Mabadiliko ya Katiba ya Kenya, wanaodai Katiba Mpya Tanzania mnalo la kujifunza

Hana analoweza kuamua kwa Zanzibar, tunahitaji katiba mpya Tanzania
 
Sio mbaya mbaya ni kufikia kuwa katiba itazuia kila kitu

USSR

Kwa taarifa yako katiba mpya sio ya kumaliza kila kitu, maana hata agano jipya kwa wakristo inasemekana limeboreshwa kuliko agano la kale, lakini bado wakristo wana matatizo yao. Hao Wakenya kupitia katiba mpya wana ubora mkubwa kuliko sisi, hata kama wana matatizo kadhaa. Huwezi fananisha na huu upuuzi unaoendelea hapa kwetu.
 
Suala la tume kuamua nani awe rais Ni upuuzi mtupu hakuna haja ya kupiga kura kwa katiba ya sasa
 
Rais wa muungano anatakiwa azungumzie mambo yanagusa pande zote mbili sio Tanganyika tu
Na ikija Ile tunayoitamni zaidi ya Mzee warioba ambayo ni ya maoni yetu sisi Rasmi huyu wa Muungano hatogusa mambo yanayohusu Tanganyika mambo ya madini maliasili havita muhusu yeye atakua wa UN na masafari yake kama ya hangaya
 
Katiba ya Kenya imetufunza mengi mno, ilichofanikiwa zaidi ni kubadilisha tawala za vyama, lakini haikuwahi kubadilisha hali za maisha za wakenya au kuzuia ufisadi au ufujaji wa fedha kwa namna yoyote ile, tuwe makini aidha tungoje kwanza, tusiwe na papara,tuachane na njaa za upinzani juu ya takwa lao la madaraka.
 
Bunge la Kenya lipo kwenye mjadala wa kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba yake kwa kinatajwa na muungano wa Kenya Kwanza ya Rais Ruto kuunganisha taifa, hii ni baada ya mpango wa Rais Kenyatta wa BBI kukataliwa na Majaji huku pande mbili za kieleweke na tangatanga zikiumana kipindi hicho.

Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 iliyotangazwa na marehemu Mzee Kibaki na mshindani wake Raila wakiwaambia wakenya kuwa italiweka pamoja taifa kitu kilichoshindika ,italeta maendeleo kitu kilichoshindika hali ya maisha ya wakenya ni ngumu licha ya Serikali kuzidiwa madeni ya ndani na nje.

Hapa Tanzania kuna kundi tangu mwanzo linadai eti katiba mpya italeta usawa na kuwa jawabu la mambo yote ya kiuchumi na kijamii kitu ambacho si kweli, usalama wa Kenya uko hoi mauaji, utekaji, na wanasiasa sasa wanaopinga Ruto wanatamani kukimbia nchi licha ya katiba mpya huku wapinzani wakiandamana kupinga matokeo na kutotambua matokeo kuwa kuwa tume ya uchaguzi ilimpendelea rais Ruto kama hapa Tanzania wapinzani wakigomea matokeo ya 2020

My take: Baada ya Tanzania kupata Katiba tutajikuta matatizo yetu yapo palepale maana watu ni walewale tu

USSR
Kwa hiyo kwa mawazo yako tusibadili katiba ,ili iweje kwa hakili yako hii iliyopo inafaa

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Hivi makubaliano ya 1964 yanaweza kuwa applied leo?. Muungano usioeleweka. Mzanzibar anasimamia na kucontrol mambo ya Tanganyika lakini mtanganyika hawezi kucontrol mambo ya Zanzibar.
 
Katiba ya Kenya imetufunza mengi mno, ilichofanikiwa zaidi ni kubadilisha tawala za vyama, lakini haikuwahi kubadilisha hali za maisha za wakenya au kuzuia ufisadi au ufujaji wa fedha kwa namna yoyote ile, tuwe makini aidha tungoje kwanza, tusiwe na papara,tuachane na njaa za upinzani juu ya takwa lao la madaraka.

Tatizo lako unashindwa kutofautisha katiba mpya na ujinga wa viongozi. Umesahau Kenya Wana magavana na senator na mabunge ya kaunti. Wana Tume huru, Wana weza kupinga matokeo ya urais mahakamani, mahakama yaweza kutengua uchaguzi , majaji wanaomba kazi ya ujaji na kufanyiwa interview hadharani.

Tatizo lako unaona katiba mpya Kama hitaji la wapinzani na sio nchi. Wapinzani watapigia kelele Yale yanao wahusu.
 
Katiba ya Kenya imetufunza mengi mno, ilichofanikiwa zaidi ni kubadilisha tawala za vyama, lakini haikuwahi kubadilisha hali za maisha za wakenya au kuzuia ufisadi au ufujaji wa fedha kwa namna yoyote ile, tuwe makini aidha tungoje kwanza, tusiwe na papara,tuachane na njaa za upinzani juu ya takwa lao la madaraka.
🤣🤣🤣 Wewe utakuwa ni wale wa kupita bila kupingwa na ndio maana huoni umuhimu wa katiba mpya.

Sasahivi Jiandae kutumia kiinua mgongo chako kwenye kampeni. PUMBAFU
 
Tunachoka sisi ni Katiba Mpya.. iwe na mabadiliko au hisiwe nayo lakin UKAWA ni lazima...
 
Bunge la Kenya lipo kwenye mjadala wa kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba yake kwa kinatajwa na muungano wa Kenya Kwanza ya Rais Ruto kuunganisha taifa, hii ni baada ya mpango wa Rais Kenyatta wa BBI kukataliwa na Majaji huku pande mbili za kieleweke na tangatanga zikiumana kipindi hicho.

Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 iliyotangazwa na marehemu Mzee Kibaki na mshindani wake Raila wakiwaambia wakenya kuwa italiweka pamoja taifa kitu kilichoshindika ,italeta maendeleo kitu kilichoshindika hali ya maisha ya wakenya ni ngumu licha ya Serikali kuzidiwa madeni ya ndani na nje.

Hapa Tanzania kuna kundi tangu mwanzo linadai eti katiba mpya italeta usawa na kuwa jawabu la mambo yote ya kiuchumi na kijamii kitu ambacho si kweli, usalama wa Kenya uko hoi mauaji, utekaji, na wanasiasa sasa wanaopinga Ruto wanatamani kukimbia nchi licha ya katiba mpya huku wapinzani wakiandamana kupinga matokeo na kutotambua matokeo kuwa kuwa tume ya uchaguzi ilimpendelea rais Ruto kama hapa Tanzania wapinzani wakigomea matokeo ya 2020

My take: Baada ya Tanzania kupata Katiba tutajikuta matatizo yetu yapo palepale maana watu ni walewale tu

USSR
Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania maeneo machache yanahitajika. Hakuna haja ya Katiba Mpya, bali mabadiliko kwenye maeneo machache kama vile kuruhusu wagombea huru. Hakuna sababu yoyote ya kusema ili mtu agombee nafasi ya kuchaguliwa (uenyekiti wa mtaa/kijiji, udiwani, ubunge na uraisi) ni lazima adhaminiwe na chama cha siasa.

Ila suala la katiba likishughulikiwa kiholela na kuwa na mtazamo wa "Katiba Mpya!" "Katiba Mpya!" inaweza kuwa hivi:

332353206_535298785371577_553345934153692923_n.jpg
 
Katiba mpya ni muhimu sana ,hii ya sasa imewapa madaraka makubwa viongozi,ndio nchi imekuwa shamba la bibi
 
Back
Top Bottom