Ndugu Watanzania,
Kipekee napenda kumshukuru Mungu kwa kuniamsha salama.
Sasa naanza kuona kwa vitendo kitu ambacho nilitumia my mental image na kuona kuwa nchi fulani zitaingilia uchaguzi wetu huu na viashiria vimeanza kuonekana sasa. Kitendo cha nchi yetu kukaa kwa takribani mwezi mmoja na kitu au miwili kwenye uchumi wa kati, ni njama tu ya kuitikisa nchi yetu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu. Samba mba na hilo, na hii imetokea tu baada ya kuanza kusikika kwa tetesi za kwamba, jina la Tundu Lissu linaelekea kukatwa na tume ya uchaguzi, na tumeiona barua ya mabeberu wanaoumtetea Tundu Lissu Amsterdam and Partners LLP.
Kama ulikuwa unamfuatilia Tundu Lissu tangu arudi nchini, amekuwa akitoa maneno ya kutisha na kuonyesha jeuri kubwa sana kwa serikali. Kwa mfano, kama TL ameweza kuwapata wadhamini kutoka Zanzibar bila ya kwenda kufanya mikutano ya hadhara visiwani kule, swali la kujiuliza hapa ni kwamba, mikutano aliyokuwa anaifanya huku Tanzania bara ilikuwa na lengo gani zaidi ya kuonyesha ubabe zidi ya NEC? Hii jeuri aliyonayo huyu ndugu inatoka kwa hawa mabeberu na si vinginevyo.
Aidha, kutikiswa huku kumeanza kuweka wazi wazi kuwa Tundu Lissu ni mgombea wa namna gani na mabeberu wanataka nini hasa kwenye uchaguzi huu. Naona mambo haya: (1) Tundu Lissu ni mgombea aliyeandaliwa na mabeberu ili aweze kumng’oa madarakani Mh. Magufuli; (2) hata kama Mh. Magufuli atashinda, Chadema hawatakubali, na mabeberu watawasaidia kwa namna yoyote ile ili kuleta taharuki baada ya uchaguzi mkuu.
Katika bara la Afrika, maraisi wa namna ya Mh. Magufuli ambao ni wazalendo kweli kweli katika nchi zao, na hufanya kila namna kulinda maliasili za nchi zidi ya uporaji wa mabeberu, huchukiwa sana na watu hawa. Tumeziona juhudi za Mh. Raisi kwa miaka hii mitano katika kuipigania nchi hii. Katika uchaguzi huu, jamaa hawa watafanya kila mbinu ili wamung’oe Mh. Raisi madarakani na kumuweka Tundu Lissu ili kuitumiza malengo yao. Ndugu watanzania wenzangu, nchi yetu imeanza kutikiswa, nawasihi tuiombee nchi yetu na Mh. Raisi pia ili Mungu ampe hekima na busura na nguvu ya kutuvusha salama dhidi ya mpango huu ovu. Kama Mungu alituvusha salama kwenye janga la Korona, naamini atatuvusha tena kwenye uchaguzi huu.
Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu.