A
Anonymous
Guest
Pia, tuliambiwa Wachina wanakuja lakini tangu Mwaka 2025 hadi leo kimya, treni ya abiria ni mbovu, imechakaa haifai hata kidogo, na tunapoelekea itakuja kuua Watu kutokana na kuchakaa kwake, mabehewa yanayumba sana, safari ya kuchukuwa saa 24 inachukua saa 48.
Hivyo, tunaiomba Serikali ituletee mabehewa na locomotives mpya, tunateseka jamani, mbona TRC wana treni za abiria zaidi ya 3, TAZARA kuna treni 1 tu na lenyewe kila trip moja likirudi lazima lichomelewe.
Treni ya abiria ya TAZARA ni kama Jahannam inayotembea abiria tunaumizwa sana na hali hii.
Yapo mengi ndani ya tazara ambayo hatuwezi kuyaelezea yakaisha. 🙏🙏🙏