Mabasi ya 'Dar Express' yanahujumiwa?

Mabasi ya 'Dar Express' yanahujumiwa?

Weshashiba hela hao! Ukienda kata ticket hasa ofisi za Arusha , Vibinti walaaa havijali ndo kwanza vinavuta tumidomo twaoo!!! Mie nlipoona hivyo huyoooo nkaondoka kwenda kata Kilimanjaro ya nini shida yakhee? Weshashiba pesa wajiona matawi ya juu kumbe hata mchicha umewazidi kimo ati....
Jirekebisheni.......
Nendeni mkajifunze customer care...... Mabasi yenye nidhamu mengi siku hizi
Ulizeni njia ya Dar Mwanza Mtaambiwa...:wacko:
..Kuna Kadada huwa kapo hapo Ofisi yao ya Arusha mahali wanapotoa mizigo(Parcels), kwanza muda wote Kamenuna, pili Customer Service sifuri, tatu kana Majibu ya kunya, Nne kabaya.....Tano.......
Hivi Watanzania sisi ni watu wa aina gani, Mtu umewekwa mahali utoe huduma, na hio huduma wewe haikugharimu hata senti tano yako, ni sauti yako,mikono na miguu yako ukishirikisha Ubongo wako. Thats All
Kama Uongozi wa Dar Express mnasoma huu Uzi, anzeni na hako Kadada, katoeni hapo...Alaaah
 
Kwakweli nimesoma hizi Taarifa kwamasikitiko makubwa,Nashukuru sana nimeiona hii thread.Mimi si mmiliki ila namfahamu vizuri mmiliki maana kwangu nindugu kabisa nawahakikishia namjulisha sasa hivi!Nantamuomba akinuruhusu nitaweka namba yake hapa ili wana jf mpatapo shida muwasiliane nae mojakwamoja!Kwasasa mnaweza muona anakwa ana pale nyerere road karibu nakiwanda cha Sigara uliza ofisi za Dar ex,anakuwepo karibu kilasiku kuanzia saa kumi namoja jioni.Uliza Mkurugenzi.Kwakweli wafanyakazi au mfanyakazi akisikia unaenda kumshitaki atakuomba msamaha yuko more than makini!
 
Liver pool Hotel (MOMBO) ndiyo pekee inayoongoza kwa UCHAFU, tena mabwana afya sidhani kama huikagua!! Jamani, hawa wamiliki washauriwe.
 
Kwakweli nimesoma hizi Taarifa kwamasikitiko makubwa,Nashukuru sana nimeiona hii thread.Mimi si mmiliki ila namfahamu vizuri mmiliki maana kwangu nindugu kabisa nawahakikishia namjulisha sasa hivi!Nantamuomba akinuruhusu nitaweka namba yake hapa ili wana jf mpatapo shida muwasiliane nae mojakwamoja!Kwasasa mnaweza muona anakwa ana pale nyerere road karibu nakiwanda cha Sigara uliza ofisi za Dar ex,anakuwepo karibu kilasiku kuanzia saa kumi namoja jioni.Uliza Mkurugenzi.Kwakweli wafanyakazi au mfanyakazi akisikia unaenda kumshitaki atakuomba msamaha yuko more than makini!

tafadhali fanya hivyo.....tena ikiwezekana aje hapa asome comment za watu.....na ikibidi ajisajili ili tumuulize maswali ya papo kwa hapo.....ni biashara ile bana......
 
Nimeipenda sana Metro!, naona wako makini sana wale watu! pamoja na kwamba wasiwasi wangu ni kumuachia dereva mmoja aendeshe gari all the way bila kupumzika, inatisha sana.
 
haaa, nipeni contacts za huyu jamaa nimjulishe aje asome hizi comments za wateja wake, naona anaelekea kuwa scandnavia......hivi huyu jamaa alishaacha mchezo wake wa kusimama msituni na kusimamisha bus zake ghafla na kucheki customer care ipoje? akikuta customer care haipo standard humwambia dereva ampe funguo na bus attendants avue uniform na team mpya kuingia hapohapo! au amezeeka?
 
tafadhali fanya hivyo.....tena ikiwezekana aje hapa asome comment za watu.....na ikibidi ajisajili ili tumuulize maswali ya papo kwa hapo.....ni biashara ile bana......

Preta nalishugulikia hili,Ila nimeongea namkurugenzi amesikitika sana kwamatatizo ambayo wateja wake wanayapata ktk huduma yake bila yeye kujua!Anaomba mnapopata shida mumjulishe mara moja ili aweze kuchukua hatua!Mtapata namba yk soon.Kwasasa fuata maelekezo niliyatoa hapo juu namana yakumpata.
 
Ki ukweli ni kwamba huduma za mabasi ya Dar Express ni za hali ya juu sana, hicho ndicho kitu ambacho naamini wanaotumia mabasi hayo kitaendelea kuwavutia. Mimi huwa natumia Dar express siku zote nikikosa basi kilimanjaro nikikosa hayo mawili basi nahairisha safari kabisa labla iwe ni lazima sana. Wacha walete mabasi yao watapanda wao na familia zao, sisi tunachofuata kule ni huduma nzuri na pia tumeshazowea. Hawa jamaa kila kitu wanataka washike wao, sio sahihi kabisa
 
wewe kama ni mfuatiliaji habari kwenye vyombo vya habari kama mitandao,tv,radio na vyanzo vingine vya habari kuna mpango unasukwa wa kuleta magari ya kusafirisha abiria ya mafisadi flani,sasa ushindani mkubwa wa kibiashara kwa usafiri wa arusha to dar huyu jamaa wa dar express huduma zake zimevutia watu wengi wanaofanya safari kwenye njia hiyo.lini umesikia hayo magari yamesababisha ajali kubwa kama hyo mengine ambayo kilakukicha huachikusikia yamesababisha ajali,japo kua hakuna anaeweza kutabiri ajali au kupenda litokee,au kutokupata ajali ni ujanja,simaanishi hivyo ila tahadhari inatakiwa ichukuliwe mapema,kivipi.....mfano kuwa na magari yenye standard inayokubalika kimataifa,angalia mabasi ya dar express sio ya kuunga unga kama hayo mengi yaliopo barabarani,angalia madereva wake kuanzia mavazi mpaka muonekano wa mtu,wewe kama ni mlevi na mla mirungi na ulevi wowote pale kazi hupati ndugu yangu,angalia madereva wa magari mengine unawakuta wapo rufly na uhuni usio na mpango barabarani.ustaarabu kwa ujumla pale dar express ni standard yaani unaokidhi haja.

Kwa hiyo unaogopa ushindani?Wacha walete ndo tuone yupi ana huduma nzuri,halafu haka katabia ka ubaguzi na hicho chama chenu,akifanya mwingine fisadi mkifanya nyinyi sawa,haya tutaona mwisho wenu.
 
Preta nalishugulikia hili,Ila nimeongea namkurugenzi amesikitika sana kwamatatizo ambayo wateja wake wanayapata ktk huduma yake bila yeye kujua!Anaomba mnapopata shida mumjulishe mara moja ili aweze kuchukua hatua!Mtapata namba yk soon.Kwasasa fuata maelekezo niliyatoa hapo juu namana yakumpata.

tatizo linakuja wapi ujue....mimi siwezi kwenda Nyerere road kwa sababu siishi Daresalamu.......wewe fanya hima utuwekee namba yake au aje JF.....asiogope tutampa ushirikiano......
 
Mkuu, Mabasi yaliyofungiwa ni 14 tu. Dar Express wana mabasi zaidi ya 20. Watu wengine wameshkilia mtazamo wa hujuma dhidi ya Dar express bila kufanya hata kautafiti kadogo tu. Sio siri, kama wewe ni mtumiaji wa mara kwa mara wa mabasi ya Dar Express, utakuwa umegundua kuwa ubora wa huduma ya baadhi ya mabasi hayo imeshuka sana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Mimi ni mteja mzuri tu wa kampuni hii. Huwa ninapanda Dar Express walau mara mbili kila mwezi( Dar- Arusha, Arusha -Dar). Katika safari zangu mbili zilizopita, safari yetu iliishia njiani - kisa ubovu wa gari. Tumetoka Dar, kufika chalinze gari ikaanza kuvuja oil sana. Jamaa wakapambana nayo ikatulia. Tulipofika mombo( Mkumbara?), bodi ikakatika na kulalia tairi za nyuma. Hapo ikawa mwisho wa safari yetu. Sikukata tamaa, nikaunga unga safari hadi Arusha. Niliopomaliza shughuli zangu nikaamua kurudi Dar kwa kutumia tena Dar Express. Njiani pancha mara tatu. Tukafika mahali, gari ikienda spidi zaidi ya 80, inayumba sana. haya mambo hayakuwepo siku za nyuma! Isitoshe, kuna baadhi ya madereva wao ni wakorofi mno. mmoja alikuwa akienda kwa kasi sana. Abiria tukapiga kelele. Akapunguza mwendo, akawa anatembea spidi ya kilomota 40 kwa saa- kutoka Segera hadi chalinze!

Ushauri kwangu kwa mzee Mremi: Ajitahidi kudumisha viwango vya ubora alivyoanza navyo; Awalipe madereva wake vizuri na aweke mfumo mzuri wa kufuatilia maoni kutoka kwa wateja wake.

Mkuu upo sahihi sana, hawa wamiliki wa mabasi walifikiri wataendelea kukamata hilo soko kwa muda wote, sasa ushindani umeanza kuwa mkubwa na walishindwa kujipanga sasa wanataka kudai kwamba wanahujumiwa. Huduma za Dar express zimeshuka sana, nilishawahi kupanda basi linalokwenda Nairobi, kioo kilikuwa na crack na walikuwa wanakwenda huku wakiweka vipande vya miti kwani muda wowote ilikuwa kinaanguka. Binafsi nilifanya jitihada za kuwasiliana na makampuni machache ya mabasi kwa lengo la kuwapa mawazo yangu juu ya kuboresha huduma wakimwemo dar express, lakini ilionekena wanaamini safi huo uzoefu walionao na bila kuongeza taaluma nyinginezo, na hizi dalili za wao kupotea kwenye biashara hii ilishaonekana. Bali kama watachukua hatua kwa kuruhusu taaluma kuchukua nafasi yake katika biashara ya usafirishaji, basi wanaweza kusalimika; vinginevyo watatokomea. Moja kati ya makampuni niliyoyatembelea na kuwapa proposal ya mpango wa uendeshaji wa huduma ya usafirishaji, walipokea proposal yangu na tulikuwa na muda wa kujadili vya kutosha juu ya huduma hii na walikuwa katka harakati za kuingiza magari mengi na inaonekana walijiandaa na walisoma madhaifu ya kina dar express.
 
tatizo linakuja wapi ujue....mimi siwezi kwenda Nyerere road kwa sababu siishi Daresalamu.......wewe fanya hima utuwekee namba yake au aje JF.....asiogope tutampa ushirikiano......

Namba ya Mkurugenzi (MREMI) - 0784 276060
 
Jumamosi ya Tarehe 14 mwezi huu as Saba nlikua natoka Dar kwenda Arusha kwa usafiri wa Gari hili, kwakua nlikua nina haraka nlikata Gari ya Mapema ili niwahi kufika.
Safari ilikua nzuri but kufika Mwanga Gari Clutch zikakataa. Tulikaa Mwanga karibu masaa manne bila msaada wowote mpaka saa moja usiku.

Hakuna cha Dereva wala mhudumu aliekua tayari kutusikiliza. Wengine walidandia magari mengine kwa gharama zao wakaishia.

Kimbembe kwenye Reacue Bus, Konda wake sijui mgeni? ana kauli chafu, abiria Kama watatu hivi walivushwa vituo.

Kurudi nikakamatia Kilimanjaro,
Swaaaaafi!!!!!
 
kwani gari kuharibika ni kitu cha ajabu!!hiyo ni sawa na mtu kuwa mgonjwa,je mtu huyo afanyweje?!

...Are You really a Great Thinker??? Mtu kuwa Mgonjwa ana suffer peke yake na ikifikia hata hatua ya KUFA anakufa peke yake na anaenda kufukiwa Peke yake.
Gari likiwa na ubovu wa break kwa mfano, linaweza kumwaga abiria pale mto Wami na kusababisha vifo vya abiria kadhaa!
Is this too hard to think? Unaidhalilisha JF Comrade, Dah!
 
haya mabasi nayo yaishakuwa ya hovyo na yamezeeka,nlikuwa mteja wao sana,walinitibua wiki 2 zilizopita,nimepanda basi lao la kwanza,ar-dsm saa 1145 lakini tukafika dar saa 1800,hata kilichonifanya niwahi sikufanikiwa,facken!nimehamia kilimanjaro,atleast
Saa za Kichina hizo Mkuu? 11:45 na 18:00 umemaanisha kuwa mlitoka saa tano na dakika 45 asubuhi na mkafika Arusha saa Kumi na Mbili Jioni so Mlitumia masaa Sita na dakika 15 .... Kutoka Dar kwenda Arusha? Duh! Speed hiyo nakumbuka Miaka ya Nyuma Dar Express ilikuwa ikienda na Kurudi Moshi Dar Dar Moshi....
 
Back
Top Bottom