Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Wewe ndio uache mihemuko. Use your common sense. Hata kama kuna katiba lakini kuna taratibu za kufuata kila sehemu. Ndio maana waislam wote wanaosoma shule za kikristo wanafuata taratibu za shule hizo. Hijabu inaachwa getini hutaki usiende.
Tatizo hili. Kwa hiyo shule za kikristo ni taasisi za serikali. Kwa hiyo serikali hii ni ya kikristo kama ilivyo shule za kikristo.

Kwann nyie ndugu zetu hamukiri tu kuwa hili ni kosa na litarekebishwa.

tunaongea hays kwa kutilia mkazo 4R za mama. Ni wakati wa kufanya Maridhiano kama taifa. Mna pungukiwa na nini mkiridhiria iwapo mnakiri ktk hili katiba inasiginwa
 
Kiukweli ni kitu kinakera sana, dadangu alienda huko toka maisha yake ya baleghe na kujitambua hajawahi kuonekana mguu wake acha hilo paja mabega nywele ila walivyo hawana adabu wakamvalisha hivyohivyo aisee!!! Alafu wao wanafurahia hvyo kumuacha mtoto uchi ati
NI BORA LIWEKWE AZIMIO LA KUGOMEA HII KITU
 
Hao wanaotaka utengano wa majimbo hawana akili nzuri,Tanganyika ni moja katiba inayotuongoza ni moja,kingine siyo kila kitu ni cha kuiga hao walioona bora ni wao na sisi ni sisi.

Unaonaje ukabaki na mwanao ukampeleka kwenye fani zinazoruhusu hayo mavazi?dini ipo moyoni hao unaodhani wanajifunika sana kuna scenes zinafika wanayavua yote wanafanya maovu mwisho itatokea vita hapa mseme watoto wetu wasiende wataua watu.
Ndugu kwann utangulize mambo vita, wakati kinachotakiwa ni kupress the button tu.

Kwa vile katiba imekiukwa muda wote huu ni suala la kiongozi mwenye dhamana hii kutoa tamko.
 
Kiukweli ni kitu kinakera sana, dadangu alienda huko toka maisha yake ya baleghe na kujitambua hajawahi kuonekana mguu wake acha hilo paja mabega nywele ila walivyo hawana adabu wakamvalisha hivyohivyo aisee!!! Alafu wao wanafurahia hvyo kumuacha mtoto uchi ati
NI BORA LIWEKWE AZIMIO LA KUGOMEA HII KITU

Hatua ya pili tutakwenda mahakamani. Nililipeleka bakwata hili lkn wao wakanijibu mamlaka yao wanaishia mlangoni wa msikiti wa kutoka nje. Kwa hiyo hawana msaada.
 
Jeshi ni kama serikali inayojitegemea na haina dini. Hata kuvaa misalaba nayo nje nje hairuhusiwi. Jeshi kila mtu ni sawa na ndiyo maana wanawake wananyoa nyele zao na kubaki vipara. Kwenye jeshi kuna kuuwa kwa kutetea nchi sio kutetea Mungu! Nafikiri rudi kwanza ujiulize kazi ya jeshi ni nini hasa. Na sio kwenye wanakiuka katiba!! acha vichekesho. Kama unapenda sana imani basi usimpeleke mtoto wako jeshini au akajiunge na majeshi ya kiarabu ambako atakuwa mpishi au nesi.
My people. Tanzania nani Katuroga kuwa jeshi halifati katiba.

Tafuteni clip ya mkuu wa jeshi aliyestaafu alivyoingilia kati na kufata katiba.

Tafuteni clip yake ya mwisho mzee wetu huyu
 
Nikiandika kama muislamu mwanaume na niliyepitia mafunzo ya jkt kwa mujibu miaka kadhaa nyuma .

1. Niseme tu jkt/jeshi/ polisi ni kazi ambazo hazifai kwa muislamu awe wa kike au wa kiume na hii ni kiimani zaidi maana hata wanaume tulivaa pitshort kibukta ambacho hakifuniki magoti hivyo kuacha mwili uchi
maana uchi wa mwanaume ni kitovuni mpaka kwenye magoti hii ni kwa mujibu wa kidini (uislamu).

2. Muda wa ibada huwa unakosekana kutokana na ratiba zilivyo kule na pia mavazi hayaruhusu kuswalia hivyo ni ngumu kwa kijana wa kiislamu kutimiza swala zote tano kwa wakati , japo kuna watu watatumia mlango wa udhuru ila jibu langu ni kuwa udhuru haupo maana haukulazimishwa kwenda kule.

3. Kama umeona kuvuliwa nguo kwa wasichana wa kiislamu ni jambo kubwa mkuu kuna kitu inaitwa KUPIGWA TOCHI sitozama ndani zaidi ila wengi mnafahamu na kwa wale ambao hamfahamu basi jaribuni kuuliza uliza sitolielezea kiundani ila ni ukaguzi wa mwili mzima na hii ni kwa wanaume na wanawake no exception MEANING KAMA DAKTARI NI MWANAMKE ATAHUDUMIA WOTE NA KWA MWANAUME PIA HIVYO HIVYO.

4. Jeshi huwa halazimishwi mtu kwenda na hata usipokwenda hakuna atakayekufuatilia na haito affect chochote kwenye maisha yako ya kila siku hivyo sioni kama kuna ulazima wa binti au kijana wa kiislamu kwenda jeshi.

5. Ukifika kule kuna mkataba utasainishwa na kuna wiki mbili za uzalendo na kama haujiskii kubaki upo huru kuuvunja mkataba na kuondoka ndani ya hizo wiki mbili hakuna wa kukulazimisha.
Perfect , umelezea vizuri sana 💯
 
Kuna waislamu Tanzania hawajielewi utasikia tunashukuru tuna Raisi na wabunge kibao wanachosahau Pesa zao za mishahara na posho Pesa hutoka vyanzo haramu mfano hupitisha bajeti ya wizara ya fedha ambayo moja ya vyanzo vikubwa vya serikali ni Kodi ya pombe na Waziri husoma wazi bila kificho na Raisi Muislamu husaini kuidhinisha na hijabu yake kuwa hiyo bajeti ruksa kupita na Kodi za pombe zake humo ndani

Akimaliza kusaini anawahi msikitini swala tano
Dhambi kwa muislamu ni kula nguruwe. Zingine siyo dhambi
Utawakuta mabinti wa kiislamu wamevaa majuba wameacha macho tu lkn hawana bikra na hawajaolewa.
Ukiwauliza watakuambia wanajistili, sijui na baridi
 
Ni hoja nzuri tu.
Lakini jeshini siyo mskitini au kanisani kule ni kazi kazi.
Vipi kwenye michezo?
Huyo ni mchezaji wa Timu ya Morocco (Islamic country)
 
Attachments

  • images (6).jpeg
    images (6).jpeg
    28.7 KB · Views: 2
ndugu pole kwa kuumia na
pole kwa mahaba ya dini,ninakushauri ubadilike na ufahamu kwamba dini haivaliwi kama mavazi haipo kwenye nguo bali swala la imani lipo nafsini zaidi ni vizuri ukaelewa kwamba sheria za jkt hazijaanza leo zilikuwepo tangu siku za nyuma na waliopitia huko wanalifahamu hilo pale hakuna utambulisho wa kidini maana siyo sehemu ya kupractice dini bali ni sehemu ya mavunzo ya ukakamavu kwa vijana na unavyoona hayo mavazi siyo kwamba ndiyo huwa wanayavaa kila siku na kila wakati hapana hiyo ni kwa ajili ya wakati maalumu kutegemea na programu wanayofanya..kule mazoezi ni mengi tu yapo hadi ya kujiburuza kwenye matope watavaa nguo ambazo viongozi wa mafunzo wamemeona kuwa zinafaa kwa wakati huo na wewe ama mimi siyo wakufunzi hivyo huna nafasi ya kupanga nini kifanyike kule na wakati gani
zaidi ni kwamba naona tunaingiza mahaba ya dini mahali ambapo hapastahili naomba tusiwe na mihemko kwa sababu siyo lazima mtoto wako aende jkt kama hujaridhishwa na namna yao basi mwache mwanao abaki nyumbani
likiruhusiwa hili la kwako kuingizwa jkt basi tutakuwa na jkt ambayo haina maana maana Tanzania tunayo madhehebu mengi lakini hakuna mtu anayeingia kwenye dhehebu la mwezake kuhoji imani ila tukiwa nje ya nyumba za ibada tunaheshimiana kila mtu kwa imani yake ila kwenye mambo kama haya ya jeshi siyo kweli kwamba yanahitaji kujengeana makanisa na misikiti mle ndani hapana.

nakushauri uwe mpole na usiwapige tena picha siku nyingine wanapokuwa kwenye mafunzo kwani hairuhusiwi.
Ndugu hii ni nchi insyoendesha kwa katiba, Sio kama wanavyosema kuwa viongozi waneamua.

Pili ungejisomea Kodogo falsafa unaeelewa umuhimu wa imani ktk kutetea nchi na mtu mmoja mmoja.

Serikali yyt lazima iongeze na imani. Serikali ya ina imani.

lkn kubwa zaidi ubora wa serikali hutegemea imani aliyonayo mtendaji wa serikali.

Nchi hii imekuwa ikiongozwa kwa muda mrefu na tabaka moja la jamii. Kiasi kwamba maamuzi yao yaliyoegemea imani zao za asili wanadhani ndio sheria ya taasisi na serikali kuu kwa ujumla.

Ili kuendesha taasisi yyt ya serikali katiba ya nchi ndio msingi mkuu, na wala si imani ya mtendaji wa serikali.

Katiba inatoa uhuru wa wananchi wa kuabudu akiwa ktk majukumu binafsi au majukumu ya taifa.

Jkt ni taasisi inayopaswa kuheshimu katiba. Kwa kutambua hili nchi zilizoamua kuheshimu utawala bora, haki za binadamu ximeweka utaratibu wa maeneo ya kambi za kijeshi kuwapatia haki hiyo waumini wa imani tofauti kupractice imani zao.

Nchi hizo zikiongozwa na Marekani yenyewe.

Swali inakuwaje nchi kama Marekani yenye waislam wachache inawalinda waislam, masingasinga na mayahudi kupractice imani zao jeshini. Huku tz yenye idadi kubwa ya waislam ikiwabagua, na kuwadhibiti.

Tunapitwa hata na malawi.

Nilitarajia mtu kama wewe unaonekana kuwa msomi angesema tu hili suala ni fikra mpya, hatujaizoea lkn kama taifa tumefanya makosa na hivyo kosa hili la kikatiba tulisahihishe.

Na tuonyeshe uwezo wetu wa kuvumilia values za jamii zote zilizoorodheshwa ndani ya katiba tunazitekeleza kwa kuunga mkono dhana ya 4R ya mama Samia

Pitia link hizi uone mataifa ya kidemokrasia yanavyotekeleza haki hii

Police Scotland uniform to include Muslim hijab

Malawi Defence Force allows Muslim soldiers to wear hijab Malawi 24 | Latest News from Malawi

SOUTH AFRICA ARMY ALLOW MUSLIM WOMAN TO WEAR HIJAB - Google Suche

View: https://youtu.be/zddiPwicaH0?si=oDVehMbqsHZVbpLm

View: https://youtu.be/RDx2zl5li5k?si=TwW5LxcLzKEYHPPA

View: https://youtu.be/LFVeJK2ZdkQ?si=3xNDM8I5KvSnTWs1

View: https://youtu.be/vwFzn5TucuQ?si=BmHGBiZ5p2LkMIy7
 
Sio lazima waende jeshi,
si lazima ni kweli na hiyo sio mada yetu. Mada haijasema ni lazima kwa mabinti wa kiislam kwenda jkt. Mada ni jkt wafate utawala bora kwa kutekeleza sheria na haki ya uhuru wa kuabudu iliyoainishwa ktk katiba ya nchi. Kwani kuvaa mavazi ya stara ni ibada.

Tatizo watz tuko nyuma na somo la uraia. Kujua haki zetu
 
Sawa ujamaa ni imani.
Ni vizuri tukifuata imani ya serikali yetu na wala sio huo upuuzi wa imani zingine.
Hujui somo la uraia. Kwa hiyo unataka kuwalazimisha watz wafate imani ya kipagani. Wakati katiba imeapa kuwapa uhuru wananchi wafate imani zao.

Watz wengi ni bora andazi
 
Wiki hii zimetoka nafasi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kujiunga na mafunzo ya JKT.

Moja ya kitendo kinachokosa utu na kinachokiuka utamaduni wetu ni kuwavisha watoto wetu wa kike mavazi ya watoto wa kiume, nazungumzia vibukta kwa lazima.

Katiba ambayo ndio sheria mama inamlinda kila raia na imani yake kwa kutoa haki na uhuru wa kuabudu.

Kuvaa mavazi yenye stara kwa wanawake/mabinti wa kiislam ni sehemu ya ibada (kuabudu) inaolindwa na katiba.

Ndio maana wanafunzi mashuleni walipewa uhuru huo miaka ya 80 na serikali hii hii baada ya waislam kusimama umara na kutetea haki hii.

Huko JKT watoto wetu wa kiislam watavalishwa vibukta kwa jina la serikali isiyo na dini, kwa jina la uzalendo kwanza.

Kumekuwa na dhana kuwa tendo hili inafanywa kwa kwa kuwa itikadi ya nchi haina dini. Basi tunachojiuliza dhana hii kwa kuwa serikali haina dini ina maana ya kuwadhibiti wananchi wenye dini au kuwalinda?

Kudhibiti kwa kuwavua baadhi ya Watanzania imani za dini zao badala ya kuzilinda.

Ukweli katiba ya nchi ndio sheria kuu na hivyo kama kuna Sheria za JKT zinazowataka wasichana kuvaa vibukta.

Ieleweke ya kuwa sheria na amri hiyo ni batili. Kwa kuwa inakwenda kinyume na katiba ya nchi inayotoa haki ya uhuru wa kuabudu.

Hoja ya uzalendo au serikali isiyo na dini naamini ni ya tafsiri ya tabaka la sasa la watendaji chini ya Chama Cha Mapinduzi tulioamua kuwaamini na kuwachagua watekeleze matakwa yetu. Kinyume chake wameamua kutafsiri dhana hizi kwa matakwa na imani tulizonazo ambazo haziathiri imani binafsi.

Kwa miaka mingi sasa JKT imeamua kuminya wenye dini wasipractice uhuru wao wa kuabudu unalindwa na katiba.

Kwani JKT ni moja ya taasisi hizo ni zetu sisi umma.

Tunaitaja jamii, vyama vya siasa, kijamii na taasisi za dini kupaza sauti na kuwatetea mabinti hawa ambao hawana wa kuwasemea.

Kama ambavyo vijana wa kike waliruhusiwa kuvaa nguo zenye stara mashuleni kwanini katika mafunzo ya JKT wasiwe na uhuru huo.

Ni katiba, ni serikali au sheria za chuo inayolazimisha mabinti wanaohitaji mafunzo na wanaohitaji stara kuvuliwa stara zao?

Iwapo ni masharti ya serikali (JKT) hawaoni wanaisigina Katiba inayotoa uhuru wa kuabudu na kwamba kuvaa uniform maalum vitakazolinda stara zao ni haki ya kimsingi kama ambavyo nchi tena zenye waislam walio wachache wanavyoruhusiwa kutekeleza ibada hii ya mavazi kwa kuweka dressing code kwa wanaotaka kuvaa hivyo, je, hii ni dhana ya serikali au ni tafsiri za watendaji wa serikali wanavyotafsiri wao sawa na imani zao?

Kuwavua mavazi ya stara mabinti zetu ni sehemu ya Uzalendo?

Kunawataka Watanzania waelewe hili, uhuru wa kuabudu ni misingi ya haki za binadamu.

Kwanini watz tuko wa ajabu sana linapokuja suala la kuvumiliana values zetu. Kila kundi linalounda watanzania. Kwanini tulazimushwe kufata imani na values za kipagani.

Kwani Ujamaa ni imani.

imani ya Ujamaa ni upagani.

Kama dini dini ni imani
Na kama Ujamaa ni imani
Then Ujamaa ni dini.

Hivyo kusema serikali haina dini ni uongo uliotengenezwa, disinformation and unconstitutuion.

Dini ni falsafa na Ujamaa ni falsafa.

Kwanini serikali iwe na imani ambayo iwe ni lazima kwa wenye imani nyingine kuifata.

Mataifa ya kidemokrasia yanayojipambanua kusimamia haki za binadamu na uhuru wa kuabudu wameweka

GUIDE ON RELIGION AND BELIEF IN THE ARMED FORCES.

Unaweza kugoogle hii title na tuelimike

Vitani watavaa madera na nikhab?
Jehova witness nao wakitaka suti itakuwaje?
Wasabato nao wakisema wanataka natural air itakuwaje?
Marasta wakigoma kunyolewa nywele itakuwaje?'Mnatudhalilisha waislamu kila siku sisi ndio lia lia.
 
Baadhi ya Waislamu wagumu sana kuishi Kwa utengamano na watu wa Imani zingine na hata wao kwao

Wakitofautiana hata kiimani tu vita inalipuka kama ilivyo Somalia nk

Na Tanzania huitana makafiri kisa kutoamini mwezi umeandama au la utasikia huo mwezi wa makafiri wa Bakwata
 
Kama kawaida dini ya wapumbavu kila kona wanataka waingize dini pumbavu kabisa

Nilisha semaga hawa watu hawawezi ku co exit mara nyingi huwa wanataka tamaduni za dini husika ziende kwenye kila idara.....

Sasa jeshi na dini wapi na wapi
 
Kuhenyeshwa sawa lakini vile vibukta kwa watoto wa kike si sawa...ningependa na viongozi wa dini waingilie hili kati. Kuna mijitu pale inataka tu kulisha macho yao....
Hujawahi kujua jinsi vibukta vinaongeza morali, Jeshi linajitegemea haliendeshwi Kama unavyojiskia lina taratibu zake!
 
Leta hicho kifungu kinachokataza mabinti wa Kiislam kuvaa kaputula.
Ni kifungu cha 19 cha katiba. Kifungu cha pili kinachoitoa uhuru wa kuabudu. Na ibara ya 29 - 30 inayozuia mtu yyt kuzuia wengine kutekeleza haki zilizoanishwa na katiba.

Ufafanuzi.

Kuabudu ni nini.

Jamii moja inayounda watanzania wanaamini kuabudu ni kwenda ktk majumba ya ibada au kumsifia Mungu. Ktk uislam kuabudu ni kutekeleza kila amri ya Mungu. Kwa mfano kuvaa mavazi ya stara tasiyoonyeshesha mapaja, nywele za msichana wa kiislam ni ibada, ni kuabudu. Na ktk miaka ya 80 kama ulikuwepo jamii inayoamini kuamudu ni kwenda kanisani au msikitini walipanga hivi hivi wazo la watoto wa kike wa kiislam kuvaa uniform zenye sifa za kuitwa hijab. Lkn kisheria ikaoneshana yafaa wasichana kuvaa hijab.

Ndio tunachojaribu kutumia kifungu vile vile kwa wanafunzi wa mafunzo ya kijeshi na uzalendo wa kiislam, sinhasinga, wayahudu wavishwe uniform zinazikidhi sifa za kuwa ni uniform ya kiibada (kuabudu).

19. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo

(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi; na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

Masharti ya Jumla (Ib 29-30)

29. Haki na wajibu muhimu

(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
30. Mipaka ya haki na Uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu
(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
 
Vitani watavaa madera na nikhab?
Jehova witness nao wakitaka suti itakuwaje?
Wasabato nao wakisema wanataka natural air itakuwaje?
Marasta wakigoma kunyolewa nywele itakuwaje?'Mnatudhalilisha waislamu kila siku sisi ndio lia lia.
Katiba ifatwe take example Marekani.

Acheni ubinafsi hii nchi si ya wapagani keep yao na wanaowakaribia ambao yaone wamepewa haki zote.

Tukumbuke upagani ni imani kama zilivyo imani nyingine. Na ktk suala la imani watendaji wa serikali hawapaswi kutegemea imani moja na kulazimisha imani nyingine wafate kanuni za imani nyingine. Hata kama imani hiyo ni ya chama tawala.

Hakuna kulazimishana ktk imani. Kila mtu abaki na imani yake.
 
Back
Top Bottom