Mabasi mapya ya Shabiby Express yatajwa kuwa bora zaidi Tanzania

Mabasi mapya ya Shabiby Express yatajwa kuwa bora zaidi Tanzania

Hivi karibuni, mfanyabiashara na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby ameingiza mabasi 12 ya kisasa aina ya Yutong.

Inaelezwa kuwa, mabasi hayo ni ya aina yake nchini kwani yana mfumo wa kisasa wa ubebaji wa abiria. Ndani ya mabasi hayo, unakutana na viti vyenye mpangilio tofauti na mabasi ya zamani. Upande mmoja, una siti mbili kwa abiria wawili. Upande mwingine una siti moja kwa abiria mmoja.

Sifa nyingine, kila siti ina televisheni yake. Ina mfumo wa kuchajia simu na mfumo wa kusikiliza redio ya simu ya mkononi (earphone).
Sifa nyingine, Basi zima lina siti 34 tu.

Tangu kuanza kwa usafiri wa mabasi hayo, abiria wanaotoka Dar kwenda Dodoma wamekuwa wakichangamkia kupita kawaida. Maeneleo Tanzania.

View attachment 1747373View attachment 1747374View attachment 1747375View attachment 1747376
Safiii sana
 
Tahmeed walikua nalo siku mwaka 2016 na sasa wameyatoa barabarani...
Siku hizi wanayo ya 1x1x1....yaani colum tatu...njia mbili za kupita..hakuna ujirani mwema wala hakuna kugusana 😬
 
Back
Top Bottom