Mabasi ya Vikunai - Stesheni na Temeke - Vikunai kukatisha safari

EMMANUELEY

Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
8
Reaction score
0
Mimi / sisi m /wakaazi wa eneo la VIKUNAI, MANISPAA YA TEMEKE, jirani na mradi wa NSSF KIJICHI, kwa mujibu wa taratibu za usafiri na usafirishaji, tunazo gari za RUTI tofauti kuna za TEMEKE - VIKUNAI kupitia KIJICHI na zingine ni za VIKUNAI - STESHENI kupitia Mbagala Zakhiem.

Naanza na hizi za TEMEKE VIKUNAI KUPITIA KIJICHI

Gari hizi ziko zaidi ya KUMI lakini HAKUNA ZINAZOFIKA VIKUNAI wakati wote wa siku, safari zao huwa zinaishia MBAGALA KUU, na kama siku hiyo wamejisikia hufika mpaka MGENI NANI. Na mara kadhaa tumekuwa tukitoa ripoti kwa wasimamizi wa usalama barabarani lakini hakuna mabadiriko. OMBI LETU GARI HIZI ZIFIKE VIKUNAI KAMA LESENI ZAO ZINAVYOWATAKA kwani kinyume cha hapo ni ukuikaji wa masharti ya leseni zao.

PILI, NI MAGARI YA VIKUNAI STESHENI KUPITIA ZAKHIEM

Gari hizi zikitoka Stesheni zikifika Zakhiem huwa zinaishia hapo na kupakia upya kuelekea Mgeni Nani, ambapo mara zote ndipo huwa mwisho wa safari zao, huwa hazifiki VIKUNAI isipokuwa kuna gari MOJA HUWA INAKUJA ASUBUHI SANA NA KUANZIA SAFARI VIKUNAI KILA SIKU, lakini nayo saa za mchana ama jioni haifiki Vikunai huishia Zakhiem, na kukaa FUNGU hapo.

Kwa utaratibu huu kwanza wanatusababishia kutumia gharama kubwa kila siku, lakini kutupa wakati mgumu kufika majumbani wakati serikali imeshaandaa mazingira safi na ya gharama nafuu, hivyo kutulazimu pale Zakhiem kupanda VI HIACE ambavyo havijasajiliwa kupita njia ya VIKUNAI KWA GHARAMA zaidi ya sh 500/ wakati toka STESHENI MPAKA VIKUNAI NI SH 450/

Kwa ujumbe huu naomba tusaidiwe kwa kadri inavyowezekana, na ni vyema vile vi-hiace vikazuiliwa kuja huku kwani vinaingilia ruti ambayo sio yao na kutunyima fursa. Swala hili kwa kina linafahamika na wahusika wa pande ama sekta zinazohusika, kama USALAMA BARABARANI, SUMATRA, SERIKALI YA MTAA nk lakini linaonekana kuwa zito kutekelezeka, kupitia uiwanja huu ambao unatembelewa na na viongozi ili kupata msaada, maana wanafunzi na wafanyakazi wakazi wa eneo la Vikunai tunapata tabu sana.

Ahsante kwa ushirikiano wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…