Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea gawio na michango kutoka mashirika na taasisi za umma Ikulu jijini Dar es Salaam, leo tarehe 11/06/2024.
MABEYO (CDF MSTAAFU): Vijana wanakosa mwelekeo, tunajenga hofu kwa taifa la kesho
Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu) akizunguza kwa niaba ya Wenyeviti wa Bodi amesema kuna umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na na kuishi katika maoni ya Serikali kwa kuzingatia mabadiliko ya kiuchumi ili kutengeneza njia nzuri kwa Taifa.
Amesema hayo wakati wa kukabidhi gawio na michango kwa Rais Samia Suluhu kutoka katika mashirika na Taasisi za Umma Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Juni 11, 2024.
Viongozi wa Serikali, Wakuu wa Mashirika na Taasisi za umma pamoja na Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kupokea Gawio na Michango kutoka kwa Mashirika na Taasisi za Umma, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya kupokea Gawio na Michango kutoka kwa Mashirika na Taasisi za Umma, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni, 2024.