SoC03 Mabadiliko ya tabia nchi: Tufanye nini kuirudisha Eden katika miji na majiji?

Stories of Change - 2023 Competition

Jerry Farms

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
202
Reaction score
167
Ni dhahili hali sasa inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyoenda. Mwanadamu amekua akifurahia na kuvumbua dhana mbalimbali za kumsaidia kazi! Maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia yamepamba moto katika nyanja mbalimbali....kilimo, usafirishaji, mawasiliano, viwanda, afya nakadhalika. Yote haya kwa namna moja yamechangia katika kuathiri mazingira asili ya toka kuumbwa kwa ulimwengu.

Kulingana na ripoti ya UNEP ya 2022 inakadiliwa kuwa ifikapo mwaka 2030 mataifa yatalazimika kutumia taklibani dola bilion 340 kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nnchi!!!! Hapa tunamnukuu mkurungenzi wa UNEP, "Mabadiliko ya tabia nnchi yana athari sawa kwa wanadamu...jitihada za lazima zinapaswa kuwepo kukabiliana na athari hizi.." Inger Andersen, mkurungenzi mtendaji UNEP 2022, Mkutano wa UNEP Nairobi Kenya.

Hapa swali ni je...niisubiri serikali yangu kukabiliana na athari hizi? Nini nifanye kukabiliana na mabadiliko ya tabia nnchi? Maswali ni mengi, hemu natutazame athari za mabadiliko ya tabia nnchi kwa uchache hapa Tanzania.

KUSUASUA KWA SHUGHULI ZA KILIMO NA KUPUNGUA KWA MAVUNO MWAKA 2022/2023
Hili linaonekana katika kila kona huko majumbani mwetu. Mikoa iliyokua ikisifika kwa uzalishaji wa chakula imeshuka kwa kasi ya 5G! Katika uzalishaji wa chakula, hali hii imepelekea kupanda maradufu kwa bei ya chakula mfano soko la Kahama mjini maharagwe yametoka 2000 mpaka 3000, mchele umetoka 1800 mpaka 2400/3000! Kuringana na Ripoti ya mamlaka ya utabiri wa hali ya Hewa Tanzania ya 2022, mikoa ya kaskazini ilikumbwa na ukame na mvua chache kwa kipindi cha Machi, 2022! Hali hii imepelekea kushuka kwa shughuli za kilimo katika mikoa ya kaskazini mfano Arusha n.k.

VIFO VYA MIFUGO KUTOKANA NA UPUNGUFU WA MAJI NA MALISHO
Hali hii imeshuhudiwa katika mikoa ya Katavi, Morogoro na hata Simiyu. Hapa tumetaja kwa uchache lakini hali si nzuri saana kwa wafugaji. Kutokana na ukame mazao mengine ya mifugo nayo yanashuka mfano ubora wa nyama na maziwa, "Ng'ombe katika kipindi cha ukame wanashuka uzito mpaka kufikia kilo 100...!" Abdala Ulega, Waziri wa kilimo, 2022( mkutano kukabiliana na athari za tabia nnchi wa 2.2.22).

KUONGEZEKA KWA JOTO
Wakazi katika majiji mfano Dar es Salaam, Dodoma na hata katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Simiyu n.k wameshuhudia kuongezeka kwa joto kuanzia mwezi wa 3 mpaka 11 katika mwaka 2022. Kwa mujibu wa ripoti ya Hali ya hewa ya Tanzania, mikoa ya Pwani na kaskazini ilikumbwa na halo hio mwezi Machi, 2022.

MAFURIKO NA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA MAJI, UMEME NA BARABARA
Hali hii imekua ikishuhudiwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. Uharibifu huu kwa kiasi kikubwa unaathiri maisha ya kila siku ya wakazi katika mikoa husika, vilevile inaigharimu serikali katika kufanya ukarabati wa miundombinu tajwa. Baada ya kuangalia kwa uchache athari hizi, zifuatazo ni njia zinazoweza kufanyika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nnchi.

MIPANGO YA KIMAENDELEO IJUMUISHAYO UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Mamlaka za kuandaa mipango ya kimaendeleo nnchini zinapaswa kujumuisha mipango jumuishi ya uhifadhi wa mazingira mfano. Liundwe takwa la kisheria kwa kila mdau wa maendeleo kupanda miti katika eneo lake la uwekezaji. Hilo limekua likishuhuduwa kwa wakulima wa Tumbaku katika mikoa ya Shinyanga na Tabora. Umefika muda sasa katika shughuli zote za uwekezaji wawekezaji watakiwe kuwa wahifadhi wa mazingira.

UJENZI UENDE SAMBAMBA NA UPANDAJI WA MITI
Mamlaka za mipango miji katika halmashauri mbalimbali ziwatake wamiliki wa viwanja katika miji na majiji kupanda miti na kihifadhi mazingira. Katika utoaji wa vibari vya ujenzi basi wajenzi watakwe kuacha mita kadhaa katika viwanja vyao kwa ajili ya kuotesha miti. Vilevile uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ujumuishe maeneo ya upandaji wa miti na uhifadhi wa uoto wa asili. Pia watu wa TANROADS na TARURA na wao waweke sheria inayotaka wajenzi wa barabara kuandaa "Green corridors" katika uandaaji na utekelezaji wa miradi ya barabara.

TAKWA BINAFSI LA UHIFADHI WA MAZINGIRA
Katika jamii, imezoeleka kwa wanajamii kutojali. Wananchi wamekua na kutojali kwa waharibifu wa mazingira kwa madai kua wameiachia jukumu hilo selikali!!!!! Shime kwa mwananchi mwenyewe kutunza, kukememea vitendo vya uharibifu wa mazingira na kuripoti juu ya uharibifu wa mazingira.

MATUMIZI YA NISHATI MBADALA
Hivi ni kweli mimi mwananchi wa kawaida ntamudu matumizi ya gesi? Hili ni swali ambalo wananchi wengi wamekua wakijiuliza.Kukabiliana na hili itabidi serikali ibuni mpango mkakati wa sabazaji wa nishati ambayo mwanachi wa kawaida anaweza kuimudu mfano (majiko yatumiayo nishati ya jua! Kama yapo ama elimu ya jinsi ya kutumia vinyesi vya wanyama kuandaa nishati n.k) shime kwa wanasayansi wazawa kuja na ubunifu kumsaidia mtanzania.

HITIMISHO
Mabadiliko ya tabia nnchi yana athari katika nyanja zoote za kimaendeleo, uwajibikaji jumuishi katika kukabiliana na janga hilo si jambo la kupuunzwa zaidi. Hivyo ndugu msomaji kaa na utafakari ni nini unaweza kufanya kukabiliana na janga hili ambalo kisababishi mkuu ni binadamu mwenyenye. Tafakari njema.
 
Upvote 3

Kuna Namna mengi ya haya huwa yanaishia kwenye makaratasi na makabati na droo za ofisi.... Ikizidi sana zinabaki katika folders kwenye computers.
 
Duu! Hatuna budi kuwakumbusha wahusika pasi na kuchoka.
Unaongelea climate change au climate variability mkuu?
Climate change
Unaongelea climate change au climate variability mkuu?
C

Climate change mkuu
 
Back
Top Bottom