Mabaki haya ya kiutamduni yapaswa kurejeshwa kwa China

Mabaki haya ya kiutamduni yapaswa kurejeshwa kwa China

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
Vyombo vya habari vya Uingereza hivi karibuni vimeripoti kwamba Mfuko wa David ambao ni jumba binafsi la makumbusho la nchini Uingereza, utatoa takriban kauri 1,700 za kale za Kichina kwa Jumba la Makumbusho la Uingereza. Kauri hizo zenye thamani ya paundi bilioni moja za Kiingereza zina historia ndefu na thamani kubwa ya kiutamduni.

Kwa lugha ya Kiingereza, kauri na China ni neno moja. Kauri za kale sio tu ni hazina ya sanaa, bali pia ni ushahidi wa historia na utamaduni wa China, na Mfuko wa David haupaswi kuchangia kauri hizo kwa Jumba la Makumbusho la Uingereza, bali inapaswa kuzirudisha China.


Katika miaka ya 1920 na 1930, mfuko huo ulikusanya kauri hizo za kale kutoka nchini China kwa njia mbalimbali na kuzisafirisha hadi Uingereza. Wakati huo, China ilikuwa katika kipindi cha vita vya mara kwa mara na machafuko ya kijamii, na pia ilikuwa ikinyanyaswa na nchi za kigeni, ikiwemo Uingereza.


Kama zamani Mfuko wa David uliweza kupora, basi leo unapaswa kubadilisha mawazo yake na kurudisha mabaki haya ya kitamaduni kwa China. Ikiwa ulikuwa na nia njema ya kuzihifadhi kauri hizo, basi sasa China ni nchi yenye nguvu na utulivu, kauri hizo zinapaswa kurejeshwa kwa China mara moja.

Lakini sasa, badala ya kuzirudisha kwa wamiliki wake wa awali, Mfuko wa David umetoa mabaki hayo ya kiutamaduni ya China yenye thamani kubwa kwa Jumba la Makumbusho la Uingereza.

Kama tunavyojua, historia ya Jumba la Makumbusho la Uingereza ni historia chafu ya uporaji wa kikoloni. Takwimu zinaonesha kuwa, kuna takriban mabaki 23,000 ya kitamaduni ya China kwenye jumba hilo, na kati ya mabaki hayo, mengi yaliporwa na wavamizi wa Uingereza wakati wa vita dhidi ya China zaidi miaka 100 iliyopita.

Mbali na mabaki ya utamaduni ya China, mabaki mengine mengi ya kitamaduni katika Jumba la Makumbusho la Uingereza yana alama za uporaji na wizi, yakiwemo mabaki ya kitamaduni ya Kiafrika yenye thamani kubwa. Kulingana na takwimu, kuna mabaki takriban 200,000 ya kitamaduni katika Jumba hilo yanayotoka bara la Afrika.

Katika miaka mingi iliyopita, nchi nyingi za Afrika zikiwemo Misri, Nigeria, Kenya, na Ethiopia, zimekuwa zikijitahidi kurudisha mabaki yao ya kitamaduni yaliyoporwa na Uingereza, lakini zote zimekabiliwa na changamoto kubwa kama China.

Mabaki ya kitamaduni ni alama ya utamaduni na historia ya nchi. Hojaji iliyofanywa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) mwishoni mwa mwaka jana kati ya watumiaji wa mtandao duniani kote inaonesha kuwa, asilimia 90.3 ya watu waliohojiwa wanaona kwamba, mabaki ya kitamaduni yaliyoporwa na Uingereza yanapaswa kurejeshwa kwa nchi zao za asili haraka iwezekanavyo, na maumivu ya kikoloni hayawezi kuruhusiwa kuendelea.
 
Back
Top Bottom