SoC03 Mabadiliko ya mfumo wa elimu

SoC03 Mabadiliko ya mfumo wa elimu

Stories of Change - 2023 Competition

Chalala04

New Member
Joined
Jun 24, 2023
Posts
4
Reaction score
4
Elimu ni ujuzi anaopokea mtu kutoka Kwa we ye uekewa zaidi juu ya jambo fulani
Kuna aina tatu za elimu

1. Elimu rasmi
hii ni ule ujuzi tunaoupata kutoka a mfumo maalumu wa serikali mfano shule na vyuo

2. Elimu ya jadi
hii ule ujuzi unaopatikana kutoka na mafunzo ya makabila na jamii zetu mfano jando na unyago

3. Elimu ya utambuzi

Hii ni ule ujuzi tunaoupata kwa lengo la kutuongoza maisha ya Kila siku iwe bila kufundishwa na mtu yoyote aidha kwa kuona, kugundua au kubuni au kufundishwa mfano kutamka maneno kufanya kazi kama kufua, kupika, nk
Elimu hii lizima uwe nayo hata uusipoenda shule, jando /unyago lazima utaipata maana ndiyo maisha yetu lazima ujifunze lugha mama kupitia elimu hii, ujifunze kutembea na nk

CHANGAMOTO YA ELIMU YA TANZANIA

1. Imejikita zaidi kwenye nadharia

Elimu yetu sio komavu haipo kwenye matendo bali kwenye maongezi na maandiko, mfano asilimia kubwa ya shule zetu haina maabara za kufanya majaribio ya kibaologia na kemia asilimia zaidi ya 60, shule zenye vitendo japo kwa asilimia 70% basi ni za mjini.

2. Elimu inakosa uhalisia
Elimu yetu haina uhalisia hata kidogo, mitaala ya elimu haina misimamo, mfano historia na biologia zinapishana juu ya chazo cha binadamu ila zote zinakubalika ilitakiwa wataalamu wa elimu yetu waje na mfumo ambao hauna mkizano ili kutengeneza elimu yenye uhalisia, kuna vitu vingi tunajifunza ambavyo havipo makazini wala kwenye maisha ya kawaida

3. Mpangilio mbaya wa mitaala

Hii changamoto innasikitisha sana mfano elimu ya shule ya msinngi na sekondari kwa kiasi kikubwa utofauti wake ni lugha ila vitu vinafanana sasa hatuoni kuna haja ya kupanga kitu kimoja kanachoeleweka, mimi nafikiri tuchague kuwa tuanze na kufundishana kingereza alafu ndiyo tukasome hiyo mitaala kwa kingereza tu sio unasoma miaka saba kwa kiswahili alafu unaenda kurudia kwa kingereza miaka minne haileti maana
Pia, elimu yetu haina mtiririko sahihi mfano, unakuwa mwanafunzi amemaliza kidato cha nne anaenda ngazi ya diploma alafu akimaliiza anaenda kurudia vilevile ngazi ya degree hatuoni kuna haja ya kubadili

MAONI NA USHAURI

1. Tuachane na elimu isiyo na tija kwetu na kuja a mambo mengi yasiyo na faida kwenye taifa na maisha yetu ya kawaida nadomo kama stadi za kazi na haiba na michezo iwe msingi wa elimu yetu

2. Tupunguze mlolongo wa elimu yetu mfano, elimu ya msingi ni miaka saba tuweke mitano, tujikite zaidi kwenye lugha ili anayetoka elimu ya msingi kwa kua amesoma sana lugha itamlaisishia lugha kwenye elimu ya msingi, pia haiba na michezo na stadi za kazi itamfanya awe mbunifu toka chini.
Diploma na degree kwasababu wanasoma vitu vinavyofanana kwa asilimia kubwa tutafute kitu cha tofauti iadha kwa diploma au degree au, tuondoe kidato cha tano

3. Elimu ijikite zaidi kwenye vitendo sio maneno ili itujengee taifa tendaji toka chini mpaka juu

4. Kuongeza ufuatilia kwenye ufundishaji sio mwalimu akiajiliwa ndiyo imeisha tuongee ufuatiliaji zaidi
 
Upvote 1
Back
Top Bottom