Fred Mwakitundu
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 227
- 382
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro imemweka kiti moto mmiliki wa mabasi ya Ester Luxury Coach baaada ya mabasi yake kudaiwa kukubuhu katika biashara ya usafrishaji madawa ya kulevya aina ya milungi.
Mmiliki huyo alifika mbele ya kamati hiyo hivi karibuni iliyoketi chini ya mwenyekiti wake na ambaye ni mkuu wa mkoa wa kilimanjaro,Nurdin Hassan Babu kikao kilichofanyika jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa kilimanjaro.
Habari za uhakika zilizodhibitishwa na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo aliyeomba kutotajwa jina lake,zimetonya kuwa kuitwa na kuhojiwa kwa mmiliki huyo wa mabasi kumetokana na kuwepo kwa matukio ya mara kwa ya mabasi hayo kusafrisha madawa hayo ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi yanaangukia kwenye madawa ya kulevya na anyepatikana na hatia adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.
Hata hivyo mmiliki wa mabasi hayo (jina kapuni)licha ya kukiri kuitwa mbele ya kamati hiyo pamoja na mabasi yake kudaiwa kusafrisha madawa hayo,aliahidi kukutana na wanahabari kutolea ufafanuzi sakata hilo lakini akaingia mitini,
Taarifa zinatonya kuwa baada ya kuwekwa kiti moto alionywa kuacha mara moja biashara hiyo vinginevyo sheria itachukua mkondo wake ikiwamo kumfutia leseni ya usafrishaji abiria pamoja na kumfikisha mahakamani.
Hata hivyo baadhi ya watu wamehoji ni kwa nini vyombo vya uchunguzi visichukue hatua ya kuwakamata watumishi wa mabasi hayo na kuwafikisha makahamani pindi wanapokamatwa na mzigo badala ya kumbembeleza mwenye mali na kumuonya wakati huku mtaani polisi wamekuwa wakifukuzana na wauza milungi kila uchao.
Kazi kwenu vyombo vya uchunguzi,acheni ubaguzi kwenye matukio ya kijinai,sheria ing'ate kwa wakubwa na wadogo