"Mabeberu" Marekani waanza mbinyo kwa Tanzania. Washawishi Serikali yao na Jumuiya ya Kimataifa kuanza vikwazo na kukata misaada

Tutatumia bidhaa kutoka China siio lazima marekani
Na kweli China imekuwa kimbilio la wengi ambao wanasema hawataki kuingiliwa mambo ya ndani hadi pale wanapokuta wachina hawacheki na kima kwenye maslahi yao. Sijui na sisi tutawabinafsishia bandari au kiwanja cha ndege wakitushika pabaya tukiwekwa kando na dunia nzima maana hamna raha ya kudeal na mtu dhaifu kama yule asiye na option
 
Si ndio watafika huko mkuu? wanaenda kwa hatua.
 
NI wakati wa Africa kuondoa mawazo mgando ya kusaidiw kila siku
Dunia ya Sasa sio ile ya wakati wa nyerere
Ndio maana tunaletewa misaada inayodhuru hata afya zetu
Beberu hawez kumpenda Mtu mweusi hata siku moja
Tutaenda sawa tu na mchina kwani mchina nqe anatuhitaji Sana tu
Kupata masoko ya bidhaa zake
 
Ni kweli kabisa ndiyo maana wanafikiria vikwazo zaidi vitakavyotoa mbinyo na pia kuhusu ushirikiano wa kibiashara.
Hapa lazima maumivu yawe makali kiasi kwamba kila raia aliyepo nchini atasikia kisu kimegusa mfupa..
 

Kwa hiyo unafurahia kuwa dampo la bidhaa duni yaani unaruka majivu unakanyaga moto.

Maskini hivi unajua kinachoendelea na SGR ya Kenya, Hivi unajua gate way ya mchina kwa Afrika ya mashariki inaenda kuwa Kenya na juzi tu washakula deal la kupeleka maparachichi . haya Sisi tunapeleka nini au ndo tunasubiria bidhaa zao huku

Hivi una hata Idea ya international trade na jinsi inavyofanya kazi. unajua hata kiwango chetu kati hiyo biashara na china yupo katika position ipi. Hivi hizo hela za kununua vitu China unajua mtapata vipi au unajua mzunguko wetu wa pesa utaathirika vipi[/QUOTE]
 
Tunarudi kuleee kwa miezi 18 ya kufunga mikanda ambayo ilitokea kuwa miaka 18. Chai ya maziwa na mayai itakua anasa.
 
Ni kweli kabisa ndiyo maana wanafikiria vikwazo zaidi vitakavyotoa mbinyo na pia kuhusu ushirikiano wa kibiashara.
Hapa lazima maumivu yawe makali kiasi kwamba kila raia aliyepo nchini atasikia kisu kimegusa mfupa..

Tuombe Tu yasifikie huko ila yakifika huko hata yule omba omba wa barabarani ataskia maumivu yake.

self sufficciency economy, what a stupid myth yaani mmarekani kubana Huawei ya China na yeye akabanwa vizuri hadi akasurrender itakuwa uchumi wetu huu ambao hata 100$ billion haujafika na bajeti inayotegemea zaidi ya 40% kutoka kwa wahisani..

Bora niishie jukwaa la celebrity nikaone vituko fake vya mastar kuliko hivi vituko na stress za " great thinkers"
 
Scandinavia ni waylaid misaada wakubwa pia. Wakiacha kucha his bakuli tutayasikia maumivu.
 
Jiulize wewe wale waliotuletea majeshi ya Burundi hapa Pemba kutuua hadharani wapo upande gani?
Msifikiri mauaji na uonevu kwa masikini wa mungu wasio na silaha ni wema kwenu bali ni shari kwenu
Gaddafi alikua mbabe kuliko Magufuli mwisho wake anglia hapo chini
 
Very poor argument and analysis. Umefika Zimbabwe au unasimliwa tu? Ni migodi gani ya maana Zimbabwe inayomilikiwa na Wachina.

Wachina katika Ulimwengu wa uchimbaji madini ni zero. Na hiyo ndiyo sababu ya Wachina nchini kwao kuyakaribisha makampuni ya US, Canada na Australia kuchimba dhahabu.

Wachina hawana teknolojia ya kuchimba madini. Wanaiga kutengeneza vifaa vya kuchimbia na kuchenjulia madini LAKINI wameshindwa kuiga teknolojia ya uchimbaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao Marekani wenyewe Trump analalamika kaibiwa kura, mbona hawasemi?
 
Angalia wanalochukia

View attachment 1626020

Wanachukia Tanzania kuanza kujijenga upya kitaifa, wanataka tuendelee kuwa shamba la bibi. Halafu kuna watanzania wanashangilia; watu wa hovyo sana hawa.
Wewe ndiyo mbumbumbu kabisa! Umeelewa maana ya hiyo sentensi. Hivi wewe unafurahia utaifishaji wa maendeleo ya watu?

Kama hujui, sentensi hiyo ina maana Magufuli na CCM wanatupeleka kwenye Tanzania ya Mwalimu ya mwaka 1967 ya kutaifisha mali/maendeleo ya watu na kuyaweka chini umma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili nalo litapika kama mengine na kila mtu atalisahau kila nchi ina maslahi kwa nchi nyingine na vikwazo vinafanya kazi pande zote nao watakosa kile walichokuwa wanakipata kutoka kwetu.
 
X Ray mtatumia tv asilia POA
MRA mtatumia Nini?
CT Scan je?
ECG mtafanyia Nini?
Msijifananishe na wachina wakati nyie hamna hata kiwanda Cha tooth pick
Iran, North Korea, Syria, Zimbabwe, Venezuela, Cuba, Myanmar hawana hivyo vifaa?
Tutanunua vya Russia na China.

Maisha yatakuwa magumu kwa wote lakini siyo raisi na hao wanaopingana nae. Raisi huyu hata akiondoka bado athari za vikwazo vitaitafuna nchi miaka mingi baadaye, mfano Zimbabwe Morgan Tshovingirai na Bob Mugabe wameshakufa lakini vikwazo bado vinaitafuna nchi yao.

Hao akina Lissu wataenda kuishi nje, watapewa ufadhili wa pesa na vitu muhimu, watoto wao watasomeshwa nje huku tutabaki sisi fuata upepo na ndugu zetu maskini huko vijijini.
 
Mimi naamini aliyeiba kura, anayefunga watu ovyo, anayeua, anayeteka, anayebambikia kesi watu za uhujumu uchumi, ni dhahiri huyo ni wakala wa shetani.

Tuipende nchi kwa kukataa kwa nguvu zetu zote, udikteta. Tuungane kutetea demokrasia, haki na uhuru wa watu wa kutoa maoni, kuchagua na kuchaguliwa. Udikteta hauna nafasi duniani, usiwe na nafasi Tanzania. Watu kama mahela au mambombosasa kuwepo kwao Tanzania ni laana kwa Taifa letu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwana Kulifaindi mwana kuligeti muache tu aendeleze ubabe MABEBERU wamsagie Kunguni.
 
Hakuna kurudi nyuma wakati 5 years hata buku hamjamwongezea mtumishi wa serikali afu mnajitutumua hapa hahaha

Hivi sgr yenyewe imefika KIGOMA?

Sent from my TECNO CF8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…