Mohamed Abubakar
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 984
- 1,179
- Thread starter
- #321
Shukran sana mkuu kwa kulielewa hili na imenimaliza.Kusema kweli mimi nilikuwa sijawahi kufahamu kwamba wanafunzi wa kike wanavalishwa bukta huko JKT hadi nilipoona hizi picha kwenye uzi wako mtoa mada.
Hii ni mbaya sana. Haiwezekani JKT wakiuke katiba kwa kisingizio cha uzaleno. Huo ni zaidi ya uwendawazimu.
Na kibaya zaidi eti wanawanyoa nywele kama wafungwa. ikiwa JKT wataendelea na upumbavu huu kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita, binti yangu bora aishie kidato cha nne kisha aende chuo cha kati na hatimaye chuo kikuu.
Kama kwenda JKT ndio tiketi ya kwenda chuo kikuu ni bora binti yangu atumie njia mbadala kufika huko kuliko kwenda kuvuliwa sketi na maafande wa JKT wanaovuta bangi na kuvalishwa bukta kwa lazima huku mapaja yote yakiwa wazi. Sikubali.
Jambo jingine la kipumbavu na kiuendawazimu linalosemekana kufanyika huko kwenye makambi ya JKT ni maafande kuwageuza watoto hawa wa kike kuwa wake zao. Hili ni jambk la hatari sana.
Ewe chuki, chukua hatua ya kumpima binti yako kabla hajaenda JKT na akirudi nyumbani mpime tena ili kujiridhisha. Kama akirudi akiwa ameharibiwa au ameambukizwa UKIMWI na maafande, fungua kesi serikali iwajibike kwa uhalifu huo.
Ukweli usiotakwa kusemwa kuwa kuna hisia wanajeshi wanafanya watoto wa kike kuwa ni wake zao.
Na kisaikolojia kuwavisha watoto wa kike bukta na kuwachanganya na watoto wa kiume na kuwafanyisha mazoezi magumu kunawaondokea watoto wa kike aibu na kuwaweka tayari kufanywa lolote ili mradi asiolewe mateso zaidi.
Huko mbeleni tutahitaji kama zilivyo shule za bweni za wasichana au wavulana. Na kambi hizi pia ziwe ktk mfumo huu. Hii nchi ni ya kwetu sote. Na hini ni kosa kubwa limefanywa na waumini wa dini zote kuwaachia walevi watufanyie maamuzi kwa niaba yetu.