SoC04 Mabadiliko yanahitajika katika mfumo wa elimu ya Tanzania katika miaka kadhaa ijayo

SoC04 Mabadiliko yanahitajika katika mfumo wa elimu ya Tanzania katika miaka kadhaa ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

i_mukhsin_

New Member
Joined
Oct 5, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Katika elimu ya chuo kikuu.
1: Kwenye mfumo wa elimu ya chuo kikuu kwa sasa mwanafunzi anapoanza chuo huwa anasoma masomo mengi tofauti tofauti ambayo mengine ni nje ya kile ambacho amelenga kukisomea. Kwa maoni yangu mimi naona pale mwanafunzi anapoanza chuo kwa mwaka wa kwanza ningeshauri kuwa aende Direc kwenye kile ambacho anatarajia kukisomea. Kwa mfano, mtu anaesomea (bachelor of commerce in procurement and logistics management), ingefaa aanze kusoma procurement since first day anaingia chuoni. Na sio kujifunza vitu ambavyo havina umuhimu sana. Hii ingesaidia hata pale mtu anapoomba kazi basi awe specific na kile alichoomba na pia anakuwa na uwezo wa kufanya kutokana na kile alichosoma.

2: Pia katika miaka ya masomo ningependekeza kuwa kwa yule anaesomea kitu kama procurement basi asome darasani hata ile miaka miwili then ule mwaka wa tatu ( wa mwisho) at least awe kwenye sector husika ambayo inajihusisha na hiyo kozi ili mwanafunzi aweze kufanya kwa vitendo na kwa ufasaha wa hali ya juu na pia hata ikitokea mtu anaenda kuomba kazi basi anakuwa na uwezo wa hiyo kazi(experience) kwa vitendo na sio experience kwenye CV tu. Hii itasaidia nchi yetu kuwa na wasomi ambao ni wasomi wanaoweza kubadili nchi yetu kwa vitendo na sio maneno tyu. Taasisi nyingi siku hizi zinapotangaza nafasi za kazi huwa wanataka watu wenye uzoefu angalau mwaka au miaka kadhaa. Je, wanafunzi wanapomaliza chuo na tangazo la kazi likatoka huo uzoefu anatoa wapi.? Kwahiyo kutokana na mambo kama hayo nchi kama Tanzania tunatakiwa kufanya mabadiliko na kuweka elimu ya vitendo kabisa ili mtu aweze kusoma na kuelewa kile anachokisomea na aweze kukifanyia kazi kwa juhudi. Hii itasaidia kuleta weledi kazini na kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini na kijamii nchini.
 
Upvote 1
Kwenye mfumo wa elimu ya chuo kikuu kwa sasa mwanafunzi anapoanza chuo huwa anasoma masomo mengi tofauti tofauti ambayo mengine ni nje ya kile ambacho amelenga kukisomea. Kwa maoni yangu mimi naona pale mwanafunzi anapoanza chuo kwa mwaka wa kwanza ningeshauri kuwa aende Direc kwenye kile ambacho anatarajia kukisomea. Kwa mfano, mtu anaesomea (bachelor of commerce in procurement and logistics management), ingefaa aanze kusoma procurement since first day anaingia chuoni. Na sio kujifunza vitu ambavyo havina umuhimu sana.
Mmmh! Hapa umenishtua sana. Kwamba hata chuoni bado kuna changamoto ya kufundishwa usohitaji kwelii!?🤯. Tazama vizuri zaidi asee je? Nikipendekeza kwamba masomo yote yanakuwa na uhusiano na kasi yake mahsusi je bado nnakosea?

Na bandugu nina swali kwa wote wenye uelekeo wa kupunguza masomo je haitakuwa hatari kuyakataa maarifa.?

Pia katika miaka ya masomo ningependekeza kuwa kwa yule anaesomea kitu kama procurement basi asome darasani hata ile miaka miwili then ule mwaka wa tatu ( wa mwisho) at least awe kwenye sector husika ambayo inajihusisha na hiyo kozi ili mwanafunzi aweze kufanya kwa vitendo na kwa ufasaha wa hali ya juu na pia hata ikitokea mtu anaenda kuomba kazi basi anakuwa na uwezo wa hiyo kazi(experience) kwa vitendo na sio experience kwenye CV tu. Hii
Hii nzuri koasi chake ili akajue kazi kama kazi. Japo isije kwa gharama ya kukosa kuzisoma nadharia ambazo hatazikuta kazini. Maana tunajua fika baadhi ya kazi kwa jinsi zinavyofanyika utakuta ni kitendo kimoja mara sabini kwa siku, siku 365 na robo za mwaka. Kwa hivyo siki mazingira yakibadilika kidogo kama hakuna nadharia kamilifu watu watapoteana...
Tanzania tunatakiwa kufanya mabadiliko na kuweka elimu ya vitendo kabisa ili mtu aweze kusoma na kuelewa kile anachokisomea na aweze kukifanyia kazi kwa juhudi.
Ahsante
 
Back
Top Bottom