Mabao 3 pekee msimu uliopita! Je, Shalulile atafanikiwa kuibeba Yanga?

Mabao 3 pekee msimu uliopita! Je, Shalulile atafanikiwa kuibeba Yanga?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
1785224865390.png

Mshambuliaji hatari wa kimataifa wa Namibia, Peter Shalulile, alihitimisha msimu wa 2025/26 wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini akiwa na mabao matatu katika mechi 13 alizoichezea klabu ya Mamelodi Sundowns.

Soma: PETER SHALULILE rasmi ni mwananchi Yanga. Asante GSM kwa kuendelea kuonyesha upendo

SHA.png
🟄 Idadi ya mechi alizocheza - 13

Mabao yote matatu ya Shalulile yamepatikana kwenye michezo tofauti:
  1. Dhidi ya Magesi FC (20/08): Alifunga bao 1 katika ushindi wa mabao 2-0 ugenini.
  2. Dhidi ya Stellenbosch FC (30/08): Alifunga bao la ushindi (1-0) wakiwa ugenini.
  3. Dhidi ya Orlando Pirates (01/11): Alifunga bao 1 katika sare ya 1-1 nyumbani.
Tangu alipofunga bao lake la mwisho mnamo Novemba 1, 2025 dhidi ya Orlando Pirates, Shalulile amekuwa kwenye ukame wa mabao kwa michezo sita (6) mfululizo aliyocheza dhidi ya TS Galaxy, Sekhukhune United, Orlando Pirates, Richards Bay, Polokwane City, na Kaizer Chiefs.

Katika msimu huo, Shalulile alianza kikosi cha kwanza mara saba, akacheza dakika 562 bila kutoa asisti yoyote, huku akipata wastani wa alama 6.64 kwa mujibu wa tathmini za kiwango chake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anaondoka Sundowns akiwa ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo. Akiwa huko, alitwaa mataji matano ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Kombe la Nedbank, taji la MTN8, Kombe la African Football League na Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Shalulile ameandika historia kama mmoja wa washambuliaji bora kuwahi kucheza Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL), akihitimisha safari yake nchini humo akiwa amefunga zaidi ya mabao 130 na kuvunja rekodi ya mabao 129 iliyokuwa ikishikiliwa na Siyabonga "Bhele" Nomvethe.

Shalulile sasa anaanza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka na Yanga SC baada ya kuondoka Mamelodi Sundowns, huku mashabiki wakisubiri kuona kama ataendelea na kiwango chake akiwa na timu yake mpya.
 
Akili za mashabiki wanajua kasajiliwa yule Shelulile MVP wa msimu wa 2019/2020.😁

BTW:Hakupata nafasi kikosi cha kwanza hizo mechi 13 ni sub tupu ni dakika chache mno kwa mechi.
 
Kwa hii amateur ligi atafunga sana tu na usishangae akawa top scorer


We ligi timu zinazotoa ushindani ni tatu tu
 
Kwa hii amateur ligi atafunga sana tu na usishangae akawa top scorer


We ligi timu zinazotoa ushindani ni tatu tu
Haswaaa, Shalulile atakiwasha sana, league haina ushindani wowote.
 
Akili za mashabiki wanajua kasajiliwa yule Shelulile MVP wa msimu wa 2019/2020.😁

BTW:Hakupata nafasi kikosi cha kwanza hizo mechi 13 ni sub tupu ni dakika chache mno kwa mechi.
Bado haiondoi ukweli Peter Shalulile ni mchezaji mwenye mafanikio. Lakini pia ana nidhamu ndani na nje ya uwanja. Msimu uliopita ni kweli alicheza mechi chache kutokana na majeraha, na pia kuja kwa kocha mpya kwenye timu yao. Hili ni jambo la kawaida sana kwa mchezaji.
Tusubiri muda ufike ili ukweli ujulikane.
 
Watanzania ndivyo walivyo, watamsifia wee wakati hana lolote kwani ameshaisha na kuzeeka vilevile ndio maana hata huko Mamelodi akatemwa.

Wanaoweka matumaini makubwa kwa huyo mnamibia watakuja kujuta kwani hana maajabu yoyote aliyonayo.

Mchezaji yeyote mzuri hawezi kuja kucheza mpira Tanzania, hilo nalikataa ni vikaragosi tu ndivyo vinavyokuja hapa.

It's the time that perfects everything so time will tell in not so distant futurefuture.
 
Back
Top Bottom