Mabilioni yanayotumika kugawa magari na vifaa kwa Polisi wakati huu, je, Serikali inaboresha na maslahi yao pia?

Mabilioni yanayotumika kugawa magari na vifaa kwa Polisi wakati huu, je, Serikali inaboresha na maslahi yao pia?

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Siyo siri moja kati ya majeshi ambayo naweza kukiri imani yake kwa Wananchi wengi ni kama imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na matukio mbalimbali yanayowahusu nchini basi ni Jeshi la Polisi.

Polisi wanahusiana na Wananchi moja kwa moja tofauti na majedhi mengine, inawezekana hiyo ikawa inachangia msuguano mara nyingi baina ya pande hizo mbili kwa kuwa Mwananchi anamtegemea Askari Polisi na Askari naye anamtegemea na kumtumikia Mwananchi.

Hivyo, basi ni jukumu la Jeshi la Polisi lenyewe kufanya jitihada ili imani ya Wananchi iwe juu kwao na waendelee kuliamini, ukiona imani inatia shaka basi ujue hata hali ya usalama inaweza ikatia shaka pia.

Kwa sasa Tanzania tupo katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025, kama kawaida wakati wa Uchaguzi kunakuwa na ‘tensheni’ ya juu, ndivyo ilivyo sasa, na wanaokuwa na majukumu makubwa muda mwingi ni Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na vitengo vingine kadhaa kuhakikisha usalama wa ndani ya Nchi unalindwa.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya ugawaji au usambazaji wa magari ya kazi kwa Jeshi la Polisi unaofanywa na Serikali, mbali na hapo pia kuna vifaa mbalimbali ambavyo vimekuwa vikisambazwa na kuweka hadharani.

Inawezekana ikaonekana ni tukio la kawaida, lakini kuanzia Aprili au Mei kama sijakosea kumekuwa na matukio mengi ya aina hiyo, ikimaanisha ulinzi unaboreshwa (wanaofanya hivyo wanajua sababu za kufanya hivyo na kutangaza hadharani kuwa wamegawa vifaa hivyo).

Pia soma:
~ Jeshi la polisi Singida lapokea magari mapya manne aina ya Toyota Hilux Double Cabin ili kuimarisha ulinzi
~ Rc Ruvuma atoa shukrani kwa rais Samia kutoa magari mapya 24 kwa ajili ya shughuli za jeshi la polisi
~ Serikali yakabidhi magari 24 kwa Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma kuimarisha ulinzi na usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025


Mbali na hapo kumekuwa na matukio ya vikosi mbalimbali vya ulinzi hasa Jeshi la Mgambo kuonekana wakifanya mazoezi ya hapa na pale maeneo tofauti.

Hoja yangu
Sasa kama Serikali imeona umuhimu wa kugawa vifaa mbalimbali na kuratibu mazoezi ya Mgambo, inamaanisha hapo wanatumia gharama kubwa kufanya yote hayo, Askari wanaofanyiwa hivyo au hao Mgambo tunaishi nao mitaani huku.

Je, Serikali pia inaboresha maslahi yao binafsi au mazingira ya wao kuwa comfortable kufanya kazi au wanawajazia vifaa tu kwa kuwa wanajua wanachokitaka wao?

Tunaishi na Askari kama nilivyosema, tunajua hali zao, tunajua maisha yao, hasa wale Askari wa kawaida, achana na wale Askari wenye vyeo ambao wanakula “good time”, je maslahi yao binafsi bia yanaboreshwa au hayo wanafanya kimyakimya?

Niliona hii taarifa: Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amekabidhi magari 8 aina ya Toyotaland Cruiser 2 Hardtop na Toyota Hilux Double Cabin 6 kwa Jeshi la Polisi mkoani humo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3. Magari hayo yaliyokabidhiwa katika Viwanja vya Polisi Mabatini Jijini Mwanza...”

Zaidi soma ~
FFU wakabidhiwa Magari 8 na Mkuu wa Mkoa Mwanza kuimarisha Utendaji wa Jeshi la Polisi

Najua ulinzi na usalama ni muhimu sana tena sana lakini nikajiuliza hizo Bilioni 1.3 zimetumika Mwanza tu, ukijumlisha na Mikoa mingine tangu waanze kugawa vifaa hivyo, mpaka sasa wametumia Bilioni ngapi?

Mfano, nus utu ya bajeti waliyotumia mpaka sasa wangetumia kuwajengea nyumba Askari au kulipa madeni mbalimbali wanayodaiwa au kulipa wastaafu wa Jeshi hilo, au kuwakopesha Askari, hawaoni kwamba wangekuwa wamesaidia Mamlioni ya watu watakaonufaika na fedha hizo?
 
Hayo ni maandalizi ya kukinukisha maana hawana imani ya kushinda uchaguzi mwaka huu...
 
Ukiachilia mbali nyongeza ya mishahara kwa watumishi wote naona askari wa majeshi karibu yote wamepandishwa vyeo hapo lazima kuna ongezeko la mishahara.

Ila mishahara siku zote haitoshi hasa kwa wafanyakazi wa kawaida suala la kuboresha maisha yako linabaki kwako mwenyewe kwa kufanya biashara zingine ila ukitegemea mshahara ni changamoto, labda wale wakuu wa himaya na idara ndo wanalamba asali
 
Nimedokezwa kuwa:-
Polisi kuruta analipwa 2M.

Polisi mwenye nyota 1 analipwa 3M, 2 analipwa 4M, 3 analipwa 5M.

Kamanda Muliro analipwa 15M, IGP analipwa 50M.

Ndiyo maana polisi wanampiga mpk mawakili mahakamani.
 
Back
Top Bottom