Chama kilichojengwa katika misingi imara ya kidemokrasia ni vigumu sana kukisambaratisha.Sijui CHADEMA imejengwa kwa misingi gani.
Mtakumbuka kuwa vugu vugu la vyama vingi lilianzishwa na hawa akina marando. Kosa kubwa walilofanya ni kutaka kuingia madarakani kabla ya kujiimarisha vema. mrema alipohamia NCCR alikwenda na kundi lake kama msemaji mmoja alivyonena hapo juu. Kundi hili likadhani kuwa linamamlaka ya kutwaa chama kwasababu ya mrema. Chama kikawa Mrema na si NCCR. Akina marando wakazidiwa nguvu.
Tunakumbuka kuwa mrema aliandaliwa mambo mazuri katika mdahalo[sera],lakini kwa vile alijua kuwa ni maarufu eti ana mtaji wa watu akaongea upupu wa kukamata dhahabu.
Mrema akawa dictator akitaka fulani awe kiongozi na iwe hivyo,chama kikafa kwa ubinafsi wa mrema ambao hauna shaka kwa mtu mwenye akili timamu. Hebu fikiri,eti ni mwenyekiti wa TLP halafu anasema CCM haikamatiki siku ya pili yake anakwenda kusimamia uchaguzi wa chama chake kwa mgombea urais!!1. Huyu anataka uenyekiti aendeshe maisha lakini hana lolote lile la maana.
Marando alinitia shaka alipopitishwa na wabunge wa CCM kugombea ubunge EA.Baada ya hapo hatukumsikia tena. Lakini hii haiondoi ukweli kuwa ni mtu makini. Kujiunga na Chadema sioni tatizo, anakaribishwa sana. Jambo la muhimu ni Chadema kuelewa kuwa yeye ni kama mwanachama mwingine yoyote na kuwepo kwake ni kuimarisha chama na si kama ngazi. Asipewe ''special treatment'' lakini pia asinyimwe haki zake.
Chadema iongozwe kwa ''principles'' na si kwa matakwa.
Kuna watu wamejitoa sana Chadema,hawa wabaki na heshima zao na si kwasababu eti fulani kaja basi kesho yake ni makamu au katibu mkuu.
Kama chama kitafuata misingi imara ya sheria na taratibu mtu mmoja hawezi kukisambaratisha.
Leo hii watu wangesikia Warioba, Sitta au Msuya wamejiunga na Chadema wangefurahi kwa kisingizio cha upinzani halisi utatoka CCM, vipi Marando awe tofauti!!!
Kama hatutakubali mawazo mbadala na changamoto zinazotokana na demokrasia tutakuwa tume via kimawazo. Kama watu wataogopa dhana ya chama kusambaratishwa na mtu mmoja basi ni wazi kuwa chama hicho hakipo tayari kupewa mamlaka.
Leo hii tumesimama imara kama taifa si kwasababu ya umaarufu wa Mwl Nyerere,bali misingi ya utaifa aliyoijenga. Vivyo hivyo Chadema kiwe ni chama chenye misingi ya kisheria na taratibu na umaarufu wake uwe kwa chama na si kwa mtu au kikundi cha watu, hakuna wa kukisambaratisha.
Ahsanteni