Mabadiliko yafanyike kwa Jamii nzima ya watanzania

Mabadiliko yafanyike kwa Jamii nzima ya watanzania

bulajunior

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2024
Posts
624
Reaction score
898
Naomba namimi nichukue nafasi hii kutoa mawazo yangu:
Nimekutwa nikiona na kusikia reforms ambazo zinaendeshwa na kuenezwa nchi nzima na chama cha siasa kimoja hapa nchini. Watanzania wenzangu niseme kuwa tunakotaka kufika sio kwa namna hii tutajikuta tumeumizana sana hata hao viongozi nao ni binadamu najua wanapotumia dola kuumiza na wakati mwingine kuua watanzania wenzao kuna muda naamini wanajutia au watajutia tu.
Na hii ni kwa sababu asili zetu zinafanana wote sio viongozi au wananchi wa kawaida, nasema hivo kwa sababu hao viongozi wanaotuongoza kwa sasa wametoka humuhumu nchini na tabia zao hizihizi.
Kwa maana hiyo hata atokee mtu kutoka chama chochote mtanzania akawa kiongozi atakuwa hivihivi kama wengine kwa sababu sisi sote hatujafanya mabadiliko kitu ambacho sio jambo dogo linahitaji muda vizazi kadhaa vipite. Hili nikijariwa nitarifafanua zaidi kwenye uzi wake pekee.

Jamii yetu inawatu ambao hawawezi kuchukua hatua zenye faida ya muda mrefu Sisi tunaangalia faida ya muda mfupi tu. Nianze na wananchi wa kawaida, hawa watu hawachukui hatua za kumaliza tatizo kwa faida ya kutosumbuliwa au kuteswa na hata kuuliwa na serikali Yao hivo wanakaa kimya au kuwa na maamuzi ya hofu fulani wakiamini watakufa! na ndivyo ilivyo maana kuna vifo vinatokea na huwezi kusema vyote sio vya kweli vya uongo vinaweza kuwepo kama mambo ya siasa lakini lazima ukweli uwepo pia.
Sasa ndugu zangu watanzania tuna asili ya kupuuza na kusahau haraka mambo ya maana yenye tija kwa kizazi kijacho ndio maana hata ukiangalia hata kwenye mitandao humu utakuta watu wanajadili vitu vidogo vidogo sana na wakati huo kuja jambo muhimu tu la kiinchi linaendelea, wachache tu utakuta wanaongelea nao kwa manufaa Yao ya muda mfupi kama nilivosema mwanzo na hilo jambo litapita bila hatima nzuri au wachache hao watalimaliza.

Matokeo yake yakija negative watanzania wengi watazungumzia wengi wetu bila uelewa wowote yaani mkumbo tu na tutaliacha tena na kuwaachia wachache hao. Mambo siyataji Sana msomaji nakuachia utakuwa unajaza wewe kwenye akili yako. Na hii Hali bila mabadiliko ya kiujumla tutegemee kuwa hivi milele sisi ambao tupo saivi tutakufa na tutaacha watoto wanaishi hivihivi.

Nahamia kwa viongozi wa serikali na hata sehemu zingine makanisani na misikitini. Huku sitoongea sana maana nimesema hawa watu wanatoka kwenye Jamii moja hii madhaifu ni yaleyale. Na wao wanapuuzia kuchukua hatau muhimu kwa hofu ya kupoteza vyeo, mali, umaarufu, heshima na vingi wanavoviona wao ambavyo ni vya muda pia na havina faida kwa Jamii nzima ya watanzania labda kwa familia zao Tu na watu wa karibu kwao.
Mfano kuna viongozi wa dini walizungumza juzi hapa tunawasikia wote wakitaka amani ianzie kwenye mabadiliko lakini wamepuuzwa tayari na za ndani wengine hadi wananyofolewa na kuadhibiwa! Huko kote ni kupuuza mambo ya maana na ndio kimachotutesa watanzania.

Haya vurugu zetu nchini zinavuka mipaka hadi nje tunajadiliwa na wazungu huko na hawasiti kutupa nini tufanye lakini tunapuuza kwa kusema mabeberu wasituingilie. Jamani inawezekana ukakataa ushauri kwa mtu anaekuzidi na uhusiano wako na yeye, wewe ndio mnufaika kwa asilimia nyingi?
Juzi kati lilitokea janga la COVID 19 kama sikosei tulipata misaada kama sio mgao fulani, na kwa sababu sisi hatukuwa waathirika Sana tulitumia pesa hizo kujenga madarasa mashuleni kwetu. Kwanini hatukukataa kwamba mabeberu wasituingilie?
Lakini hata kiinchi tu ikitokea sehemu wananchi wabishi sio watiifu kwa viongozi wao tunaona wananyimwa maendeleo! kwa sababu hawawasikilizi viongozi wao. Sasa sisi kweli tupuuze ushauri wa wenzetu ambao niseme ni wakubwa kwetu natupate maendeleo?

Nahitimisha kwa kusema makosa yapo hata mimi kwenye ujumbe wangu huu naweza nikakosea kutokana na tafsiri ya mtu, lakini naamini message nzuri nayo ipo.
Asanteni sana
 
Back
Top Bottom