Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Ukristo na uislam siyo utamaduni wa Tanzania,nimekuuliza kuhusu utamaduni wa Tanzania,bukta ni kinyume na utamaduni wa kabila lipi la Tanzania?
 
Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba
Shekhe Mohamed Abubakar,
Kwema? Mbona kwenye bar nyingi mabinti wa imani yako akina ASHURA ni wengi tu wanauza vinywaji wakiwa wamevaa vibukta na vimini unaona tu hadi kunako na husemi kitu?!!

Jeshi likianza kukumbatia dini litakuwa kitu kingine, siyo jeshi tena!
 
Ndugu Mohamed hii mada ni nzuri lakini kwa hapa JF ni kama haina uzito, kwani katika kipindi hiki tunachopita nacho nadhani badala ya uzuri wa mada hii itakuwa ni dhihaka na kebehi. Ninacho kiona michango mingi itakuwa si ya hoja bali ni mihemko ya kidini, hivyo basi ingekuwa tungeomba taasisi za dini husika zikae na vyombo vya ulinzi na usalama na viangalie jinsi gani ya kuendesha program zao kwa kuzingatia imani, utamaduni na mila za wananchi wake. Tunaposema serikali haina dini bali wananchi ndiyo wenye dini kauli tata iliyoficha na kunyima haki za wenye dini.
 
Sio lazima waende jeshi,
 
Kusema kweli mimi nilikuwa sijawahi kufahamu kwamba wanafunzi wa kike wanavalishwa bukta huko JKT hadi nilipoona hizi picha kwenye uzi wako mtoa mada.

Hii ni mbaya sana. Haiwezekani JKT wakiuke katiba kwa kisingizio cha uzaleno. Huo ni zaidi ya uwendawazimu.

Na kibaya zaidi eti wanawanyoa nywele kama wafungwa. ikiwa JKT wataendelea na upumbavu huu kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita, binti yangu bora aishie kidato cha nne kisha aende chuo cha kati na hatimaye chuo kikuu.

Kama kwenda JKT ndio tiketi ya kwenda chuo kikuu ni bora binti yangu atumie njia mbadala kufika huko kuliko kwenda kuvuliwa sketi na maafande wa JKT wanaovuta bangi na kuvalishwa bukta kwa lazima huku mapaja yote yakiwa wazi. Sikubali.

Jambo jingine la kipumbavu na kiuendawazimu linalosemekana kufanyika huko kwenye makambi ya JKT ni maafande kuwageuza watoto hawa wa kike kuwa wake zao. Hili ni jambk la hatari sana.

Ewe chuki, chukua hatua ya kumpima binti yako kabla hajaenda JKT na akirudi nyumbani mpime tena ili kujiridhisha. Kama akirudi akiwa ameharibiwa au ameambukizwa UKIMWI na maafande, fungua kesi serikali iwajibike kwa uhalifu huo.
 
Acheni mihemko tufate katiba.

Si watz wanapigania katiba mpya? Itakuwa na maana gn kama haitofatwa kama hii iliopo.

Mada uhuru wa kuabudu ndani ya katiba ni kwa ajili ya wanafunzi tu au taasisi zote ikiwemo jkt, jwtz, jeshi la polisi, magereza nk
Leta hicho kifungu kinachokataza mabinti wa Kiislam kuvaa kaputula.
 

Hata hivyo huwezi kupata majibu sahihi hadi uwe na ufahamu wa falsafa ya uongozi.

#ujamaa ni imani
Sawa ujamaa ni imani.
Ni vizuri tukifuata imani ya serikali yetu na wala sio huo upuuzi wa imani zingine.
 
Jkt ni shule ya Jeshi na wanafunzi wanatakiwa kufuata taratibu za jeshi .

Mwisho wake utataka waanze kuvaa buibui na kanzu .
 
Wahamishie Afghanistan hutojutia
 
ndugu pole kwa kuumia na
pole kwa mahaba ya dini,ninakushauri ubadilike na ufahamu kwamba dini haivaliwi kama mavazi haipo kwenye nguo bali swala la imani lipo nafsini zaidi ni vizuri ukaelewa kwamba sheria za jkt hazijaanza leo zilikuwepo tangu siku za nyuma na waliopitia huko wanalifahamu hilo pale hakuna utambulisho wa kidini maana siyo sehemu ya kupractice dini bali ni sehemu ya mavunzo ya ukakamavu kwa vijana na unavyoona hayo mavazi siyo kwamba ndiyo huwa wanayavaa kila siku na kila wakati hapana hiyo ni kwa ajili ya wakati maalumu kutegemea na programu wanayofanya..kule mazoezi ni mengi tu yapo hadi ya kujiburuza kwenye matope watavaa nguo ambazo viongozi wa mafunzo wamemeona kuwa zinafaa kwa wakati huo na wewe ama mimi siyo wakufunzi hivyo huna nafasi ya kupanga nini kifanyike kule na wakati gani
zaidi ni kwamba naona tunaingiza mahaba ya dini mahali ambapo hapastahili naomba tusiwe na mihemko kwa sababu siyo lazima mtoto wako aende jkt kama hujaridhishwa na namna yao basi mwache mwanao abaki nyumbani
likiruhusiwa hili la kwako kuingizwa jkt basi tutakuwa na jkt ambayo haina maana maana Tanzania tunayo madhehebu mengi lakini hakuna mtu anayeingia kwenye dhehebu la mwezake kuhoji imani ila tukiwa nje ya nyumba za ibada tunaheshimiana kila mtu kwa imani yake ila kwenye mambo kama haya ya jeshi siyo kweli kwamba yanahitaji kujengeana makanisa na misikiti mle ndani hapana.

nakushauri uwe mpole na usiwapige tena picha siku nyingine wanapokuwa kwenye mafunzo kwani hairuhusiwi.
 
Rubbish ๐Ÿ—‘๐Ÿšฎ๐Ÿ—‘๐Ÿšฎ๐Ÿ—‘๐Ÿšฎ
 


Jeshi ni kama serikali inayojitegemea na haina dini. Hata kuvaa misalaba nayo nje nje hairuhusiwi. Jeshi kila mtu ni sawa na ndiyo maana wanawake wananyoa nyele zao na kubaki vipara. Kwenye jeshi kuna kuuwa kwa kutetea nchi sio kutetea Mungu! Nafikiri rudi kwanza ujiulize kazi ya jeshi ni nini hasa. Na sio kwenye wanakiuka katiba!! acha vichekesho. Kama unapenda sana imani basi usimpeleke mtoto wako jeshini au akajiunge na majeshi ya kiarabu ambako atakuwa mpishi au nesi.
 
Am sure dini ni Ile sauti ambayo inatembea kichwani mwako , mawazo yako,matamanio.yako,chuki,upendo ,unavyoongea mwenyewe kichwani kinafsini mwako. Sio hizi Mambo za kufanya kwa nje ili uonekane.
Yaani Yale uyafanyao ukiwa sirini Ila Muumbaji wa mbingu na nchi anakuona unavyowaza. Jamaa wamekuwa programed kuwachukia wasio wa imani yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ