Mabadiliko ya tabianchi yawafanya wanasayansi kuwa na wasiwasi zaidi kuhusu athari za sayari katika miaka ijayo

Mabadiliko ya tabianchi yawafanya wanasayansi kuwa na wasiwasi zaidi kuhusu athari za sayari katika miaka ijayo

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG31N1235746805.jpg

Kwa sasa kila mtu anatambua kuwa kadiri siku zinavyokwenda mbele ndio viwango vya joto duniani vinaendelea kuongezeka, dhana ambayo watu wengi walianza kuwa nayo akilini mwao miongo kadhaa iliyopita.

Tukitupia macho mwaka huu wa 2023 ambao ndio unaelekea ukingoni, tumeshuhudia kwa macho yetu majanga mengi zaidi yakitokea, yakiwemo moto wa msituni huko Hawaii, ukame katika Afrika, anga ya rangi ya machungwa katika Jiji la New York, na vimbunga viwili, Saola na Haikui, kusini mwa China.

Matukio haya yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi kwa sasa yanaathiri uchumi na jamii mara kwa mara hadi yamepewa jina maalum lijulikanalo kama “hatari ya hali ya hewa”. Kwa mujibu wa ripoti ya Huduma ya Mabadiliko ya Tabianchi ya Umoja wa Ulaya ya Copernicus, mwaka huu wa 2023 ni mwaka wenye joto kali zaidi kuwahi kurikodiwa, ambapo imeripotiwa hali ya hewa kupanda hadi zaidi ya nyuzi 1.46 (Fahrenheit 2.63) na kuwa ni kiwango cha juu zaidi kabla ya mapinduzi ya viwanda.

Ripoti hii mpya ya Copernicus ambayo ilitolewa wakati mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa Dubai (COP28) ukiwa unajiandaa kumaliza wiki yake ya kwanza ya mazungumzo, imesisitiza kuwa tangu mwezi Juni kumekuwa na rikodi mpya ya joto kali kila mwezi, ambapo mwezi Novemba ilikuwa ya kipekee kwa joto, na kufanya wanasayansi kuwa na wasiwasi zaidi kuhusu athari za sayari katika miaka ijayo.

Ikihusisha joto kali, mchanganyiko wa El Nino na mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na shughuli za binadamu za uchomaji wa makaa ya mawe, mafuta na gesi, ripoti hii imesisitiza nchi mbalimbali kuchukua hatua za haraka kuondoa hewa ya ukaa ili kupunguza hatari zinazoongezeka za hali mbaya ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mabadiliko ya tabia nchi sio suala linalohusu mazingira peke yake bali ni suala linalomhusu pia mwanadamu na maisha yake. Kwa sababu linaathiri mazao ya kilimo, mifugo, misitu na hata baadhi ya wakati makaazi ya watu.

Hali hii husababisha changamoto kubwa kuhusu uhakika wa upatikanaji wa chakula, kitu ambacho huathiri afya ya binadamu kwa ujumla wake, na pia husababisha kudorora kwa njia kuu anazotegemea binadamu katika kuendesha maisha yake. Hata hivyo, athari za mabadiliko ya tabia nchi na namna watu wanavyokabiliana nazo hutofautiana kutegemea na mahali.

Afrika Mashariki, eneo ambalo lina uchangiaji mdogo katika uzalishaji wa hewa chafuzi, sasa linaonekana kulipa gharama kubwa zaidi, na lipo kwenye taharuki ya kubeba mzigo mkubwa unaotokana na mabadiliko ya tabianchi. Watu wameteseka vya kutosha na ukame mkali uliokuwepo kati ya mwaka 2020 na 2022, na kama haitoshi sasa wanakabiliwa na janga jingine kubwa zaidi la mvua zinazoendelea za El Nino ambazo ni asilimia 140 juu ya viwango vya kawaida.

Mvua hizi zimesababisha maafa makubwa ya mafuriko na maporomoko ya udongo katika nchi za Kenya na Tanzania na kupelekea vifo, majeruhi ya watu wengi, pamoja na watu wengine wengi wakikosa makazi ya kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko.

Kwa mujibu wa takwimu, nchini Tanzania hadi sasa vimeripotiwa vifo vya watu 85 baada ya miili mingine zaidi kupatikana, na kwa mujibu wa ripoti idadi hii inaweza kuongezeka kwani shughuli za utafutaji miili kwenye tope bado zinaendelea.

Wakati yote haya yanatokea, viongozi mbalimbali duniani wamekutana kujadili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa uliofanyika huko Dubai kuanzia Novemba 30 hadi Disemba 12. Katika mkutano huo, nchi zaidi ya 100 zilikubaliana kuongeza mara tatu uwezo uliowekwa wa kimataifa wa kuzalisha nishati mbadala (nisati safi) ifikapo mwaka 2030.

Baadhi ya vyombo vya habari vya kigeni vinaona kuwa China ndiyo nchi pekee kubwa ambayo inatarajiwa kufikia lengo hili. Mtazamo huu unakuja kwasababu China kwa sasa inatilia maanani sana maendeleo ya nishati mbadala.

Katika kipindi kifupi, imebadilika kutoka mfuasi na kuwa kiongozi katika nishati mbadala, ambapo kiwango chake cha uzalishaji wa nishati hii kimeendelea kuwa cha juu.
 
Back
Top Bottom