Mabasi mengi ya kisasa yana kamera, tunaamini waliomteka Hayati Ali Kibao wanajulikana. Polisi waanzie hapa

Mabasi mengi ya kisasa yana kamera, tunaamini waliomteka Hayati Ali Kibao wanajulikana. Polisi waanzie hapa

Mbona hakuna abiria aliyekuwa ndani ya hilo bus aliyesema chochote mpaka sasa?!
Hata dereva hata kampuni haijasema chochote.
Watanzania hawataki mambo mengi, juzi tu hapo madereva wa maliri ya Rwanda inasemekana walimuua dereva wa basi, mbele ya abiria lakini si mwajiri wala yeyote aliyeongea chochote wala abiria aliyejaribu hata kugombelezea
 
Wakifanya hivyo ndiyo tunapigia mstari kwamba wao ndiyo wanahusika ,hadi sasa tunajua ni "Wasiojulikana" ila wakiondoa kamera tuna conclude tu......Boni Yai /MMM/Ndugu wa meddy waende ofisi za hilo Buis waombe CCTV Footage haraka iwezekanavyo.
Yaaniiii wameshazitoaa trust me
 
sema basi zima hakuna raia aliyerekodi tunakwama sana wananchi kwa kuzingatia malalamiko ya matukio kama haya
Si ajabu unaongea hayo ukiwa hauna uzoefu wa kuwekwa chini ya ulinzi hata na panya road tu.

Lile ni tukio halisi kijana sio movie, watu wana silaha za kivita mkononi hata ungekua wewe ungepata wapi ujasiri wa kutoa iyo simu kurekodi
 
Alitekwa Mo Dewji camera hazikusaidia! Alipigwa risasi Tundu Lissu camera hazikusaidia.. Tuzidishe dua ili wasipate ufahamu,waje wajutie baadae.
Kamera ziliondolewa,baada ya Tundu Lisu kupigwa risasi.

Kwa hiyo sehemu yenye kamera inaweza kuondolewa au taarifa kufutwa.

Na uchunguzi ukafanyika,taarifa haikutoka mpaka leo.

Ipo siku ukweli utasemwa,na haki itatendeka!

Wanaofanya uhalifu huu ni binadamu wenzetu,ni Watanzania waliokosa na kushindwa hoja hadharani na sasa wanaishi kwa kuvizia,na kuleta madhara .

Kuua ni udhaifu,ni jambo ambalo limeigwa nchi jirani(Tanzania hatukuwa na utamaduni wa kutekana)
 
Unisamehe kwa kuzungumza haya, INAONEKANA CDM MPAKA SASA HAMNA CHA KUFANYA KULINDA WANACHAMA WENU ZAIDI YA KUMTEGEMEA ADUI YULEYULE ATOE MSAADA na hamna ndio mnampa advantage zaidi ya kuwaoveride, lazima muwe matured sasa.

huwezi kuiambia Serikali au polisi ambao tayari ni watuhumiwa eti wakwambie kama lile basi lina Camera au halina au kuwataka walewale watuhumiwa wafanye uchunguzi.

Wanafanya uchunguzi watakwambia Marehemu alikuwa anatembea na mke wa mtu au alidhurumu watu ( sorry for this, ni mfano tu), itaishia hapo watakamatwa watu feki ambao hata tayari ni wafungwa ambao sentenced to death watapelekwa mahakamani watafungwa second time kwa special promise.

Tegeta bus linatekwa tena kwa kuliblock kwa mbele na watu wameshika silaha hadharani, hii confidence inatoka wapi?

Nafikiri CDM kama kweli Mkoa serious na haya mambo dhidi ya wanachama wenu, basi mnapaswa kuwa serious kidogo nyie kama nyie bila kuzitegemea mamlaka, kuzitegemea mamlaka zilezile mnazozituhumu haileti maana, harakati zozote huwa zina gharama zake na hizi ndio gharama ambazo chadema na wafuasi wake mnapaswa kulipa.
 
sema basi zima hakuna raia aliyerekodi tunakwama sana wananchi kwa kuzingatia malalamiko ya matukio kama haya
Mabasi yana orodha ya abiria waliosafiri kwa three na siku husika(Manifest).
Tiketi hutolewa kwa njia ya mtandao na namba za simu zipo (katika wote waliokuwepo kwenye basi wapo wenye uwezo wa kutoa maelezo sahihi).
Hii sitegemei wachunguzi wakose pakuanzia
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mabasi yana orodha ya abiria waliosafiri kwa three na siku husika(Manifest).
Tiketi hutolewa kwa njia ya mtandao na namba za simu zipo (katika wote waliokuwepo kwenye basi wapo wenye uwezo wa kutoa maelezo sahihi).
Hii sitegemei wachunguzi wakose pakuanzia
Safi mkuu
 
Si ajabu unaongea hayo ukiwa hauna uzoefu wa kuwekwa chini ya ulinzi hata na panya road tu.

Lile ni tukio halisi kijana sio movie, watu wana silaha za kivita mkononi hata ungekua wewe ungepata wapi ujasiri wa kutoa iyo simu kurekodi
Sawa mkuu, acha watu waendelee kutekwa. Kama wananchi wenyewe wa umoja wao hawawezi shirikiana basi zima kuanza kurekodi. Tanzania hii itaokolewa na miujiza
 
Hao abiria waliokuwa kwenye hilo gari wako wapi mpaka sasa kusema jambo? Kwahy baada ya tukio Bus likaendelea na safari yake kama vile hakuna lililotokea?

Kwa akili zetu za kibongo lazima kuna mtu alichomoa simu yake na kuanza kurikodi hilo tukio, hy video iko wapi?

C alichukuliwa mbele ya wanausalama wa barabarani, walifanya nini?

Sio kila gari la kisasa lina Camera, huo n uongo. Kuwa na camera na kuweza ku-operating camera n vitu viwili tofauti.
 
Chadema: Tunaishtumu serikali kwa haya yanayoendelea.

Chadema: Tunaiomba serikali ishughulikie haya mambo yanayoendelea.


Guys, hatuwezi kufika kwa style hii.
 
Nafikiri jibu unalo mwenyewe
Safi, na ndo mana nasema JPM alisingiziwa mabaya mengi mana hayo mambo yalikuwepo hata kabla yake ila baada ya kuongeza kuwabana Chadema ndio mana kelele zilikuwa nyingi tofauti na watangulizi wake.
 
Back
Top Bottom