Mabinti endeleeni kutupenda wachaga sio wote tunaroho za uharibifu

Mabinti endeleeni kutupenda wachaga sio wote tunaroho za uharibifu

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Ushauri tu Wapendwa;
Sio wachaga wote wana roho za mateso kama matukio yanayoendelea hivi karibuni

Naomba niwahakikishie mabinti kuna makaka wazuri wenye roho nzuri sana na wanawito wa kuwa mume wa mtu na familia

Tunaombaa msitukasirikie msituchukie .mkaamua.kutuogopa bado wazuri wapo na wana wito wa familia

Mungu azidi kutukutanisha na nyie popote mnapotutafuta
Tunawahakikishia tunawapenda na yutazidi kuwapenda

Na pale tulipokosea tunaomba msamaha kwa kila mwenye mapenzi.mema na tunawahakikishia tulipodondoka tutaamka na tutasimama tena na tena

Wenu,
Mwakilishi wa Wachaga wote,
Dar es salaam.
 
Tunawahakikishia wapo tunaojua kupenda na kuwathamini mabinti
Na tutahakikisha kila mwanandoa kuanzia sasa anakua na bima kubwa ili ikitokea emergency yoyote tusiteseke kama awali
tunawapenda tutazidi kuwapenda
 
USIOGOPE KUOA MCHAGGA

Nimeona wanaume wengi mmeingiwa na hofu juu ya ndoa.

Watu wanasema "Usioe wa kabila fulani, WACHAGGA ni wauaji wa waume zao wakifanikiwa" na maneno mengine mengi. Maneno haya yamevunja ndoa nyingi kabla hata hazijaanza.

Nimekuandalia ujumbe huu ukutie moyo:

MSIKILIZE MUNGU, USISIKILIZE KELELE ZA WATU

Ndugu yangu,

Ndoa si kabila. Ndoa ni agano mbele za Mungu.

Ukioa kwa kusikiliza maneno ya watu, utaishi kwa hofu ya watu. Ukioa kwa kumsikiliza Mungu, utaishi kwa amani ya Mungu.

1. Kabila halimfanyi mtu kuwa mke mwema au mbaya.
Uovu na wema havina kabila. Mchagga mwema yupo, na wa kabila lingine mwovu yupo. Kila kabila lina malaika wake na lina wabaya wake. Usihukumu bustani nzima kwa sababu ya ua moja lililokwisha nyauka.

2. Mwanamke sahihi hutoka kwa Bwana, si kwa ukoo.
Biblia inasema: "Mke mwema hutoka kwa Bwana" Mithali 19:14.
Mungu haangalii kama ni Mchagga, Mhaya, Msukuma au Mpare. Mungu anaangalia moyo. Mtu akiwa na Mungu, Mungu humchorea mtu sahihi. Hata awe wa wapi, Mungu akisema huyu ndiye, ndiye.

3. Hofu si kutoka kwa Mungu.
Mungu hajakupa roho ya woga. Hofu ya kuoa kwa sababu ya porojo za mitandaoni na vijiwe vya kahawa itakuzuia usimkose yule Mungu aliyekuandalia. Usikubali shetani akutishe na hadithi za kusadikika.

Badala ya kuuliza "Ni kabila gani?" Anza kuuliza:

  • Je, huyu mwanamke anampenda Mungu kuliko anavyonipenda mimi?
  • Je, ana heshima, bidii na hekima ya kujenga nyumba?
  • Je, nikiwa chini, atanivumilia na kuniombea?
  • Je, amani yangu inathibitisha ndani yangu huyu ndiye?

Mke sahihi si yule asiye na mapungufu, ni yule Mungu aliyemkusudia awe safari yako ya kwenda mbinguni.

Kwa hiyo ndugu yangu, inuka. Omba. Fungua macho ya rohoni. Usioe kabila, oa mtu. Oa tabia, oa maombi, oa maono.

Mungu akiwa ndiye kiongozi wako, hatakuletea mwuaji, atakuletea msaidizi. Hatakuletea adui wa mafanikio yako, atakuletea mlinzi wa mafanikio yako.

Acha kuogopa. Anza kuamini.

"Mke mwema ni taji ya mumewe." Mithali 12:4

#Appostle Pdidy
 
Ukipata MCHAGGA wako wahi chap Ukamtolee MAHARI
WACHAGGA NI DILI
WACHAGGA NI WAPAMBANAJI
USIDANGANYIKE NDOA NI MPANGO WA MUNGU

Cc

#Chasakaa
 
Mimi niliapa wanangu wakifika umri wa kuingia kwenye ndoa waende kote ila sio uchagani. Naeza toa laana.
Aiseee dah
Poleni jamani sio wote tusameheane
 
Tuwe tu wa kweli kuna baadhi ya pisi za kichaga ni mali hatari yaani unashitukia tu imeshakuua. Mimi kwakweli pigeni kelele ila hawa mademu wa kichaga siachi
 
Ushauri tu
Wapendwa
sio wachaga wote wana roho za mateso kama matukio yanayoendelea hivi karibuni


Naomba niwahakikishie mabinti kuna makaka wazuri wenye roho nzuri sana na wanawito wa kuwa mume wa mtu na familia

Tunaombaa msitukasirikie msituchukie .mkaamua.kutuogopa bado wazuri wapo na wana wito wa familia

Mungu azidi kutukutanisha na nyie popote mnapotutafuta
Tunawahakikishia tunawapenda na yutazidi kuwapenda

Na pale tulipokosea tunaomba msamaha kwa kila mwenye mapenzi.mema na tunawahakikishia tulipodondoka tutaamka na tutasimama tena na tena

Wenu
Mwakilishi wa Wachaga wote
Dar es salaam
watachomokea wap mkuu. wakat huo huko mkoan walikuwa wanapanga folen wenyewe kukutaka
 
Aiseee dah
Poleni jamani sio wote tusameheane
Sisi kipande hii tumeoa kipande ile ya Wamasai, wale wanaosema Masai hua hawaolewi na kipande ingine hapana sio kweli tumeoa Masai na imepata watoto kubwa wainne sasa ni wakubwa yellosubhai
 
Kabila halihusiani na ubaya.Ni mtu tu alivyo na kichwa chake chenye mawazo hasi.
NB: Ila kwenye hela siwatetei.
 
Aiseee dah
Poleni jamani sio wote tusameheane
Ni kweli mkuu, upo sahihi kabisa ila tahadhari ni muhimu, na hii sio kwa wachaga tu zipo familia ni mwiko kwenda kuoa kwenye baadhi ya koo/ kabila sababu ya imani za wazee/ancestors.
 
Back
Top Bottom