Mabasi mapya ya Shabiby Express yatajwa kuwa bora zaidi Tanzania

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
317
Reaction score
520
Hivi karibuni, mfanyabiashara na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby ameingiza mabasi 12 ya kisasa aina ya Yutong.

Inaelezwa kuwa, mabasi hayo ni ya aina yake nchini kwani yana mfumo wa kisasa wa ubebaji wa abiria. Ndani ya mabasi hayo, unakutana na viti vyenye mpangilio tofauti na mabasi ya zamani. Upande mmoja, una siti mbili kwa abiria wawili. Upande mwingine una siti moja kwa abiria mmoja.

Sifa nyingine, kila siti ina televisheni yake. Ina mfumo wa kuchajia simu na mfumo wa kusikiliza redio ya simu ya mkononi (earphone).
Sifa nyingine, Basi zima lina siti 34 tu.

Tangu kuanza kwa usafiri wa mabasi hayo, abiria wanaotoka Dar kwenda Dodoma wamekuwa wakichangamkia kupita kawaida. Maeneleo Tanzania.

 
Haya mabasi tayari walikuwa nalo moja tokea miaka 3 au 2 iliopita kama sikosei kabla ya haya mapya.
 
Hujataja nauli brother...
 
Kuna mwana mmoja kbl ya kupanda bus anaomba chart ya siti aone majina ya abiria, siti anayochagua inategemea na jina analoliona kwenye siti.
Nipale unapokutana na jina la Janet ukajua binti kumbe mzee
 
Nipale unapokutana na jina la Janet ukajua binti kumbe mzee
Unatakiwa kuwa strategical, unampoza na Buku 2 Mkatushab tiket ili apate kumbukumbu nzur za janet.... au unamwambia nipe siti nzur ilinkufupisha safari wao wanajuaga!!
 
Kuna mwana mmoja kbl ya kupanda bus anaomba chart ya siti aone majina ya abiria, siti anayochagua inategemea na jina analoliona kwenye siti.
Unakutana na Jina Beatrice Dominic unajua bonge la Pisi. Kumbe ni yule mmama mkurugenzi Mnoko Wa Ubungo..
 

Tahmeed walikua nalo siku mwaka 2016 na sasa wameyatoa barabarani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…