"Mabeberu" Marekani waanza mbinyo kwa Tanzania. Washawishi Serikali yao na Jumuiya ya Kimataifa kuanza vikwazo na kukata misaada

To my understanding ni kwamba hali hii lazima itokee kwa sababu nyingi sana.
1. makampuni ya uwekezaji kutoka Marekani wamekuwa ni sehemu ya sera ya nje ya Marekani hasa kubinya nchi zenye uchumi mdogo na kufanya vogue investments zinazoheshimu sera za Marekani huku zikipuuza ustawi na sera za mataifa maskini ambao wameweka uwekezaji huo

2. Siku zote bwana mkubwa Marekani anapambana kuzuia ushindani aina yeyote kutoka mataifa yanayopiga hatua za kimaendeleo. Wameshaweka margin ya kila uwezo mkubwa wa kiuchumi utokane na NATO nations. Ndo maana hata mchina anakumbana na embargo kubwa ya kiuchumi kutoka US kwa kuwa hayumo kwenye NATO ring.

3. Masharti ya kuheshimu haki za binadamu hasa mkazo ukiwekwa kwenye same sex relationship ndiyo sera kuu ya kunyima misaada. Kwa nini hili wanalisisitiza, ni kwa sababu nyuma yake ni kumaliza ama kufreeze tamaduni za mataifa madogo waweze kuingia kwenye ulimwengu wao ambao mipaka na miiko ya tamaduni vimeshakufa

4. Lengo lingine ni kupata eneo la kuuzia silaha zao na kukwapua maliasili za nchi ili kuimarisha federal reserve yao. (Hili ni eneo pana sana)
 
Umeandika zaidi nadharia na unproved theories.

Mataifa ya Afrika yanashindwa kuujenga uchumi wa mataifa yao kutokana na uongozi mbaya. Badala ya kuliona hilo na kulifanyia kazi wamebakia kuwalaumu wazungu.

Umeongelea China, nadhani kuna mambo mengi kuhusu China ambayo huyajui. Hivi unajua kuwa makampuni makubwa yaliyowekeza China, siyo ya China bali ni ya America na Ulaya? Sera ya ujamaa ya China iliifanya China kuishi kwenye umaskini mkubwa kwa miaka mingi, na miaka hiyo uchumi wa China ulikuwa unakua kwa chini ya 3%. Walipofanya mageuzi nakuruhusu makampuni ya nje kuwekeza China, uchumi wa China ulibadilika ghafla, na ukuaji wake kuna wakati ulifikia 12% kwa mwaka. China inajua faida kubwa ya uwekezaji wa makampuni ya Ulaya na America nchini China, ndiyo maana Waziri wao Mkuu mara nyingi anaenda Ulaya kutafuta wawekezaji.

FDI kutoka Ulaya, America, Australia na Hong Kong kwenda China kwa mwaka inafikia dola bilioni 80. China tunayoishabikia inatambua umuhimu wa mitaji ya nje katika kuhuisha uchumi wake, mataifa maskini ya Afrika yanaona uwekezaji wa nje kwenye mataifa yao hauna faida bali ni unyonyaji tu!

Afrika imejaa wasomi wa makaratasi lakini wasio na kitu kichwani cha kuyasaidia mataifa yao. Dubai ilikuwa hoi kuliko Afrika lakini ndani ya miaka 15 ilibadilika ghafla. Hiyo ilitokea baada ya kupata viongozi wenye elimu ya kweli, akili na maono.

Adui wa kwanza wa maendeleo ya uchumi ni kodi zisuzolipika. Hakuna nchi hata moja iliyokuwa maskini halafu ilibafilika na kuwa na maendeleo makubwa kwa kuongeza ukubwa wa kodi au uwingi wa kodi.

Kiongpzi mwenye uelewa mdogo anafikiria kuongeza mapato ya serikali kwa kuongeza kodi. Lakini kiongozi mwerevu huongeza mapato ya Serikali kwa kupunguza kodi na kuongeza uwekezaji.

Kuhusu masoko ya silaha, nadhani siyo sahihi kuwalaumu watengenezaji wa silaha. Kama waafrika wanamalizia pesa zao kununulia silaha badala ya kuwapelekea wananchi wao maji, basi hilo ni tatizo linalosababishwa na upu.mbavu wa Mwafrika. Hakuna anayelazimishwa kununua silaha.

Kama baba unamalizia hela yote kwenye kimpumu au mbege wakati wanao wanalala njaa, hawaendi shule - wa kulaumiwa ni huyo baba na siyo mama mpika mbege au kimpumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimepata bahati ya kuishi huko na nimezungumza na RAIA wengi wa huko
Hali Halisi ni wale jamaa wanaishi maisha kama ya watoto We matajiri wakubwa wa tanzania yetu
Kama kuna wakosoaji wapo wapo tu
Amini nakwambia jamaa wamamaisha mazuri sana
Ndio maana nakwambia wewe unaangalia upande mmoja tu.
 
Ni mtanzania punguani pekee anayeweza kusherehekea nchi yake ikibagazwa. Hata mfanye nini chama cha Mbowe kishajifia tu.
 
Vilevile ujue hakuna sheria/jamii inayomlazimisha mtu kwenda kwa msiba au sherehe ya jirani lakn ikitokea tunalazimika kwenda hata kama tunanungunika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…