Uchaguzi 2020 Mabeberu wameitikisa nchi, ajenda yao kuu ni kumuweka Tundu Lissu madarakani

Lijuakali alielezea nani mwizi wa kura
Kama kweli nyinyi CCM mnajiamini kuwa mmewafanyia maendeleo makubwa wananchi wa nchi hii, basi waachieni wenyewe wananchi waamue kwenye sanduku la kura.........

Lakini hizi tetesi zilizoenea hivi sasa kuwa nyinyi CCM mnapanga njama za kulikata jina la Tundu Lissu, zitaliingiza Taifa hili katika machafuko makubwa, ambayo hayajawahi shuhudiwa nchi hii
 
1. Futa kesi....
Raisi aingilie mahakama ama mnaishauri mahakama?
Na kwa order gani labda ama utaratibu gani?

Kwani haya yakifanyika serikali kama nia yao ni uchaguzi huru na wa haki wataathirika wapi?

1. Futa kesi zote zanazomkabili Lissu au ziahirishe hadi baada ya uchaguzi.

2. Acha hatima ya Lissu kiuchaguzi iamuriwe na wapiga kura kwa kuhakikisha uhuru na uwazi kamili katika kampeni, kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo.

Hao mabeberu unaowaongelea wewe wanatokea wapi katika hatua hizo mbili?

Bandugu mnatuchanganya. Mabeberu wanataka haki na nyie mnataka kuminya haki.

Kwa mtaji huu yaonesha yupi ni mbaya (zaidi) baina ya mabeberu na mkoloni mweusi nyie.
 
Mtanzania wa leo sio wa mwaka 1987 wengi wao wanajitambua! Ni yeye lissu tu
 
Ndugu Watanzania,

Kipekee napenda kumshukuru Mungu kwa kuniamsha salama.

Sasa naanza kuona kwa vitendo kitu ambacho nilitumia my mental image na kuona kuwa nchi fulani zitaingilia uchaguzi wetu huu na viashiria vimeanza kuonekana sasa. Kitendo cha nchi yetu kukaa kwa takribani mwezi mmoja na kitu au miwili kwenye uchumi wa kati, ni njama tu ya kuitikisa nchi yetu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu. Samba mba na hilo, na hii imetokea tu baada ya kuanza kusikika kwa tetesi za kwamba, jina la Tundu Lissu linaelekea kukatwa na tume ya uchaguzi, na tumeiona barua ya mabeberu wanaoumtetea Tundu Lissu Amsterdam and Partners LLP.

Kama ulikuwa unamfuatilia Tundu Lissu tangu arudi nchini, amekuwa akitoa maneno ya kutisha na kuonyesha jeuri kubwa sana kwa serikali. Kwa mfano, kama TL ameweza kuwapata wadhamini kutoka Zanzibar bila ya kwenda kufanya mikutano ya hadhara visiwani kule, swali la kujiuliza hapa ni kwamba, mikutano aliyokuwa anaifanya huku Tanzania bara ilikuwa na lengo gani zaidi ya kuonyesha ubabe zidi ya NEC? Hii jeuri aliyonayo huyu ndugu inatoka kwa hawa mabeberu na si vinginevyo.

Aidha, kutikiswa huku kumeanza kuweka wazi wazi kuwa Tundu Lissu ni mgombea wa namna gani na mabeberu wanataka nini hasa kwenye uchaguzi huu. Naona mambo haya: (1) Tundu Lissu ni mgombea aliyeandaliwa na mabeberu ili aweze kumng’oa madarakani Mh. Magufuli; (2) hata kama Mh. Magufuli atashinda, Chadema hawatakubali, na mabeberu watawasaidia kwa namna yoyote ile ili kuleta taharuki baada ya uchaguzi mkuu.

Katika bara la Afrika, maraisi wa namna ya Mh. Magufuli ambao ni wazalendo kweli kweli katika nchi zao, na hufanya kila namna kulinda maliasili za nchi zidi ya uporaji wa mabeberu, huchukiwa sana na watu hawa. Tumeziona juhudi za Mh. Raisi kwa miaka hii mitano katika kuipigania nchi hii. Katika uchaguzi huu, jamaa hawa watafanya kila mbinu ili wamung’oe Mh. Raisi madarakani na kumuweka Tundu Lissu ili kuitumiza malengo yao. Ndugu watanzania wenzangu, nchi yetu imeanza kutikiswa, nawasihi tuiombee nchi yetu na Mh. Raisi pia ili Mungu ampe hekima na busura na nguvu ya kutuvusha salama dhidi ya mpango huu ovu. Kama Mungu alituvusha salama kwenye janga la Korona, naamini atatuvusha tena kwenye uchaguzi huu.

Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu.
Mm kama itatokea hivyo nitamshukuru sana mungu itakuwa asante mungu nikikumbuka walivyo niacha masikini kupitia uvuvi mpaka leo engine zangu wameziteka walivyo kuja walituomba tuwaonyeshe nyavu zetu iliwazikague tulifanya walichotaka matokeo yake walizichoma bila kuzipima nakuteka engine wanadai tuwalipe pesa ndio tupate engine zetu kwenye vituambavyo tulisalimisha vipimwe huu uchomaji unatoka wapi bila kupima na kuteka engine zetu kwakweli ikitokea utawala kutolewa binafsi nitamshukuru mungu anaetupenda
 
1. Futa kesi....
Raisi aingilie mahakama ama mnaishauri mahakama?
Na kwa order gani labda ama utaratibu gani?

Uzi huu unajieliza vyema:

Pongezi Sirro, Mahakama na Tume ya Uchaguzi kazi kwenu.

Nani asiyejua uhuru wa vyombo vinavyosemekana kuwa ni huru unavyoingiliwa na mamlaka na hasa katika awamu hii?

Ndiyo maana ni kiu ya wengi kuona kuwa mgombea ajaye ni yule:

IMG_20200804_210728_515.jpg

Na si huyu anayetumia dola kwa namna yoyote ile (zikiwamo janja janja na hata ghiliba) ili kubakia madarakani:

IMG_20200820_093436_378.jpg

Safari hii tutabanana hapa hapa.

Sera ziko wapi kuhusu "uhuru wetu?"

Hapendwi mtu hapa!
 
Chorus: tumeibiwa kura...[emoji3][emoji3]
Uzi huu unajieliza vyema:

Pongezi Sirro, Mahakama na Tume ya Uchaguzi kazi kwenu.

Nani asiyejua uhuru wa vyombo vinavyosemekana kuwa ni huru unavyoingiliwa na mamlaka na hasa katika awamu hii?

Ndiyo maana ni kiu ya wengi kuona kuwa mgombea ajaye ni yule:

View attachment 1546434

Na si huyu anayetumia dola kwa namna yoyote ile (zikiwamo janja janja na hata ghiliba) ili kubakia madarakani:

View attachment 1546435

Safari hii tutabanana hapa hapa.

Sera ziko wapi kuhusu "uhuru wetu?"

Hapendwi mtu hapa!
 
Ndugu Watanzania,

Kipekee napenda kumshukuru Mungu kwa kuniamsha salama.

Sasa naanza kuona kwa vitendo kitu ambacho nilitumia my mental image na kuona kuwa nchi fulani zitaingilia uchaguzi wetu huu na viashiria vimeanza kuonekana sasa. Kitendo cha nchi yetu kukaa kwa takribani mwezi mmoja na kitu au miwili kwenye uchumi wa kati, ni njama tu ya kuitikisa nchi yetu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu. Samba mba na hilo, na hii imetokea tu baada ya kuanza kusikika kwa tetesi za kwamba, jina la Tundu Lissu linaelekea kukatwa na tume ya uchaguzi, na tumeiona barua ya mabeberu wanaoumtetea Tundu Lissu Amsterdam and Partners LLP.

Kama ulikuwa unamfuatilia Tundu Lissu tangu arudi nchini, amekuwa akitoa maneno ya kutisha na kuonyesha jeuri kubwa sana kwa serikali. Kwa mfano, kama TL ameweza kuwapata wadhamini kutoka Zanzibar bila ya kwenda kufanya mikutano ya hadhara visiwani kule, swali la kujiuliza hapa ni kwamba, mikutano aliyokuwa anaifanya huku Tanzania bara ilikuwa na lengo gani zaidi ya kuonyesha ubabe zidi ya NEC? Hii jeuri aliyonayo huyu ndugu inatoka kwa hawa mabeberu na si vinginevyo.

Aidha, kutikiswa huku kumeanza kuweka wazi wazi kuwa Tundu Lissu ni mgombea wa namna gani na mabeberu wanataka nini hasa kwenye uchaguzi huu. Naona mambo haya: (1) Tundu Lissu ni mgombea aliyeandaliwa na mabeberu ili aweze kumng’oa madarakani Mh. Magufuli; (2) hata kama Mh. Magufuli atashinda, Chadema hawatakubali, na mabeberu watawasaidia kwa namna yoyote ile ili kuleta taharuki baada ya uchaguzi mkuu.

Katika bara la Afrika, maraisi wa namna ya Mh. Magufuli ambao ni wazalendo kweli kweli katika nchi zao, na hufanya kila namna kulinda maliasili za nchi zidi ya uporaji wa mabeberu, huchukiwa sana na watu hawa. Tumeziona juhudi za Mh. Raisi kwa miaka hii mitano katika kuipigania nchi hii. Katika uchaguzi huu, jamaa hawa watafanya kila mbinu ili wamung’oe Mh. Raisi madarakani na kumuweka Tundu Lissu ili kuitumiza malengo yao. Ndugu watanzania wenzangu, nchi yetu imeanza kutikiswa, nawasihi tuiombee nchi yetu na Mh. Raisi pia ili Mungu ampe hekima na busura na nguvu ya kutuvusha salama dhidi ya mpango huu ovu. Kama Mungu alituvusha salama kwenye janga la Korona, naamini atatuvusha tena kwenye uchaguzi huu.

Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu.
hakuna Cha mzalendo Wala nn tofauti yake kubwa na watangulizi wake ni kwamba yy anakula peke yake hataki wengine wale,tunazidi kurud nyuma kwa speed endelea kuwaita mabeberu wanaotusaidia mpk arv
 
Back
Top Bottom