Mabasi aina ya Scania na Mercedes Benz vs Yutong na Zongtong: Mchina ameuza ramani ya vita kwa adui

Nani kasema kwamba Kilimanjaro ana f330?? Iso izo 94 Kilimanjaro anaweka kwenye polo pia p series ambazo ni 95 za lorry, labda nikuelekeze vizuri f330 overhang yake ni ndogo sana pale mbele tyre za mbele ziko mbele zaidi ya 94, na nilikuambia nilikuambia pamoja na specification zake f330 bado ni special bus kama hutaki niletee f330 iliyo na kibin ya lorry tuache kubishana kama hauna basu jua f330 sio lorry usibishe kitu kilicho wazi, pili nilikuuliza straight kuhusu f360 na ulichojibu ndicho unachokifahamu hakuna mtego pale.
 
Mkuu..
Napenda tu mnavyobishana kwa point na facts, ila hapa mmh mmh..kama unakana kauli yako mwenyewe vile
 

Unafahamu kwa nini overhanga ya f330 Ni ndogo pale mbele ?
Unafahamu mkono wa stearing kwenye lori ni mfupi kushinda wa basi?
Unaposema kuwa tairi za mbele kwenye f330 zipo mbele hufikirii kuwa umeshajifunga kwenye kile ulichokiamini? Na kwamba una prove kuwa hiyo Ni chassis ya Lori?
Umeshawahi Pima wheel base ya Lori ukaona utofauti wake na wheel base ya basi?

Scania 94 inakuja katika version ya basi na Lori mkono wa stearing wa 94l huwa unafungiana na f330 , 124 ,144,164 , Ila ikishakuwa 94 basi mkono huo haufungi kokote zaidi ya basi mwenzake .

F330 ndio 114 340, zinafungiana kila kifaaa hakuna tofauti

Sent
 
Mkuu..
Napenda tu mnavyobishana kwa point na facts, ila hapa mmh mmh..kama unakana kauli yako mwenyewe vile
Kitendo tu cha kusema kuwa f330 Ina over hang ndogo tayari kajichanganya, Lori pekee inakuja na overhang ndogo ,kwa basi lazima tairi la mbele liwe nyuma ya dereva. Ni moja ya sababu f330 hazikuuzwa Kama basi ulaya
Akiendelea nitamchambulia na kumtofautishia suspension systems za Lori amabazo f330 inatumia

Sent
 
Lakini mkuu lory gani f330 ulishawahi kuona kweli
 
Mkuu..
Napenda tu mnavyobishana kwa point na facts, ila hapa mmh mmh..kama unakana kauli yako mwenyewe vile
Sikani nilichomaanisha Kilimanjaro anavisha chasis zq lorry sasa kama lorry zinakaa kwa mlango mbele nilikuwa najibu hoja ya kwamba f330 ni lorry ndio maana zina mlango kati.

Msimamo wangu ni kupinga kwamba f330 ni lorry kwa sababu tuu inafanana na malory kwa muundo chasis yake ilihali hakuna lorry linalotumia chasis ya f330
 
Lakini mkuu lory gani f330 ulishawahi kuona kweli
Mkuu mm nakuambia jamaa anajichanganya yeye na wala si mm nakupa fact

Jamaa amesema kwamba overhang kuwa fupi mbele tayari ni lorry namuuliza je anazijua scania L series?? Je anajua kwamba scania wanazo lorry zenye overhang ndefu nitaleta ushahidi.

Scania wameamua kutengeneza f330 kwa sababu zao na wameamua ziwe kwaajili ya bus tuu na si kubeba mizigo kwa sababu zao na mzungu sio mjinga ndio maana unaona hadi leo hakuna lorry ya f330 sasa anakuja mtu na sababu ambazo hazijashiba hatuwezi muelewa.
 
Nakukumbusha tuu ukiendelea msimamo wako wa OVERHANG fupi ni kwa malori hapo chini unitajie majina ya hayo mabasi kwenye picha mkuu
 
Achana na L series mkuu mwanza ipo p270 ni garbage truck ina overhanging ndefu balaa

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
Lakini mkuu lory gani f330 ulishawahi kuona kweli
safi kabisa ili uelewe kinachoongelewa ni vema kwanza ukafahamu naming ya scania engines pamona na chassis zake
series 1 hadi 3 walikuwa wana name uwezo wa engine kwanza , then series , aina ya chassis then kulikuwa horse power pembeni 113m 320 hapa ilikuwa 11 ni ujazo wa engine 3 ni series ,m ni medium duty chassis na 320ni horsepower

series 4 wali name kwa ujazo wa engine , then series then aina ya kazi gari iliyokuwa designed kufanya then horse powers, md 124l 400hp, 12 ni ujazo wa engine , 4 ni series L ni long haulage na 400 ni horsepower
ilipokuja series 5 , wakaamua Ku name kutokana na cabins pamoja na horsepower, ujazo wa engine kutoka hapo haukuzingatiwa tena, sababu kulikuwa na horsepower za aina moja kwa engine zaidi ya moja
mfano p360 p ni cabin ndogo na 360 ni horsepower, G ni cabin ya sleeper R ni sleeper ya double bed,T ni ile yenye bonnet, F ni kwa engine ya mbele bila cabin na k , ni kwa engine nyuma bila cabin.

F330 inayozungumziwa hapa ilitoka katika kipindi euro 3 ,specification zinaanza ku fade out. technically ilikuwa ni series 4 za mwishoni ndio sababu hata horsepower number hawakuzi round off , sababu ilikuwa named kwa principles za series 5 , nimetoa mfano hats hiyo 114 340 hp kwenye technical sheets haikuwa 340 hp wali round off kwa mbwebwe zao tu

hutaona lori imeandikwa F330 , for sure ila technical sheet ya 114 340 inaonesha ni 334 horsepower, 114 380 ni 370 horsepower kwenye sheet yake
 
Unachozungumzia hapa ni kwamba f330 ndio iyo iyo 114-340?? Tuzungumzie f330 kama 330 mm nina amini hata engine head haziingiliani mkuu simama kwenye mada.
 
Swali langu nakuuliza je ulishaona 114 330 au 124 330 au 113 330 maana mimi ninachojua hizo walitoa kwa ajili bus
 
Unaendelea kukurupuka, 114 kwa nn isikae kwenye bus?

Kuna ile gari ilikuwa inatoka tanga kwenda singida au shinyanga ilikua na engine ya R420
 

F330 hata ukiuliza Saab scania ilikuwa ni basi ya dharula tu , hata ulaya hazikuuzwa ! hapa kwenyewe Tanzania wachache sana walimiliki hiyo basi, na wali feli miserably moja ya sababu ni kuwa specification zake zilikuwa ni za lory so nightmares kwa bus owners, zilikuwa very heavy kwenye diesel japo pia nguvu ilikuwepo ya kutosha .kama unakumbuka Allys bus service ,Leina Tours , ndo ilikuwa habari ya F330!

kuhusu scania kuwa na lori zenye overhang ndefu ,ukiacha gari za kubeba takataka ulaya sio kitu cha kawaida , nafahamu L series , ilikuwa ni series 4 , series 4 lori zote zina share chassis parts , except T series ambayo ni bonnetted version na ilishakuwa discontinued
 
Oil au fuel?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…