Odhiambo cairo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,989
- 22,078
Kumbe pamoja na kukaa Marekani na kufanya kazi huko bado ni zero brain ?!Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Africa Mashariki , Mtukufu Mulamula , ambaye amewataka mabalozi hao kufuata sheria na taratibu za kidiplomasia , hakufafanua taratibu hizo kama zinawakataza mabalozi kuhudhuria kesi mahakamani au la .
View attachment 1900584
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amewataka mabalozi wanaokwenda mahakamani kufuatilia mwenendo ya kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufuata sheria na taratibu za kidiplomasia.
Balozi Mulamula ameyasema hayo leo Agosti 20,2021 jijini Dar es Salaama wakati akizungumza na mabalozi, wakuu wa taasisi na mashirika ya kimataifa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Lilongwe, Malawi Agosti 17–18.
Katika mkutano huo, Balozi Mulamula amesisitiza kwamba mabalozi wanaokwenda mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi ya Mbowe kufuata sheria na taratibu za kimataifa za kidiplomasia ili kujiepusha na ukiukwaji wa sheria na taratibu hizo.
Chanzo: Mwananchi
Masikini Tanzania na wasomi wake !!