyime haki ya kucheza mchezaji ambae yuko ndani ya uwanja wakaruhusu mpigaji kuweza kucheza rebound na kufunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom