Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haujapita katika jimbo lake (Kigoma mjini)Zitto lazima atapinga mradi huu!
Acha upuuzi, kawapazie sauti Wamarekani, sisi huyo anatuhusu vipi!? Tuelekeze kituo tukajiandikishe tumpigie kura basi!The world needs Michael Bloomberg let us all support him. Paza sauti popote ulipo duniani MICHAEL BLOOMBERG
Sio mjuzi wa hii barabara ila ndio inayounganisha mkoa wa kigoma na jiji LA Mwanza Kwa njia ya Lami kupitia nyakanazi? Sababu navyojua hiyo bara bara ilikuwa na mkandarasi tayari, au ni nyingine?
Yote haya yananikumbusha maneno ya mbunge wa KILWA..Mr. Bwege... alisema, nanukuu.... 'CCM TUNAWAJUA, WATABANAA LAKINI KULEE MWISHOOOONIIIII WATAACHIA'... mwisho wa kunukuuView attachment 1365779
SERIKALI ya Tanzania imetiliana saini mkataba na wakandarasi wanne wa kampuni ya ujenzi ya China kwa ajili ya barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo wilayani Kakonko hadi Manyovu wilayani Buhigwe yenye urefu wa kilometa 260 kwa gharama ya Sh bilioni 584.7.
Waziri wa Ujenzi, Isack Kamwelwe aliongoza viongozi wa Serikali ya Tanzania kushuhudia utiaji saini huo ambao Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Patrick Mfugale aliongoza utiaji saini huo kwa Serikali ya Tanzania ambao unafanyika kutokana na mkopo wa riba nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) huku Serikali ya Tanzania ikitoa kiasi cha Sh bilioni 58 kuchangia ujenzi huo.
Akizungumza kabla ya utiaji saini, Kamwelwe alisema ujenzi huo wa barabara ni matokeo ya ahadi aliyotoa Dk John Magufuli wakati wa kampeni za urais mwaka 2015. Alisema aliona ukanda wa magharibi una changamoto kubwa. Akitoa taarifa kabla ya utiaji saini huo, Mfugale alisema mradi huo wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umegawanywa kwenye vipande vinne kuwezesha ujenzi wake kufanywa kwa haraka na katika kipindi cha miaka mitatu barabara hiyo inapaswa ianze kutumika.
Aliwataja wakandarasi hao kuwa ni Zhejiang Communication Construction Group Co. Ltd iliyopewa kipande cha Manyovu hadi Kasulu kilometa 68.2 kwa gharama ya Sh bilioni 76.1 na Sinohydro Corporation Ltd iliyopewa kipande cha kuanzia Kasulu Mjini hadi Mvugwe wilayani Kasulu kilometa 70.5 kwa gharama ya Sh bilioni 83.7.
Wengine ni STECOL Corporation iliyopewa kipande cha kuanzia Kijiji cha Mvugwe hadi eneo la njia panda ya Kambi ya Wakimbizi Nduta wilayani Kibondo kilometa 59.3 kwa gharama ya Sh bilioni 84.7 na China Hennan International Cooperation Group (CHICCO) kilometa 62.5 iliyopewa kipande cha kuanzia njia panda ya Kambi ya Wakimbizi ya Nduta hadi Kijiji cha Kabingo kwa gharama ya Sh bilioni 95.5.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema atasimamia kwa karibu kuhakikisha fedha za utekelezaji wa mradi huo zinatolewa kwa wakati ili kuwezesha kutekelezwa kwa muda huo uliopangwa.
Dk Mpango alisema ujenzi wa barabara hiyo siyo muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Kigoma na watu wake pekee, bali kwa Taifa kutokana na mkoa kuwa kitovu cha uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa barabara la Afrika; na kuongeza kuwa lazima Tanroads waoneshe weledi wao katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo kwa viwango na wakati huku akionya wakandarasi kutoyumbisha na kuomba kuongezewa muda bila sababu.
Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema barabara hiyo ni tukio muhimu kwa mkoa huo kwani kuna watu ambao hawajawahi kuona lami hivyo kwao jambo hilo lilileta manung’uko makubwa na kujiona kama siyo sehemu ya Tanzania.
Akitoa neno kwa niaba ya wananchi wake, Mkuu wa mkoa, Emmanuel Maganga alisema kwao mradi huo ni moja ya miradi iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu kutokana na umuhimu wake kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo kwani ni mkoa wa kimkakati kwa ajili ya soko la Ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu. Aliwataka wakandarasi kuzingatia kuajiri vijana kutoka mkoani humo katika kazi ambazo hazihitaji utaalamu.
SijakuelewaNyanza Road ways co. Ltd miaka nenda rudi.
Kampuni ya wenyewe.
akili za kijinga sana hizi. Yaani kila mradi wanajenga wageni wakati vijana wetu hawana kazi, why?
Ninatamani sana pangekuwa na ramani za barabara hizi, lakini sijui kwa nini hilo huwa ni gumu kulifanya!Sio mjuzi wa hii barabara ila ndio inayounganisha mkoa wa kigoma na jiji LA Mwanza Kwa njia ya Lami kupitia nyakanazi? Sababu navyojua hiyo bara bara ilikuwa na mkandarasi tayari, au ni nyingine?
Zitto lazima atapinga mradi huu!
siwezi kupinga kwa sababu ni moja ya miradi nimepigia kelele maisha yangu yote ya Ubunge na ipo kwenye ilani ya ACT mwaka 2015 na pia African Development Bank niliwasumbua sana kuhusu Mradi huu.
Wala Mradi huu hautakuwa sababu ya watu wa Kigoma kuipa kura CCM kwani sio hisani bali ni Haki yetu
Zana Za Kilimo aliitisha wazee wake ili mradi usifanikiwe , na akishindwa kwa njia za asili ataandika barua kwa "Mabeberu"Sio mjuzi wa hii barabara ila ndio inayounganisha mkoa wa kigoma na jiji LA Mwanza Kwa njia ya Lami kupitia nyakanazi? Sababu navyojua hiyo bara bara ilikuwa na mkandarasi tayari, au ni nyingine?
Hii ndiyo faida ya wananchi kuwa na utayari na uthubutu wa kuchagua na kuishi na "strong opposition parties". Katika maeneo hayo chama tawala kinakosa namna zaidi ya kuanza kuwekeza miradi mikubwa ya maendeleo ili kuwafanya wavutiwe na sera zao.View attachment 1365779
SERIKALI ya Tanzania imetiliana saini mkataba na wakandarasi wanne wa kampuni ya ujenzi ya China kwa ajili ya barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo wilayani Kakonko hadi Manyovu wilayani Buhigwe yenye urefu wa kilometa 260 kwa gharama ya Sh bilioni 584.7.
Waziri wa Ujenzi, Isack Kamwelwe aliongoza viongozi wa Serikali ya Tanzania kushuhudia utiaji saini huo ambao Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Patrick Mfugale aliongoza utiaji saini huo kwa Serikali ya Tanzania ambao unafanyika kutokana na mkopo wa riba nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) huku Serikali ya Tanzania ikitoa kiasi cha Sh bilioni 58 kuchangia ujenzi huo.
Akizungumza kabla ya utiaji saini, Kamwelwe alisema ujenzi huo wa barabara ni matokeo ya ahadi aliyotoa Dk John Magufuli wakati wa kampeni za urais mwaka 2015. Alisema aliona ukanda wa magharibi una changamoto kubwa. Akitoa taarifa kabla ya utiaji saini huo, Mfugale alisema mradi huo wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umegawanywa kwenye vipande vinne kuwezesha ujenzi wake kufanywa kwa haraka na katika kipindi cha miaka mitatu barabara hiyo inapaswa ianze kutumika.
Aliwataja wakandarasi hao kuwa ni Zhejiang Communication Construction Group Co. Ltd iliyopewa kipande cha Manyovu hadi Kasulu kilometa 68.2 kwa gharama ya Sh bilioni 76.1 na Sinohydro Corporation Ltd iliyopewa kipande cha kuanzia Kasulu Mjini hadi Mvugwe wilayani Kasulu kilometa 70.5 kwa gharama ya Sh bilioni 83.7.
Wengine ni STECOL Corporation iliyopewa kipande cha kuanzia Kijiji cha Mvugwe hadi eneo la njia panda ya Kambi ya Wakimbizi Nduta wilayani Kibondo kilometa 59.3 kwa gharama ya Sh bilioni 84.7 na China Hennan International Cooperation Group (CHICCO) kilometa 62.5 iliyopewa kipande cha kuanzia njia panda ya Kambi ya Wakimbizi ya Nduta hadi Kijiji cha Kabingo kwa gharama ya Sh bilioni 95.5.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema atasimamia kwa karibu kuhakikisha fedha za utekelezaji wa mradi huo zinatolewa kwa wakati ili kuwezesha kutekelezwa kwa muda huo uliopangwa.
Dk Mpango alisema ujenzi wa barabara hiyo siyo muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Kigoma na watu wake pekee, bali kwa Taifa kutokana na mkoa kuwa kitovu cha uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa barabara la Afrika; na kuongeza kuwa lazima Tanroads waoneshe weledi wao katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo kwa viwango na wakati huku akionya wakandarasi kutoyumbisha na kuomba kuongezewa muda bila sababu.
Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema barabara hiyo ni tukio muhimu kwa mkoa huo kwani kuna watu ambao hawajawahi kuona lami hivyo kwao jambo hilo lilileta manung’uko makubwa na kujiona kama siyo sehemu ya Tanzania.
Akitoa neno kwa niaba ya wananchi wake, Mkuu wa mkoa, Emmanuel Maganga alisema kwao mradi huo ni moja ya miradi iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu kutokana na umuhimu wake kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo kwani ni mkoa wa kimkakati kwa ajili ya soko la Ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu. Aliwataka wakandarasi kuzingatia kuajiri vijana kutoka mkoani humo katika kazi ambazo hazihitaji utaalamu.
Hiyo nyingineSio mjuzi wa hii barabara ila ndio inayounganisha mkoa wa kigoma na jiji LA Mwanza Kwa njia ya Lami kupitia nyakanazi? Sababu navyojua hiyo bara bara ilikuwa na mkandarasi tayari, au ni nyingine?
Tangu lini barabara ya kigoma Nyakanazi ikapita Manyovu?
Wewe zitto kweli unatabia za umaraya maraya , juzi hapa umepinga tanzania tusipewe mkopo! Umaraya wa kupiga kelele ili serikari ya ccm ipewe huu mkopo wa kujenga hii barabara ulitoka wapi.siwezi kupinga kwa sababu ni moja ya miradi nimepigia kelele maisha yangu yote ya Ubunge na ipo kwenye ilani ya ACT mwaka 2015 na pia African Development Bank niliwasumbua sana kuhusu Mradi huu.