Mabasi ya HYUNDAI yanamuonekano mzuri sana. Vipi kuhusu ubora wake?

Mabasi ya HYUNDAI yanamuonekano mzuri sana. Vipi kuhusu ubora wake?

Ndugu zangu kuna mabasi ya vilabu wanayopanda wachezaji mfno Arsenal, man u,n.k,je Yale kampuni gani ni mapana marefu na mazuri sana
Sasa yale ndiyo Hyundai, kampuni ya Korea. Ni Royal Coach, yaani hadhi ya kifalme kabisa. Team za Real Madrid, FC Barcelona, Man U na National Team nyingi hutumia mabasi hayo. Yako poa sana.

Ama kuhusu mada, mabasi ya Higer ni mazuri sana tena sana kuliko Yutong.
Kwa walio wahi kusafiri kwenda Mtwara kwa mfano, Machinga Bus zake zote ni Higer. Ubora sina uhakika ila speed yake wenyewe wanadai inapepea zaidi ya Yutong Buses.

Pia nimeshawahi kupanda Golden Dragon, nazo ziko vizuri ndani kwani ukiwa na smartphone, huna shida ya kuchaji ukiwa safarini. Ninewahi kupanda gari hizo wakati naenda Lindi kikazi,mabasi ya kampuni moja Millenium Coach.

Scania kwa kweli za bodi ya Marcopolo hazishikiki, ni more than 1bn/-,hiyo hela ni ndefu sana!
 
Hizo basi sio Hyundai balo ni za kichina kampuni inaitwa HIGER sema zinakua kama na logo zinataka kufanana
 
Kuna Yutong, Zhongtong, Higer,na Golden Dragon hawa wote.. Ndio walewale tu..wanazipenda sababu ni nafuu tofauti na Scania hasa Marcopolo body ni ghali sana.. Ni wachache wenye uwezo wa kumudu gharama..
Marcopolo moja unanunua hizo Chinese buses 3
 
COARTEM Hayo mabasi siyo ya Hyundai ni ya kampuni flani ya wachina inaitwa Higer. Sijui kuhusu ubora wake ila nimeyapanda ni very comfortable na kuna sehemu ya kuchaji simu hadi raha!
 
Ndugu zangu kuna mabasi ya vilabu wanayopanda wachezaji mfno Arsenal, man u,n.k,je Yale kampuni gani ni mapana marefu na mazuri sana
Sasa yale ndiyo Hyundai, kampuni ya Korea. Ni Royal Coach, yaani hadhi ya kifalme kabisa. Team za Real Madrid, FC Barcelona, Man U na National Team nyingi hutumia mabasi hayo. Yako poa sana.

Ama kuhusu mada, mabasi ya Higer ni mazuri sana tena sana kuliko Yutong.
Kwa walio wahi kusafiri kwenda Mtwara kwa mfano, Machinga Bus zake zote ni Higer. Ubora sina uhakika ila speed yake wenyewe wanadai inapepea zaidi ya Yutong Buses.

Pia nimeshawahi kupanda Golden Dragon, nazo ziko vizuri ndani kwani ukiwa na smartphone, huna shida ya kuchaji ukiwa safarini. Nimewahi kupanda gari hizo wakati naenda Lindi kikazi,mabasi ya kampuni moja Millenium Coach.

Scania kwa kweli za bodi ya Marcopolo hazishikiki, ni more than 1bn/-,hiyo hela ni ndefu sana!
 
Dar Lux anayo mabasi aina hii miaka 2-3 iliyopita na nimepanda toka mwanza hadi Dar ni very comfortable na imara tena linatulia sana barabarani hata linapokuwa na speed kubwa.
 
Lakini scania bado ndio gari bora zaidi kuliko yote hadi sasa ila wafanyabiashara wengi wanashindwa kumudu gharama ya Kununua na services. Scania tangu iingie Tanzania miaka ya 70 hadi sasa liko kwenye ubora wake.Scania ukipata services kisawa sawa hudumu 25-30 years.
 
Wisewriter upo sahihi kuhusu uimara wa engine za Scania nakumbuka 113 sikumbuki ni toleo la mwaka ganiila still lipo bara barani...ila Scania sio engine bora kuriko zote kuna Mercedes benz na Man pia...izo zinadumu
 
Hizo basi ni luxury sana... Na wadosi wengi wanazikimbilia cuz ni bei nafuu na linapokuja swala la fuel consumption zinanusa tu tofauti na mabasi aina nyingine kama Scania, Volvo, Benz, Isuzu, UD na Fuso.
Pia makampuni mengi yamehamia huko wateja wengi wanayapenda haya mabasi hivyo wakajikuta wanakimbizwa sokoni. Mfano Tajiri mwenye bus za Upendo alikua conservative kampuni yake ikapoteza mvuto kwa wasafiri ikabidi alete Higer kuendana na ushindani... Yutong na higer ndo habari ya mjini kwa sasa. Ni makampuni machache wenye basi za kigansta wanaendelea kufanya biashara vizuri mfano champion (wazee wa idodomia wanamiliki Scania), Taqwa UD (Nissan Diesel), Shambalai, Kisbo na city boy.
Basi za kigangster mkuu?
 
Higer anatengeneza body kama unataka anakutengenezea body engine scania
 
Back
Top Bottom