Mabilioni Yanga usajili utashtua, Aziz Ki balaa!

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
KIASI kikubwa cha fedha ambacho Yanga itakivuna mwishoni mwa msimu kinaipa jeuri ya kunasa mastaa wasiopungua watatu kutoka katika timu yoyote barani Afrika na ikamudu kuwalipa mishahara na posho bila presha kwa mkataba wa miaka miwili.

Ikiwa itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Yanga itajihakikishia kitita kisichopungua Sh 4 bilioni ambacho kinatokana na mikataba minono ambayo imesaini na kampuni tofauti lakini fedha za zawadi kwa washindi wa Ligi. Kiasi kikubwa cha fedha itavuna kupitia mkataba wake wa maudhui na kampuni ya Azam Media ambao kuna kipengele kinachoipa fursa ya kupata kitita cha Sh 3 bilioni kama bonasi kwa kutwaa ubingwa au kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi kila msimu.

Timu hiyo itapata pia kiasi cha Sh 500 milioni kutoka Azam Media kama fedha za bonasi au zawadi kwa bingwa wa Ligi Kuu ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mkataba wa haki za matangazo ya ligi baina ya kampuni hiyo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Yanga pia inaripotiwa itapata bonasi ya Sh 500 milioni kutoka kwa wadhamini wao wengine, kampuni ya GSM ikiwa watatwaa ubingwa wa ligi pia watapewa kiasi cha Sh 100 milioni na mdhamini wao mkuu, kampuni ya Sportpesa.

Jina la nyota linalotajwa na vigogo wa Yanga ni mshambuliaji wa Burkina Faso anayeichezea Asec Mimosas, Aziz Ki ambaye kwa mujibu wa ripoti, tayari ameshafikia makubaliano ya awali.

Iko hivi, Aziz inadaiwa atalipwa mshahara wa Dola 5,000 (Sh 11 milioni) kwa mwezi ambapo kwa kipindi cha miaka miwili, Yanga itamlipa mshahara wa jumla kiasi cha Dola 120,000 (Sh 279 milioni).

Ikisajili mastaa watano na kuwalipa kiasi hicho cha fedha kama mshahara, maana yake Yanga itatumia kiasi cha Dola 600,000 (Sh 1.3 bilioni) kwa mwaka kuwalipa mshahara na kwa miaka miwili, Yanga itatumia kiasi cha Sh 2.6 bilioni kuwalipa nyota hao.

Katika fungu la Sh 4 bilioni ambazo itapata, Yanga itabakia na kiasi cha Sh 1.4 bilioni (Dola 600000) ambacho kinaweza kutumika kama ada ya usajili ya wachezaji hao kwa kila mmoja kupata wastani wa Dola 150,000 (Sh 349 milioni).

Kwa mujibu wa mtandao wa transfermarkt unaojishughulisha kufanya tathmini ya bei za wachezaji na thamani zao, kuna nyota zaidi ya 10 katika klabu mbalimbali barani Afrika ambao thamani zao sokoni kwa sasa ni Dola 150,000 au chini ya hapo hivyo Yanga inaweza kuwapata wakicheza kwa nafasi tofauti.

Baadhi ya wachezaji hao ni mabeki, Nathan Idumba (Cape Town City), Chadrack Isaka Boka (FC Lupopo), Sidi Yacoub na Jacques Themopeie (AS Vita), Moses Phiri (Zanaco), John Ching’andu (Zesco United), Prince Dube (Azam), Wonlo Coulibaly na Ibrahim Bance (Asec Mimosas) pamoja na Richard Boro (FC San Pedro).

Mjumbe wa Kamati ya Usajili na Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said alilithibitishia Mwanaspoti kuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanasajili nyota ambao wataifanya izidi kuwa tishio msimu ujao.

“Kikosi chetu kimeonyesha mafanikio makubwa msimu huu lakini tuna mashindano ya kimataifa msimu ujao ambayo mkakati wetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri hivyo tutahakikisha tunasajili wachezaji wenye viwango bora zaidi ambao watatuwezesha kutimiza malengo hayo,” alisema Hersi.

Kwa upande wa, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa kwa kushirikiana na wadhamini wao kampuni ya GSM, watafanya usajili utakaotikisa sio tu hapa nchini bali Afrika kwa ujumla. Kocha Nabi Mohammed amesema watasajili kwa umakini mkubwa na kwa kuzingatia ubora.

Credit: mwananchi
 
TEh teh,teheeeeeeeeee,koh koh koh,ngoja nikohoe kwanza mie
eti bilioni4,hahaaaaaaaaaaaa

Maaaninaaaaaaaaaaaaaa,tuwekee hako kasehemu cha huo mkataba.

Yaaani ubingwa Azam awape mil500,halafu bonus awape bil3,kawadanganye kina Manara brooo
 
Bilioni ngapi eti? Subutuuuuu. Hapa tu nimetoka kusikia kuwa TFF msimu ujao itaongeza zawadi na kufikia jumla ya Tsh. 1.8 B napo sio sasa ni kwamsimu ujao
 
Kuna mikataba miwili tofauti ya Adam
1.Mkataba kati ya Azam TV na TFF (TV Rights)-ambapo bingwa anapata milioni 500

2.Mkataba kati ya Azam TV na Yanga-Huu unahusu haki ya maudhui yote yanahusu Yanga,yanamilikiwa na Azam na Mkataba huo ni Wa Billion almost 30 kwa miaka 10.….…....ila kuna kipengele cha Bonuses endapo timu ikichukua ubingwa inapata Bonus ya Billion 3
 
BILIONI (3) na MILIONI (750) !!

July 8, 2021,, Mtendaji mkuu wa Azam media Tido Mhando na mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla walisaini mkataba wa mashirikiano ya MAUDHUI baina ya Yanga SC na Azam TV (MEDIA PARTNERSHIP).

Thamani ya mkataba huo ni Tsh 41.64 BILIONI kwa miaka kumi (10).

Yanga watapokea Tsh 34.8 BILIONI kutoka AZAM TV baada ya makato mbalimbali. Yanga na Azam Tv watashirikiana kuandaa na kurusha MAUDHUI ya klabu ya Yanga kama ;

▪️ Mazoezi ya timu.
▪️ Maandalizi ya mechi
▪️ Mechi za kirafiki na Exclusive mbalimbali za klabu ya Yanga kama usajili, Interviews na vitu vingine.
.
.
Klabu ya Yanga itakuwa ikipokea Tsh 200 Milioni kila mwezi kuanzia msimu huu (2021-22) hadi (2030). Pesa hiyo itakuwa ikiongezeka kila msimu.
.
.
📌 Kupitia mkataba huu klabu ya Yanga itapokea BONUS ya Tsh (3) BILIONI KILA INAPOSHIKA NAFASI YA (1) AU YA (2) kwenye ligi kuu Tanzania bara.
.
.
Yanga wataendelea kupata Bonus kila wanapofanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali.
______________________________________
.
.
Ukiacha Mkataba huo wa MAUDHUI, Yanga wakiwa MABINGWA watapata Tsh 500 Milioni kutoka kwenye mkataba wa 'TV RIGHTS' ambao Azam TV waliingia na (TFF)

Pia kwenye mkataba wa Sports pesa na Yanga SC kuna kipengele kinachoeleza kuwa, kampuni hiyo itatoa Bonus ya Tsh 100 Milioni ikiwa Yanga watatwaa ubingwa.

Vilevile katika mkataba wa (GSM) na Yanga wa utengebezaji na usambazaji wa jezi kuna kipengele cha Bonus ya Tsh 100 Milioni iwapo Yanga wakitwaa UBINGWA wa ligi kuu.

Haikuishia hapo, katika mkataba wa Yanga na Taifa Gas kuna kipengele kinachoeleza kuwa, Taifa Gas watatoa Tsh 50 Milioni iwapo Yanga watatwaa UBINGWA wa ligi kuu.

Ukijumlisha pesa hizo unapata jumla ya Tsh 3 BILIONI na Milioni 750 ambazo Yanga watapata wakiwa MABINGWA wa ligi kuu.
____________________________________

Hivyo ndivyo mikataba iliivyo, sio kwamba naandika tu from no where. Mimi huwa siandiki kitu hapa bila kufanya utafiti.

Niliandika post jana ikieleza Yanga watapata Tsh 3 BILIONI na Milioni 750 iwapo wakiwa MABINGWA, baadhi ya watu wakawa wanakejeli wakidai nawalisha matango pori.
.
.
Chukua hiyo kutoka kwangu 👇

Mjinga ni yule asiyejua kitu fulani lakini akielezwa ANAELEWA. MPUMBAVU ni yule anayejifanya anajua wakati hajui na hajui kuwa hajui.
 
TEh teh,teheeeeeeeeee,koh koh koh,ngoja nikohoe kwanza mie
eti bilioni4,hahaaaaaaaaaaaa

Maaaninaaaaaaaaaaaaaa,tuwekee hako kasehemu cha huo mkataba.

Yaaani ubingwa Azam awape mil500,halafu bonus awape bil3,kawadanganye kina Manara brooo
Pole sana kwa kupitwa halafu pole ya pili ni ya kushindwa kuelewa

Yanga waliingia mkataba na Azam wakimaudhui kwa miaka 10

Source 1: Yanga yaingia mkataba wa Tsh Bilioni 34.8 na Azam Media

Source 2: Yanga yaingia Mkataba mnono na Azam Media | East Africa Television

Source3:

Source 4: Yanga na Azam Media wasaini mkataba wa Bilioni 41 – Millard Ayo TV

Source 5: Yanga, Azam Media wasaini mkataba wa Sh41 bilioni

Utachagua mwenyewe kuwa ungependa uteseke kwa source ipi

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Kocha wa yanga mwenyewe katuma cv simba nyie endeleeni kujipa moyo tu mchezaji aache kwenda simba aende utopolo walioshindwa kumlipa ntabazonkiza.
 
Nabi Aje Kufundisha Timu La Washirikina Na Vinyamkela?? Af We Bhn!, Af Nyie Mbona Mnataka Adebayor, Ramos Mara Benzema Sijui Ronaldo, Si Tumetulia Wala Hatusemi Kitu Kuhusu Targets Zenu, Lakini Sisi Kumtaka Aziz Tena Sio Andambwile Ni Ki Tu Inakuwa Nongwa Kwenu Mnapata Mshawasha Maneno Yanawatoka Kwnn Asee? Au Mnaogopa?? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
BILIONI (3) na MILIONI (750) !!

July 8, 2021,, Mtendaji mkuu wa Azam media Tido Mhando na mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla walisaini mkataba wa mashirikiano ya MAUDHUI baina ya Yanga SC na Azam TV (MEDIA PARTNERSHIP).

Thamani ya mkataba huo ni Tsh 41.64 BILIONI kwa miaka kumi (10).

Yanga watapokea Tsh 34.8 BILIONI kutoka AZAM TV baada ya makato mbalimbali. Yanga na Azam Tv watashirikiana kuandaa na kurusha MAUDHUI ya klabu ya Yanga kama ;

[emoji3502] Mazoezi ya timu.
[emoji3502] Maandalizi ya mechi
[emoji3502] Mechi za kirafiki na Exclusive mbalimbali za klabu ya Yanga kama usajili, Interviews na vitu vingine.
.
.
Klabu ya Yanga itakuwa ikipokea Tsh 200 Milioni kila mwezi kuanzia msimu huu (2021-22) hadi (2030). Pesa hiyo itakuwa ikiongezeka kila msimu.
.
.
[emoji419] Kupitia mkataba huu klabu ya Yanga itapokea BONUS ya Tsh (3) BILIONI KILA INAPOSHIKA NAFASI YA (1) AU YA (2) kwenye ligi kuu Tanzania bara.
.
.
Yanga wataendelea kupata Bonus kila wanapofanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali.
______________________________________
.
.
Ukiacha Mkataba huo wa MAUDHUI, Yanga wakiwa MABINGWA watapata Tsh 500 Milioni kutoka kwenye mkataba wa 'TV RIGHTS' ambao Azam TV waliingia na (TFF)

Pia kwenye mkataba wa Sports pesa na Yanga SC kuna kipengele kinachoeleza kuwa, kampuni hiyo itatoa Bonus ya Tsh 100 Milioni ikiwa Yanga watatwaa ubingwa.

Vilevile katika mkataba wa (GSM) na Yanga wa utengebezaji na usambazaji wa jezi kuna kipengele cha Bonus ya Tsh 100 Milioni iwapo Yanga wakitwaa UBINGWA wa ligi kuu.

Haikuishia hapo, katika mkataba wa Yanga na Taifa Gas kuna kipengele kinachoeleza kuwa, Taifa Gas watatoa Tsh 50 Milioni iwapo Yanga watatwaa UBINGWA wa ligi kuu.

Ukijumlisha pesa hizo unapata jumla ya Tsh 3 BILIONI na Milioni 750 ambazo Yanga watapata wakiwa MABINGWA wa ligi kuu.
____________________________________

Hivyo ndivyo mikataba iliivyo, sio kwamba naandika tu from no where. Mimi huwa siandiki kitu hapa bila kufanya utafiti.

Niliandika post jana ikieleza Yanga watapata Tsh 3 BILIONI na Milioni 750 iwapo wakiwa MABINGWA, baadhi ya watu wakawa wanakejeli wakidai nawalisha matango pori.
.
.
Chukua hiyo kutoka kwangu [emoji116]

Mjinga ni yule asiyejua kitu fulani lakini akielezwa ANAELEWA. MPUMBAVU ni yule anayejifanya anajua wakati hajui na hajui kuwa hajui.
Mashabiki Wa Simba Ni MBUMBUMBU.
 
Pole sana kwa kupitwa halafu pole ya pili ni ya kushindwa kuelewa

Yanga waliingia mkataba na Azam wakimaudhui kwa miaka 10

Source 1: Yanga yaingia mkataba wa Tsh Bilioni 34.8 na Azam Media

Source 2: Yanga yaingia Mkataba mnono na Azam Media | East Africa Television

Source3:

Source 4: Yanga na Azam Media wasaini mkataba wa Bilioni 41 – Millard Ayo TV

Source 5: Yanga, Azam Media wasaini mkataba wa Sh41 bilioni

Utachagua mwenyewe kuwa ungependa uteseke kwa source ipi

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app

Pole sana,kwa hyo huo mkataba wa miaka 10 ndio upewe bil 3 mwaka wa kwanza?
 
Kuna mikataba miwili tofauti ya Adam
1.Mkataba kati ya Azam TV na TFF (TV Rights)-ambapo bingwa anapata milioni 500

2.Mkataba kati ya Azam TV na Yanga-Huu unahusu haki ya maudhui yote yanahusu Yanga,yanamilikiwa na Azam na Mkataba huo ni Wa Billion almost 30 kwa miaka 10.….…....ila kuna kipengele cha Bonuses endapo timu ikichukua ubingwa inapata Bonus ya Billion 3
Sawa,tuwekeeni hako kapengere kwani bingwa kupewa mil500 hilo liko wazi,hebu tuthibitishieni hilo nalo
 
Kwa hiyo huo mkataba ikitokea yanga hajachukua taji la ligi kuu au nafasi ya pili kwa miaka 10 Yanga atapata 0?
Akili zenu ni shida sana
 
Back
Top Bottom