Thanks for compliment na thanks pia kwa kunipa pole kuhusu kuvamiwa na vibaka , ninmiaka kumi Sasa imepita nikikumbuka ni Kama Jana tu maaana Nina kilema Cha kidole , ilinibidi Hadi nibadilishe signatures zangu kadhaa maana wakati huo nikiwa timamu nilikuwa na signature moja matata sana , sikujua Kama ilitegemea sana kidole hicho kilichokatika baada ya tukio!!!
Tukija kwenye magari mie hata Sina vyeo hivo Ila naipenda sana scania kwa kiasi flani wengi wanasema naijua , tukija kwenye V8 s huko ndio Kuna stories nyingi, hata hii slogan yao ya "when emotion meets logic " ni slogan mpya wanaitumia mwaka huu kwa 770 Ila naamini kwa waliowahi kutumia V8 hata zile za nyuma Wana Jambo la kusema !! Kuna emotion feelings flani unapata ukiendesha V8 especially likiwa loaded na Lina high milage , those monsters will get you home any how , hata Kama limechoka kiasi gani!!
Kuna mwaka flan tulipat kazi ya kusafirisha mtambo wa mzungu mmoja kutoka dar kwenda Rwanda , ilikuwa ni njia yenye milima sana ukitokea Kigali mtambo ulikuwa ni heat echanger ambayo ilikuwa imekuwa disassembled kwenye trailer 13, kwa Bahati mbaya gari yetu ndio ilionekana ni nzee Kati ya gari zote na supervisor wa mzigo Ali I rule out kwamba kwa thamani ya mzigo na terrain unapokwenda mzigo isingefaa kubebwa na gari yetu , ni 164 480 ya mwaka 2000 na wakati huo na ilikuwa ina Kama Miaka 15 , plus 2 millions km on the clock, bas baada ya vikao vya hapa na pale , tukamjenga transport officer akakubali tupakie kwa masharti ya rate pungufu ili apate pesa ya Maji...!! Kiukweli kazi ilikuwa inalipwa vzr . Kilichotokea huko rwanda gari mbili Kati ya zile pamba zilishindwa kufika eneo la tukio , moja ilikufa Engine km 110 nyuma na nyingine ikauwa gearbox layshaft km 90 kabla ya site , site manager akatoa offer ya kwenda kuvuta zile trailers , wote wakakataa , ikabidi tujitoe muhanga maana bila trela zote kutimia delivery note ilikuwa haisainiwi kwa yoyote hivyo tungepoteza muda sana pale tukaenda kuchukua trela ya kwanza tukaileta site , tukafata ya pili tukaleta site , then tukaenda kupakia horse zote mbili , kurudi dar , Sasa Ile feeling nilisikia wakati narudi nyumbani huku tumezibeba gari mbili ambazo zilitumika Kama kielelezo cha kutunyima kazi ,.. I'll just never forget that, [emoji16][emoji16], V8 zina sauti flan ya mamlaka , very sweet , and deep pound to pound note . Tulipo fika dar ndio tulikuwa gumzo kwenye Ile ofisi na tukalipwa rate Ile Ile ya wenzetu plus gharama ya kuzibeba horse na kuifikisha site zile trela ,