Mabadiliko ya Katiba ya Kenya, wanaodai Katiba Mpya Tanzania mnalo la kujifunza

Mabadiliko ya Katiba ya Kenya, wanaodai Katiba Mpya Tanzania mnalo la kujifunza

Msingi mkubwa wa katiba ni kuleta haki na uwajibikaji sio kuondoa shida za mtu binafsi
 
Bunge la Kenya lipo kwenye mjadala wa kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba yake kwa kinatajwa na muungano wa Kenya Kwanza ya Rais Ruto kuunganisha taifa, hii ni baada ya mpango wa Rais Kenyatta wa BBI kukataliwa na Majaji huku pande mbili za kieleweke na tangatanga zikiumana kipindi hicho.

Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 iliyotangazwa na marehemu Mzee Kibaki na mshindani wake Raila wakiwaambia wakenya kuwa italiweka pamoja taifa kitu kilichoshindika ,italeta maendeleo kitu kilichoshindika hali ya maisha ya wakenya ni ngumu licha ya Serikali kuzidiwa madeni ya ndani na nje.

Hapa Tanzania kuna kundi tangu mwanzo linadai eti katiba mpya italeta usawa na kuwa jawabu la mambo yote ya kiuchumi na kijamii kitu ambacho si kweli, usalama wa Kenya uko hoi mauaji, utekaji, na wanasiasa sasa wanaopinga Ruto wanatamani kukimbia nchi licha ya katiba mpya huku wapinzani wakiandamana kupinga matokeo na kutotambua matokeo kuwa kuwa tume ya uchaguzi ilimpendelea rais Ruto kama hapa Tanzania wapinzani wakigomea matokeo ya 2020

My take: Baada ya Tanzania kupata Katiba tutajikuta matatizo yetu yapo palepale maana watu ni walewale tu


USSR
Hilo hatukatai lakini,acha katiba ibadilishwe pia inaonekana imezeeka,pengine Kuna Mambo mapya yatawekwa mlo na mengine yatapunguzwa,na huwezi ukajua yatakayoongezwa mle kwenye katiba mpya yatazaidiaje,ama yatakayopunguzwa yataleta faida gani
 
Back
Top Bottom