by default
JF-Expert Member
- Jul 11, 2011
- 839
- 215
..Kuna Kadada huwa kapo hapo Ofisi yao ya Arusha mahali wanapotoa mizigo(Parcels), kwanza muda wote Kamenuna, pili Customer Service sifuri, tatu kana Majibu ya kunya, Nne kabaya.....Tano.......Weshashiba hela hao! Ukienda kata ticket hasa ofisi za Arusha , Vibinti walaaa havijali ndo kwanza vinavuta tumidomo twaoo!!! Mie nlipoona hivyo huyoooo nkaondoka kwenda kata Kilimanjaro ya nini shida yakhee? Weshashiba pesa wajiona matawi ya juu kumbe hata mchicha umewazidi kimo ati....
Jirekebisheni.......
Nendeni mkajifunze customer care...... Mabasi yenye nidhamu mengi siku hizi
Ulizeni njia ya Dar Mwanza Mtaambiwa...:wacko:
Kwakweli nimesoma hizi Taarifa kwamasikitiko makubwa,Nashukuru sana nimeiona hii thread.Mimi si mmiliki ila namfahamu vizuri mmiliki maana kwangu nindugu kabisa nawahakikishia namjulisha sasa hivi!Nantamuomba akinuruhusu nitaweka namba yake hapa ili wana jf mpatapo shida muwasiliane nae mojakwamoja!Kwasasa mnaweza muona anakwa ana pale nyerere road karibu nakiwanda cha Sigara uliza ofisi za Dar ex,anakuwepo karibu kilasiku kuanzia saa kumi namoja jioni.Uliza Mkurugenzi.Kwakweli wafanyakazi au mfanyakazi akisikia unaenda kumshitaki atakuomba msamaha yuko more than makini!
tafadhali fanya hivyo.....tena ikiwezekana aje hapa asome comment za watu.....na ikibidi ajisajili ili tumuulize maswali ya papo kwa hapo.....ni biashara ile bana......
Liver pool Hotel (MOMBO) ndiyo pekee inayoongoza kwa UCHAFU, tena mabwana afya sidhani kama huikagua!! Jamani, hawa wamiliki washauriwe.
wewe kama ni mfuatiliaji habari kwenye vyombo vya habari kama mitandao,tv,radio na vyanzo vingine vya habari kuna mpango unasukwa wa kuleta magari ya kusafirisha abiria ya mafisadi flani,sasa ushindani mkubwa wa kibiashara kwa usafiri wa arusha to dar huyu jamaa wa dar express huduma zake zimevutia watu wengi wanaofanya safari kwenye njia hiyo.lini umesikia hayo magari yamesababisha ajali kubwa kama hyo mengine ambayo kilakukicha huachikusikia yamesababisha ajali,japo kua hakuna anaeweza kutabiri ajali au kupenda litokee,au kutokupata ajali ni ujanja,simaanishi hivyo ila tahadhari inatakiwa ichukuliwe mapema,kivipi.....mfano kuwa na magari yenye standard inayokubalika kimataifa,angalia mabasi ya dar express sio ya kuunga unga kama hayo mengi yaliopo barabarani,angalia madereva wake kuanzia mavazi mpaka muonekano wa mtu,wewe kama ni mlevi na mla mirungi na ulevi wowote pale kazi hupati ndugu yangu,angalia madereva wa magari mengine unawakuta wapo rufly na uhuni usio na mpango barabarani.ustaarabu kwa ujumla pale dar express ni standard yaani unaokidhi haja.
Preta nalishugulikia hili,Ila nimeongea namkurugenzi amesikitika sana kwamatatizo ambayo wateja wake wanayapata ktk huduma yake bila yeye kujua!Anaomba mnapopata shida mumjulishe mara moja ili aweze kuchukua hatua!Mtapata namba yk soon.Kwasasa fuata maelekezo niliyatoa hapo juu namana yakumpata.
Mkuu, Mabasi yaliyofungiwa ni 14 tu. Dar Express wana mabasi zaidi ya 20. Watu wengine wameshkilia mtazamo wa hujuma dhidi ya Dar express bila kufanya hata kautafiti kadogo tu. Sio siri, kama wewe ni mtumiaji wa mara kwa mara wa mabasi ya Dar Express, utakuwa umegundua kuwa ubora wa huduma ya baadhi ya mabasi hayo imeshuka sana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Mimi ni mteja mzuri tu wa kampuni hii. Huwa ninapanda Dar Express walau mara mbili kila mwezi( Dar- Arusha, Arusha -Dar). Katika safari zangu mbili zilizopita, safari yetu iliishia njiani - kisa ubovu wa gari. Tumetoka Dar, kufika chalinze gari ikaanza kuvuja oil sana. Jamaa wakapambana nayo ikatulia. Tulipofika mombo( Mkumbara?), bodi ikakatika na kulalia tairi za nyuma. Hapo ikawa mwisho wa safari yetu. Sikukata tamaa, nikaunga unga safari hadi Arusha. Niliopomaliza shughuli zangu nikaamua kurudi Dar kwa kutumia tena Dar Express. Njiani pancha mara tatu. Tukafika mahali, gari ikienda spidi zaidi ya 80, inayumba sana. haya mambo hayakuwepo siku za nyuma! Isitoshe, kuna baadhi ya madereva wao ni wakorofi mno. mmoja alikuwa akienda kwa kasi sana. Abiria tukapiga kelele. Akapunguza mwendo, akawa anatembea spidi ya kilomota 40 kwa saa- kutoka Segera hadi chalinze!
Ushauri kwangu kwa mzee Mremi: Ajitahidi kudumisha viwango vya ubora alivyoanza navyo; Awalipe madereva wake vizuri na aweke mfumo mzuri wa kufuatilia maoni kutoka kwa wateja wake.
tatizo linakuja wapi ujue....mimi siwezi kwenda Nyerere road kwa sababu siishi Daresalamu.......wewe fanya hima utuwekee namba yake au aje JF.....asiogope tutampa ushirikiano......
kwani gari kuharibika ni kitu cha ajabu!!hiyo ni sawa na mtu kuwa mgonjwa,je mtu huyo afanyweje?!
Saa za Kichina hizo Mkuu? 11:45 na 18:00 umemaanisha kuwa mlitoka saa tano na dakika 45 asubuhi na mkafika Arusha saa Kumi na Mbili Jioni so Mlitumia masaa Sita na dakika 15 .... Kutoka Dar kwenda Arusha? Duh! Speed hiyo nakumbuka Miaka ya Nyuma Dar Express ilikuwa ikienda na Kurudi Moshi Dar Dar Moshi....haya mabasi nayo yaishakuwa ya hovyo na yamezeeka,nlikuwa mteja wao sana,walinitibua wiki 2 zilizopita,nimepanda basi lao la kwanza,ar-dsm saa 1145 lakini tukafika dar saa 1800,hata kilichonifanya niwahi sikufanikiwa,facken!nimehamia kilimanjaro,atleast