Tahadhari Ogopeni matapeli wanaojiita mawakala, wengi wao siyo waaminifu, wanachanganya bati za kampuni tofauti tofauti halafu wanakuizia bei kubwa km bati za ALAF.
Kwa uzoefu wangu km nyumba yako ni kubwa na unahitaji bati nyingi bora uende kiwandani mwenyewe.
Siri ni moja tu waliyoniambia ALAF kipindi nanunua kiwandani kwao, walisema bati lao original lina mhuri wa moto, na kweli bati zote nilizobeba pale zilikuwa na mhuri wa moto, Toka 2020 Dec hadi Leo watu wanapita wanashangaa hayapauki, utafikiri nimeweka jana. Ila kwa bei ndo habari nyingine, ukizingtia nilichukua yale ya muundo wa vigae, na ubebaji wake nilitumia semi maana kulikuwa na marefu hadi mita 12 na point. Ila namshukuru sana Mungu mambo siyo mabaya