Mshambuliaji hatari wa kimataifa wa Namibia, Peter Shalulile, alihitimisha msimu wa 2025/26 wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini akiwa na mabao matatu katika mechi 13 alizoichezea klabu ya Mamelodi Sundowns.
Soma:
PETER SHALULILE rasmi ni mwananchi Yanga. Asante GSM kwa kuendelea kuonyesha upendo
π₯ Idadi ya mechi alizocheza -
13
Mabao yote matatu ya Shalulile yamepatikana kwenye michezo tofauti:
- Dhidi ya Magesi FC (20/08): Alifunga bao 1 katika ushindi wa mabao 2-0 ugenini.
- Dhidi ya Stellenbosch FC (30/08): Alifunga bao la ushindi (1-0) wakiwa ugenini.
- Dhidi ya Orlando Pirates (01/11): Alifunga bao 1 katika sare ya 1-1 nyumbani.
Tangu alipofunga bao lake la mwisho mnamo
Novemba 1, 2025 dhidi ya Orlando Pirates, Shalulile amekuwa kwenye ukame wa mabao kwa michezo sita (6) mfululizo aliyocheza dhidi ya TS Galaxy, Sekhukhune United, Orlando Pirates, Richards Bay, Polokwane City, na Kaizer Chiefs.
Katika msimu huo, Shalulile alianza kikosi cha kwanza mara saba, akacheza dakika 562 bila kutoa asisti yoyote, huku akipata wastani wa alama 6.64 kwa mujibu wa tathmini za kiwango chake.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anaondoka Sundowns akiwa ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo. Akiwa huko, alitwaa mataji matano ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Kombe la Nedbank, taji la MTN8, Kombe la African Football League na Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.
Shalulile ameandika historia kama mmoja wa washambuliaji bora kuwahi kucheza Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL), akihitimisha safari yake nchini humo akiwa amefunga zaidi ya mabao 130 na kuvunja rekodi ya mabao 129 iliyokuwa ikishikiliwa na Siyabonga "Bhele" Nomvethe.
Shalulile sasa anaanza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka na Yanga SC baada ya kuondoka Mamelodi Sundowns, huku mashabiki wakisubiri kuona kama ataendelea na kiwango chake akiwa na timu yake mpya.