Mabere Marando afunguka kujiuzulu Usalama wa Taifa

Mabere Marando afunguka kujiuzulu Usalama wa Taifa

Marando hakuwa TISS, TISS ni taasisi mpya iliyoanza 1998 , alikuwa Idara ya Usalama wa Taifa, ambayo haikuwa hata na sheria yake.....kama jina linavyosema, ilikuwa ni Idara tu chini ya ofisi ya raisi

TISS ilikuwapo tangu miaka ya themanini ikiwa na watu makini kama akina Walingozi na Kuhanwa; ilianzishwa chini ya sheria ya usalama wa Taifa ya mwaka 1970 ikiwa ni muda mfupi wa jaribio la mapinduzi lililofanywa na timu ya Kambona. Hiyo sheria ya mwaka 1998 iliunda ilipandisha TISS kuwa idara kamili ya serikali kinyume na huko nyuma ambako ilikuwa kama taasisi ya kisiri chini ya ofisi ya Rais; Marando alitumikia TISS hadi katikati ya miaka ya themanini alipoanzisha harakati za NCCR.
 
Mwongo huyu. Ni lini mtu anajiuzulu usalama wa taifa? wakikulazimisha kujiuzulu hutafika mbali na siri zao. Mabele na Mrema wako usalama wa taifa ktk kitengo maalum cha vyama vya siasa. Aje hapa abishe.
Naomba kuongeza hapo... Maarim seif... Zitto na Prof....
 
Marando alifukuzwa kama mbwa kwa tabia mbaya na utovu wa nidham, aliasi mapambano ya vita kati ya tz na uganda na inasemekana hakuwahi kuingia ofisi za usalama wala kufanya hiyo kazi, alichukuliwa kutoka chuoni moja kwa moja kwenda vitani, yakamshinda kule akatoroka na ndio akafutwa usalama. Kama uongo aje ajibu hii post
Mbona unatumia nguvu nyingi sana
 
Back
Top Bottom