"Mabeberu" Marekani waanza mbinyo kwa Tanzania. Washawishi Serikali yao na Jumuiya ya Kimataifa kuanza vikwazo na kukata misaada

"Mabeberu" Marekani waanza mbinyo kwa Tanzania. Washawishi Serikali yao na Jumuiya ya Kimataifa kuanza vikwazo na kukata misaada

Dona kantre huna hata kiwanda Cha kutengeneza pini.
Kifuatacho ni kupunguza kazi madaktari, manesi na watu wa maabara na kuajiri waganga was kienyeji, wachawi, wabashiri na wapiga ramli.
View attachment 1626014
Sasa itakuwaje?
Lakini maisha yetu ni zaidi ya corona

Tutazoea tu kula pumba kama mwaka 1978 na yatapita

Mmmmmmmh sasa itakuwaje?

Hii inawahusu ccm tu?au na chadema

Ohoooooooo

Making loud noiseeeeee
 
X Ray mtatumia tv asilia POA
MRA mtatumia Nini?
CT Scan je?
ECG mtafanyia Nini?
Msijifananishe na wachina wakati nyie hamna hata kiwanda Cha tooth pick
Hivyo vidubwasha mbona vinapatika nchi nyingi tu duniani?

Btw, gesi ya kuendesha CT Scan na vinginevyo duniani si inaanza kuchimbwa TZ. Au na sisi tubanie?
 
Tena hizi ni rasharasha tu
Kwa hiyo tutaanza kuvaa tena chachacha au katambuga

Na hii inawahusu akina nani maana wengine hawana vyama vya siasa

Lekkker lekker

Mmmmmh siasa zimeisha na kampeni zimeisha

Sasa hawa wamerekani lengo lao ni kuona maisha yetu yanakuwa ya hovyo hovyo tu na vichaa kuongezeka

Hakika vichaa wataongezeka Tanzania kwa style kama hizi plus mbinyo

Lakini ccm kama chama tutashinda kwa kishindo mbinyo huu
 
Asiesikia la mkuu huvunjika guu, wasiojielewa watakuja hapa waanze kusema hawajali sisi ni matajiri, sasa kama tungekuwa matajiri hiyo misaada tusingekuwa tunapewa, wacheni kujidanganya.

Hapa mwananchi wa kawaida ndie atakaeumia, hivyo vikwazo vya kuinyima nchi misaada vitasababisha kodi za bidhaa zipande ili wajaribu kufidia hilo gap la kupoteza misaada, na mpaka hapa "serikali ya wanyonge" itakuwa imeshafeli.

Bahati nzuri hapa tutaumia wote, wezi wa kura na walioibiwa kura, sasa wale "praise team" nao wajiandae mapema kisaikolojia, kama ameanza mmarekani.

Kuna uwezekano mkubwa na marafiki zake wa jumuia ya ulaya nao watafuata, wacha kina Ndugai waendelee kushangilia wasilolijua kule bungeni, kwa haya yajayo watapata akili tu.

Huko tunapoelekea watatuzuia hata kufanya nao biashara, sijui hizo dola za kuwekea akiba ya fedha za kigeni zitatoka wapi.

Naona kila dalili tunaenda kuwa kama marafiki zetu wapendwa wa Zimbabwe.
Usihofu Mkuu,Mwaka 1978 na 1979 watu walikula pumba

Sasa wewe mtoto mayai mayai ndio shida inaanza hapa kwanza wewe ni chadema hivyo huu mbinyo utawafanya ccm kula bata zaidi maana tumezoea kupambana

Hata wakisema tusiende chooni mwaka mzima watu hawaogopi

Hata wakisema wanataka uhuru wa mashoga kila kona ya nchi bado watu watawakimbia tu

Beberu anataka tuanza kuwa na maisha ya hovyo hovyo
 
Wengi wanaochangia hapa hawajui global politics! Wanachangia kushabikia Tanzania kuwekewa vikwazo bila kuwa wanaangalia kuwa Tanzania Taifa ambalo global powers wanataka wawe na influence nalo sana; na sasa hivi wanamchukia Magufuli kwa sababu hnaonekana hawawezi kuwa na influence juu yake.

Mark my word kama kweli marekani itaiwekea vikwazo Tanzania ili uje tuzungumze tena. Hawawezi kurudia makosa waliyofanya Zimbabwe na kuwaacha wachina wakajizolea madini yote yale kwa bwelele ambayo wanatengezea vitu vya bei nafuu sana kwa sababu ya cheap raw materials na kuvitumia kuvuruga soko la ndani ya marekani.
 
Haha hahah hahah bila gesi yetu dunia haiathiriki na kitu
Hii sio ile ya Mtwara, hii ni Rukwa na kuna uhaba mkubwa sana duniani. Tanzania ndio mkombozi kwa sasa. Mahospitali yote yanategemea hii gas.


 
Trend ya vyama tawala kutumia nguvu ya dola kubaki madarakani mwisho wa siku mhanga mkuu huwa ni mwananchi wa kawaida. Very soon tutakua kama Zimbabwe na Venezuela kwa kisingizio cha usosholisti feki.
 
Hii sio ile ya Mtwara, hii ni Rukwa na kuna uhaba mkubwa sana duniani. Tanzania ndio mkombozi kwa sasa. Mahospitali yote yanategemea hii gas.


Angalia wanalochukia

1605319434814.png


Wanachukia Tanzania kuanza kujijenga upya kitaifa, wanataka tuendelee kuwa shamba la bibi. Halafu kuna watanzania wanashangilia; watu wa hovyo sana hawa.
 
“Dua la kuku”

Mlisema hivi hivi wakati wa KORONA
Mlisema hivi hivi wakati wa MCA (umeme wa REA)
Mlisema hivi hivi wakati wa Bandari

Narudia kusema; kuna pande mbili , Yaani upande wa Mungu (kutakia mema) na upande wa shetani (kutakia mabaya)
Jichunguze vizuri binafsi unaitakia mema Tanzania ama unaitakia mabaya (hapo utajua unamwakilisha MUNGU ama SHETANI ) katika wewe kuwa mjumbe wammojawapo kiimani
 
Angalia wanalochukia

View attachment 1626020

Wanachukia Tanzania kuanza kujijenga upya kitaifa, wanataka tuendelee kuwa shamba la bibi. Halafu kuwa watanzania wanashangilia; watu wa hivyo sana

Wanajuwa kabisa ulaji kama vile walivyokuwa wanakula zamani unakwisha, na wanajuwa pia mataifa mengi ya Afrika wanaangalia Tanzania na wao wanapata idea kama wanaweza kuwagonea wanyonyaji. Ni change ambayo wazungu inawauma sana kuikubali.

Hapa hakuna kurudi nyuma, kama deal sio win-win, hakuna anayekaa mezani kuongea.
 
Pascal Mayalla njoo huku utetee Chama Cha Msukuma. Wizi wenu wa kura, mauaji, utekaji, dhuluma za kila aina sasa zinaligharimu taifa letu.
Kwani mngetenda haki mngepungukiwa kitu gani?
Najua mudu huu una type bonge la uzi na john 🚶pembeni.
Wasalimie Mbezi Juu, kesho saa nne ntakuwa kwa Mzee Juma Mugo Kula nyama choma na divai. Karibu
Mkuu Bujibuji , asante kwa makaribisho,
kwanza hakuna chama cha Msukuma, wala chama cha mtu, kilichopo ni Chama Cha Mapinduzi, CCM, ila kinaongozwa na Msukuma na sio kinamilikiwa na Msukuma hadi ukiite chama cha Msukuma!. One good thing kuhusu Msukuma huyu, tangu ashike uongozi wa chama, amekifanyia chama some very big transformation sasa chama kinapendwa na kinakubalika na Watanzania na hili wamelionyesha tarehe 28 October.

Tukija kwenye mada ya msingi, Hawa mabeberu wa US na EU tumeisha wazoea, tuliisha toa ushauri siku nyingi kwa Msukuma, on how to go about this.


P
 
According to the State Department, overall U.S. bilateral assistance to Tanzania, not including food aid, totaled an estimated $426 million in FY2019 and $548 million in FY2020. The Trump Administration requested $329 million for such assistance in FY2021.

Kwa ufupi ripoti ya hali ya kisiasa nchini tanzania toka magufuli kuingia madarakani imewashitua wafadhiri wa demokrasia na uwazi na hasa katika maswala ya ushiriki wa jamii na asasi zisizo za kiserikali.

Na utungwaji wa sheria mbalimbali kandamizi na kuhakikisha nchi inakuwa ya chama kimoja na upinzani unatoweka.

Katika kutubinya wataacha misaada inayogusa chakula tu na wanashawishi na jumuiya za kimataifa nao kutufanyia kama wao.
In summary

There are few signs that the governance trajectory in Tanzania discussed in this report is likely to change. One analyst of Tanzania sees President Magufuli and the CCM as pursuing “restorationist developmental nationalism”—a return to the sociopolitical development agenda and dominance of the CCM during the one-party state era, in which opposition parties play a limited role, if any.69 There are arguably a paucity of strong levers through which the United States and other aid donors might be able to press for a reversal of recent trends. Targeted restrictions on aid could potentially spur constructive responses from Tanzanian authorities in some instances, but the bulk of U.S. and other foreign aid supports development goals or other U.S. policy interests that such changes might hinder. Targeted sanctions, which the United States has used in one instance, 70 also are another possible pressure tool and vehicle for signaling U.S. concerns in selected instances, but are complex to administer and may have limited effect if sanctioned officials do not have personal or financial interests within U.S. jurisdictions. The governance trends discussed in this report also could potentially warrant a change in Tanzania’s eligibility for U.S. trade

Kwa ripoti kamili https://t.co/uTUEIj29Vg?amp=1
Mkuu Return Of Undertaker , huu ni muendelezo wa ubeberu tuu, tuliisha shauri what to do

P
 
Dona kantre huna hata kiwanda Cha kutengeneza pini.
Kifuatacho ni kupunguza kazi madaktari, manesi na watu wa maabara na kuajiri waganga was kienyeji, wachawi, wabashiri na wapiga ramli.
View attachment 1626014
Ukisikia dawa za asili unawaza waganga was kienyeji
Pale muhimbili Kuna kitengo maalumu Cha dawa za asili na kinatambulika kabisa
Mawazo yenu NI kusaidiw kila kitu na mabeberu
Dawa zetu zifanyiwe utafiti na wataalam
 
Dunia ya leo hata kama hukanyagi marekani lakini kama umejiunga kwenye jumuiya za kimataifa bhasi VETO power yao huwezi kuiepuka.
Ushawishi wa marekani ni mkubwa na sisi kama sisi sidhani kama tunaweza survive kama wakiamua kweli kutukazia

Viwanda vyetu vyenyewe ndio hivi ambavyo hata kutengeneza sindano ni shida, Export zetu zenyewe nadhani unazielewa na chanzo kikubwa cha foreign reserve unakijua. Kukaziwa sisi ni rahisi sanaaaa ila tuombe tu mambo yasiharibike
Tutatumia bidhaa kutoka China siio lazima marekani
 
Dunia ya leo hata kama hukanyagi marekani lakini kama umejiunga kwenye jumuiya za kimataifa bhasi VETO power yao huwezi kuiepuka.
Ushawishi wa marekani ni mkubwa na sisi kama sisi sidhani kama tunaweza survive kama wakiamua kweli kutukazia

Viwanda vyetu vyenyewe ndio hivi ambavyo hata kutengeneza sindano ni shida, Export zetu zenyewe nadhani unazielewa na chanzo kikubwa cha foreign reserve unakijua. Kukaziwa sisi ni rahisi sanaaaa ila tuombe tu mambo yasiharibike
Uko sahihi mkuu.
 
Wanajuwa kabisa ulaji kama vile walivyokuwa wanakula zamani unakwisha, na wanajuwa pia mataifa mengi ya Afrika wanaangalia Tanzania na wao wanapata idea kama wanaweza kuwagonea wanyonyaji. Ni change ambayo wazungu inawauma sana kuikubali.

Hapa hakuna kurudi nyuma, kama deal sio win-win, hakuna anayekaa mezani kuongea.
Wametunyonya Sana hao wapumbavu
 
Back
Top Bottom