SoC01 Mabadiliko ya Mfumo wa Rufaa ya Matibabu (Medical Referral System)

SoC01 Mabadiliko ya Mfumo wa Rufaa ya Matibabu (Medical Referral System)

Stories of Change - 2021 Competition

MulegiJr

Senior Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
125
Reaction score
88
MFUMO WA RUFAA YA MATIBABU ni mfumo ambao unamwezesha mgonjwa kutoka kituo kimoja kwenda kigine kwaajili ya kujipatia Matibabu, kulingana na ukubwa wa tatizo, au uhaba wa wataalum , au kulingana na kutokuwepo kwa vifaa vya kutosha katika kituo husika.

Rufaa ya Matibabu hutolewa kulingana na ngazi ya kituo husika, kwa Mfano kutoka zahanati hadi kituo cha Afya, kutoka kituo cha Afya kwenda hospitali ya wilaya, kutoka Hospitali ya wilaya kwenda mkoa, kutoka mkoa kwenda Hospitali ya kanda na kutoka kanda kwenda Hospitali ya Taifa na kutoka Taifa kwenda nje ya nchi au Msaada kutoka hospitali private kulingana na ushauri wa wataalum husika.

Tokea tupate Uhuru nchi yetu ina Mfumo mmoja tu wa RUFAA YA MATIBABU(PHYSICAL LETTER), mtu anakuwa pewa barua hiyo toka mwanza hadi Dar es Salaam, anatoka Katavi hadi Muhimbili, anatoka mwananyamala hadi Muhimbili.

Rufaa ya matibabu inaandikwa na Jopo la madaktari kuja kwenďa kwa mganga mkuu wa Level husika.

CHANGAMOTO YA MFUMO HUU.
1. Kwa mujibu wa Shirika la Ifakara Health Institute, mfumo huu wa kizamani unaotumika nyakàti hizi za Sayansi unaendelea kugharimu maisha ya watanzania kwa mamia, na unasababisha vifo kwa Mamia, kwa maana siyo rahisi utokea Mbinga ifike muhimbili na kesho yake upate mtibabu, maana yake, itakuchukua wiki au mwezi kufanyiwa checkup upya.

2. Mfumo huu unasababisha mrudikano wa wagonjwa pia kwa madaktari maana ni rahisi kwa hospitali kama muhimbili kwa siku kuwa na Rufaa zaidi ya 200+ kulingana na uhaba wa matabibu bingwa ùko kwenye hospitali zetu za wilaya au mikoa.

3. UPOTEVU WA MUDA NA GHARAMA, mfumo huu siyo rafiki kwa sababu unasababisha mtu kutoka sehemu moja kwenda ingine na kwa maana hiyo ni rahisi mtu kutumia wiki mbili kutoka ukerewe hadi BUGANDO MEDICAL HOSPITAL akisubiri kufanyiwa checkup ya jino , kwa wiki hizo akitumia fedha, bila kuzalisha na bado gharama ya matibabu.

NINI KIFANYIKE(SOLUTION).
1. Tubadilike kutoka kwenye Physical letter, twende na kasi ya mabadiliko ya Dunia lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa Rufaa, kuwapunguzia Madaktari Rufaa nyingi, kusaidia kupunguza gharama kwa Watanzania ambao wanatumia gharama kubwa kufikia matibabu yao.

2. INTEGRATED AND AUTOMATIVE DIGITAZED MEDICAL REFERRAL system ambayo itafungwa katika level ya wilaya, mkoa, kanda na Taifa , mfumo huu utakuwa na taarifa zote za mgonjwa na taarifa za Hospitali husika, mfano, unamrufaa Mgonjwa kwenda Bugando kumbe Tarehe uliompeleka bugando Daktari husika hatokuwepo kwa muda wa wiki nzima lakini wakati huo Hospitali ya kanda ya Mara inadaktari hisika na hana mzigo wa wagonjwa wengi, unakuta ni rahisi kutoa huduma kuliko kwenda kurundika watu sehemu moja na kwa mrefu.

3. Mfumo huu utapunguza gharama kwa mgonjwa lakini pia utampa muda wa yeye kujipanga kwa ajili ya kusubiri tarehe, muda na gharama za matibabu halisi akiwa nyumbani.

4. Mfumo huu utatambua pia uharaka wa matibabu kwa Mgonjwa kwa maana hiyo mfumo utaruhusu Madaktari kushauriana, na kutoa taarifa ambazo ni sahihi na kufanya maamuzi kwa haraka zaidi.

Kuna mifumo ambayo imefaulu na inafanya kazi kwa uhakika, Mfumo wa maabara za LANCET LABORATORIES na Hospitali nyingi za Private kama Agakhan wana mfumo wa referral kutoka hospitali zao. Kwa nchi yetu ni rahisi kama taifa likashirikiana na Wadau.

Mwisho japo siyo kwa ùmuhimu kubadili mfumo wa Rufaa ya Matibabu, tutapunguza Vifo vya mama na mtoto, tutapunguza vifo wa wakati wa kujifungua, tutapunguza vifo vya wazee, lakini tutapunguza Mzigo mkubwa kwa madaktari Bingwa ambao ni wachache kulingana na mahitaji.

Ni Jozi yangu kuona napata Msaada wa Kifedha au kimfumo ambao unaweza Rahisisha unafuu wa Huduma wa Rufaa,ukizingatia saivi tuna Comolex mpya za kufikisha taarifa za Miundo mbinu za Upatikanaji na kuokoa Muda.

Naomba kuwasilisha.
View attachment 1856906 #wizarayaafya.
 
Upvote 53
Uwekezaji katika sekta ya afya uko chini. Kama sekta hii ingekuwa na uwekazaji nusu ya unaostahili kwanza ingetoa ajira kwa vijana wengi sana.

Uwajibikaji ni tatizo sugu katika nchi za kisoshalist. Kwasababu ya collectivity of resources, hakuna mwenye uchungu na mali ya umma. Viongozi wanawaza kupiga na hata wizi ukijulikana kuna kulindana.
 
Sometimes, Mifumo ìnakuwa na ugumu kwa serikali kuhandle, unakuta wanataka, lakini mazingira ya wananchi na capital inakuwa ni shida, policy ya afya ya 2017 inaonyesha utayari wa serikali juu ya kufanya integration na wadau mbali mbalikuboresha mfumo wa utoaji huduma za afya.
 
Nimeongeza Picha ya operation ya Designed referral system, unaweza pia kuipitia.
2-Figure1-1.jpg

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Hasara ya kutumia Physical (hard copy, Nakala ngumu) Rufaa ya Matibabu ni kwamba lazima ifike na ni lazima uchukue mhusika, kitu ambacho kinapoteza Maisha ya Watanzania wengi na pia kinapoteza muda na kitendo iki kinatia Uvivu wa kwenda kufatilia matibabu zaidi. Serikali inapswa kuwekeza kwenye Technologia.

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Afya ni Njia moja wapo ya kukuza Maendleo ya nchi yoyote hapa Duniani, Taifa lenye Watu wasio na Afya, maendeleo yake pia hayana Afya.@Wizara ya Afya Tanzania

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Uwekezaji katika Technologia ya Mfumo wa Rufaa ya Matibabu ni Jambo la Msingi sana kwa kuzingatia kuwa wataalum wa wabobezi wa Afya ni wachache na vifaa pia ni vichache.
 
Wakati Dunia, inapita kwenye Janga la corona, ulimwengu unapita kwenye online consultations, online medicine delivery, Appoitment with physicians for check up, but still our country is applying the same Method, where check up is done to the centre, medicine a priscribed physically and consultations are only found at the centre.. should we shift or remain with this kind of services?
 
Asante sana Mkuu kwa kuleta mada hii.

Kwa kweli tunahitaji mabadiliko Kwenye mfumo wetu wa kutoa rufaa kwa wagonjwa. Kwa mfano, unaweza kuta mgonjwa fulani ametakiwa kwenda Hospitali Ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokea Hospitali ya Mkoa ambako kimsingi ameshakutana na Daktari pengine mwenye kiwango cha Ubingwa fulani Ila kulingana wengi wa wagonjwa MNH na administrative bureaucracy, huyu mgonjwa anaweza kuanza kuonwa kwanza na Daktari ambaye yupo mafunzoni(Intern Doctor). Huku ni kumpotezea huyu mgonjwa muda na rasilimali fedha.

Changamoto nyingine kubwa ni kutokuwepo kwa Feedback ya maandishi kwenda kwa Hospitali za level ya chini. Mahali ambapo huyu mgonjwa anaishi. Kama Daktari kutoka Hosp ya mkoa ameandika barua kumtuma mgonjwa hospital ya kanda au taifa, nadhani ni busara kwa Daktari wa Hospitali ya Kanda/Taifa na yeye pia kumuandikia barua yenye maelezo ya kina hatua mbali mbali za matibabu ya mgonjwa husika. Ili shida ya mgonjwa ikijirudia iwe rahisi kwa madaktari wake wa karibu kujua wanaanzia wapi.
 
Tatizo ni Kubwa, Idea yangu, sijaifunua yote kwa kutunza baadhi ya features, lakini ni Moja ya Msukumo mkubwa wa Idea hii. MUNGU anijalie nipate support ya kuonana na Wakubwa na wategeneza Policy ya Afya. Nitafarijika sna.
 
Back
Top Bottom